Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Pundamilia07,
Nitaendeleza zaidi sehemu zenye utata..maanake kila naposoma yaliyoajiri huko Dodoma kama ilivyoandikwa kwenye tovuti ya CCM, ndio kabisa nashindwa hata kuwatetea krtk maamuzi mengi waliyofanya maanake kikao hicho kimevunja sheria ktk maswala mengi sana ya BUnge letu..

Yaani wamejadili sana kazi za Bunge na uendeshaji wake kinyume cha sheria kiasi kwamba Kikao hiicho kimefikia hata MAAMUZI kuhusiana na uendeshaji wa Bunge kwa wabunge wa chama hicho.. Chama kimefikia kuwahoji, kuwataka Wabunge wake ushirikiano Bungeni kwa faida ya chama. Tena basi mnapanga mikakati na kuunda team kuhakikisha wabunge wanakiwakilisha chama na sii wananchi..inatisha kuona chama kikingiza siasa zake bungeni kimabavu badala ya kuhubiri nje kwa wananchi ili wapate waumini..

Hii hatari kubwa mkuu wangu mahitimisho mengi ktk kikao hicho yanawafungia Udikteta kwa sababu kinachotumika ni mawazo ya serikali yenye chama kimoja tu. Sijui kama CCM wanaelewa nini maana ya demokrasia na tofauti zake bungeni ktk utunzi wa sheria kwani sioni tofauti mawazo yao enzi za Ujamaa (chama kimoja) na sasa hivi!..
 
Ngoja nirudi zangu kayenze mimi nikalime shamba la babu. Waarabu wa kayenze hizi siasa sasa zataka kutushinda nguvu
 
Ukweli ya yale yaliyojiri katika kikao cha NEC yanapatikana katika tovuti ya CCM http://www.cms.ccmtz.org/index.php?s...ails&newsid=50 the rest ni historia.

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

Kimsingi nilishindwa kabisa kumuelewa Kapt. John Chiligati alipokuwa anafafanua mapambano dhidi ya ufisadi. Anasema kwamba suala la kupambana na ufisadi ni sera ya chama, hivyo haipaswi mtu mmoja mmoja ama kikundi cha watu kuibinafsisha na kusema ni sera yake/yao na kuipigia chapuo kana kwamba wanachama wengine ktk chama wanaonekana hawaisemei na wala haiwahusu!
Mie nauliza, sasa kama wao (Kapt. Chiligati na wenzake wanaonyamazia ufisadi) wanapambana na ufisadi, mbona hatuwasikii bungeni wakikemea kwa DHATI? Suala la kuwaziba midomo akina Kimaro, Selelii, Kilango na Mwakyembe haliwezi kuwasaidia, waangalie kitu gani hawajaweka sawa kabla ya kufikiria kuwaadhibu wapinga ufisadi!
 
Lt Makamba ni aina ya kiongozi asiyejua wajibu wake,nafasi ya katibu mkuu inatakiwa ishikwe na mtu mwenye uwezo.Bwana Makamba kwa kutumia cheo chake cha katibu mkuu wa CCM taifa aliwazuia viongozi wa CCM mkoa wa Tabora wasimpokee Mheshimiwa Sitta lakini hakufanya hivyo kwa akina Lowassa na Chenge.

Ni ajabu na kweli kwamba Makamba bado ni katibu mkuu wa CCM taifa bila shaka muungwana hawezi kukwepa lawama kwa kukubali kuwa na katibu mkuu wa hovyo na anayejifungamanisha na mafisadi bila woga.

Mwenendo wa CCM chini ya muungwana unazidi kutuacha na maswali mengi kuliko wakati mwingine wowote.Chama kimeachwa mikononi mwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuongoza.Haijulikani rasmi kama bado CCM ni ya wakulima na wafanyakazi kwasababu juhudi zinazofanywa na uongozi wa CCM makao makuu kwasasa zimejikita zaidi kuwatetea majambazi na matajiri waliojichomeka katika safu za uongozi kwa namna ya ajabu.Ni bahati mbaya bado wapo watanzania wengi hawajagundua CCM ya kina makamba ipo kwaajili ya kuwalinda na kuwatetea mafisadi.

Mungu ibariki Tanzania iondokane na hili janga la kisiasa CCM
 
Mimi binafsi nafikiri somo kubwa tulilopata toka Dodoma ni kwamba kuna mtandao "original" ambao sasa unatishia hata madaraka ya Mwenyekiti wa CCM! Nina wasiwasi kwamba huu mtandao nyuma yake kuna kundi au tabaka fulani ya wananchi ambao wanaupa mtandao nguvu nyingi yakipesa. Fikiria kama mtu mmoja anayetuumiwa ufisadi wa Radar aliwapa UVCCM 400 million kwa uchaguzi tu, je mtu huyo (na wengine) wataacha kutumia hila ya pesa kuhakikisha umma na viongozi wake wanaopinga ufisadi wanashindwa. Kwa hali hii hata Rais wetu amekuwa "mateka" wa mtandao original na sioni atajiokoa vipi?
 
CCM imeshapoteza mwelekeo siku nyingi,hiki ni chama kinacholinda maslahi ya wachache mafisadi, marafiki na ndugu zao ndani ya chama husika na sio maslahi ya watanzania walio wengi.Kidogo kidogo maji yatajitenga na mafuta na itakuwa dhahiri kwa watanzania wote.
 
Kikwete amtelekeza Sitta
Aruhusu 'mafisadi' kumsulubu
Mpasuko mkubwa CCM waja

Na Mwandishi Maalum
MwanaHALISI

RAIS Jakaya Kikwete ameshindwa kulinda hadhi ya Spika wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.

Akiwa mwenyekiti wa chama hicho, Kikwete aliwaacha wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kumtuhumu Sitta kuwa aanatumia bunge kujeruhi chama na serikali yake.

Alikuwa mbunge wa kuteuliwa na rais, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyemkana na kumsulubu kwa kauli kali akisema "…Sitta ametwaa madaraka vibaya kwa kuahidi wabunge kuboresha maslahi yao."

"…Huyu Sitta amepata madaraka kwa rungu la ulaghai. Alihadaa wabunge kwamba wakimchagua ataboresha maslahi yao.," Ngombale alinukuliwa na mtoa habari akisema ndani ya kikao cha NEC.

Aliongeza kuwa Sitta "Amechapisha hata kitabu, tena nje ya nchi kinachoitwa, 'Bunge lenye meno.' Haya ni meno dhidi ya serikali ya CCM," amenukuliwa na akisema.

Ngombale aliongea kwa kudhamiria. Alisema "Sitta anahutubia sana Bunge kuliko mbunge mwenyewe. Anapenda wabunge wa upinzani kuliko wa CCM. Tabia yake hii, ameipandikiza hata kwa naibu spika na wenyeviti wake wa Bunge," Ngombale alinukuliwa aking'aka.

Lakini pamoja na tuhuma nyingi na nzito, wote walioongoza genge la "Kummaliza Sitta" kwa kumtoa uspika na hata kumfukuza kwenye chama, waliishia kunywea.

Naye Sitta, baada ya kusikiliza tuhuma, shutuma, kejeli, lakini na busara za rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Waziri Kiongozi wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, alipoza munkari wa wajumbe kwa njia ambayo mwanasiasa yeyote mzoefu angefanya.

Sitta alisema, "Kufanya kosa si kosa; kosa ni kurudia kosa." Hapo ndipo baadhi ya mahasimu wake walitazamana huku wakishindwa kucheka au kuendelea kununa.

Mtoa habari aliliambia MwanaHALISI kuwa hata wakati wa kutoka ukumbini, baadhi ya wajumbe walikuwa wakijiuliza, "Kwa kosa anasema nini? Kwamba angeasi na kuhama chama au kweli amekiri tuhuma alizotwishwa?"

Awali katika kikao cha Kamati Kuu cha Jumamosi na Jumapili, Sitta anaripotiwa kugeuka mbogo na kueleza kwa undani kile alichosema kinachosumbua serikali.

Mtoa taarifa alimnukuu Sitta akisema wakati "mtandao wa Kikwete" ulipokuwa unaomba ridhaa kwa wananchi, wao (akiiwemo yeye) hawakupanga kutumia nafasi hiyo kutafuta utajiri.
"Kama tunataka kuiba na kulea ufisadi, basi sawa. Lakini ni muhimu twende kwenye mkutano mkuu ili kubadilisha katiba ya chama chetu. Tukawaambie wanachama wetu, kwamba CCM imebadilika kutoka chama cha kutetea wanyonge na kuwa chama cha kulea mafisadi," alisema mtoa taarifa akimnukuu Sitta.

Kauli ya Sitta iliamsha munkari wa baadhi ya wajumbe waliokuwa wamebeba hoja kuu ya kumfukuza Sitta na wabunge wenzake waliotajwa kuwa 11ambao wanapiga vita ufisadi.

Katika kikao cha NEC ambacho kiliendelea hadi usiku wa Jumatatu, Asha Bakari Makame, makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), alisema Sitta anapasua chama na kwamba ndicho chanzo cha matatizo. Asha alisema kwa sauti ya kufoka, kuwa Sitta aondoke na "kubakisha hapa kadi yetu."

Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, akijibu hoja ya upatanishi, alinukuliwa na mtoa taarifa akisema kwamba hakuna upatanishi unaoweza kufanyika.

Alisema mgogoro uliomo ndani ya chama unatokana na makundi mawili; moja linalopinga ufisadi na lile linalounga mkono ufisadi.
"Ugomvi huu utaisha pale ufisadi utakapomalizika. Zaidi ya hapo, hakuna kinachoweza kuzungumzwa na kumaliza ugomvi wetu," alisema Mwakyembe.

Kwa mujibu wa taarifa, baadhi ya wajumbe watetezi wa Sitta walipokuwa wakiongea, zilikuwa zikisikika sauti za kuzomea, jambo ambalo lilimfanya mwenyekiti Kikwete kuingilia kati.

Kwa mfano, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz alinukuliwa akisema, "Sikujua kama huyu ana akili ndogo kiasi hiki." Ilikuwa ni wakati mjumbe mwingine, Injinia Stella Manyanya alipokuwa akitetea Spika Sitta.

Manyanya alinukuliwa akisema, "Sitta ni mmoja wa viongozi wa kupigiwa mfano nchini." Mtoa taarifa anasema baada ya Rostam kushambulia Manyanya, Nape Nnauye, aliyesikia kauli ya Rostam, alijibu kwa kusema, "Wewe usiyeelewa kinachosemwa, ndiyo mwenye akili ndogo."

Akizungumza katika siku ya kwanza ya kikao cha NEC, Nape alisema jina la Rais Kikwete linatumiwa vibaya na baadhi ya wasaidizi wake. Alisema baadhi yao wamo katika mkutano ule na kwamba rais angewakana hadharani.

Alitoa mfano wa sakata la Daniel ole Porokwa, Katibu Msaidizi wilaya ya Hanang, aliyefukuzwa kazi na Katibu Mkuu Yusuph Makamba kwa kisingizo cha "agizo kutoka kwa mwenyekiti Kikwete."

Hoja ya ufisadi iliyotajwa na Mwakyembe ilikuwa imeibuka mapema katika Kamati Kuu pale mjumbe Abdulrahman Kinana aliposimama upande wa Sitta na kusema, huku akitoa macho kuwa "Tuhuma za ufisadi zinazokabili baadhi ya viongozi ndizo zinaangamiza CCM."

Katika hali ambayo haikutegemewa, Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ngenda Kirumbi alimbeza Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginard Mengi, akisema kwanza si mwanachama wa CCM.

"Huyu Mengi si mwana-CCM. Namshangaa dada yangu Chilolo (Diana Chilolo mjumbe wa NEC), kusema kuwa Mengi ni mwanachama safi. Huyu Mengi ni mtu tu. Mimi nimekwenda hadi kwa balozi wa shina na katika tawi linalodaiwa kuwa Mengi ni mwanachama. Hajasajiliwa huko. Uanachama wake ni feki. Mimi siujui," alisema Kirumbi huku akimtolea macho Chilolo.

Miezi michache iliyopita Mengi alifanya ziara mkoani Singida na kwenye mkutano, Chilolo alimtaja kuwa mwanachama mzuri wa CCM. Kwenye mkutano, Mengi alichanga Sh. 100 milioni kwa ajili ya Saccos ya akinamama.

Sitta amebaki na nafasi yake ya spika na amebaki na kadi yake. Wachunguzi wa mambo wanasema inawezekana hazikuchukuliwa hatua dhidi yake kwa vile walihofia angechukua uamuzi mkali wa kuhama chama ambao ungekiumiza.

Mjadala wa kumsulubu Sitta ulitokana na mada iliyowasilishwa ndani ya vikao ambayo ilihusu hali ya kisiasa nchini, ndani ya CCM na nje ya chama hicho.

Naye mwenyekiti Kikwete,pamoja na kusema kuwa anampongeza Sitta kwa ujasiri wake, alionyesha wasiwasi wake jinsi spika anavyoendesha shughuli zake.

Alisema mambo ya ufisadi wanayojadili sharti iwe kwenye vikao vya chama na siyo bungeni; kwani yakipelekwa bungeni wanakuwa wameifanyia kazi kambi ya upinzani.

Kamati Kuu imeunda kamati ndogo ya watu watatu – Ali Hassan Mwinyi, Pius Msekwa na Abdulrahman Kinana kutafuta mahusiano kati ya bunge na kamati ya wabunge ya CCM.
Ukiacha mpambano huo kati ya Sitta na kundi zima la CCM, kitendo cha Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kutohudhiria vikao hivyo kuanzia CC hadi NEC, nacho kilizua maswali mengi miongoni mwa wajumbe.
 
"Kufanya kosa si kosa; kosa ni kurudia kosa."

This will result into an endless iteration, ambayo haitatoa kosa.

Whatever you do, whatever can be categorized as kosa, can be looped back in the iteration.

Utterly ridiculous thinking.
 
Mtoa taarifa alimnukuu Sitta akisema wakati "mtandao wa Kikwete" ulipokuwa unaomba ridhaa kwa wananchi, wao (akiiwemo yeye) hawakupanga kutumia nafasi hiyo kutafuta utajiri.
"Kama tunataka kuiba na kulea ufisadi, basi sawa. Lakini ni muhimu twende kwenye mkutano mkuu ili kubadilisha katiba ya chama chetu. Tukawaambie wanachama wetu, kwamba CCM imebadilika kutoka chama cha kutetea wanyonge na kuwa chama cha kulea mafisadi," alisema mtoa taarifa akimnukuu Sitta.

SITTA CCM sio mama wala baba yakee..sasa simwelewiiii...
 
Tatizo la Dodoma ni kumbwa. Kama chama cha CCM kimeshindwa kuzima mafisadi na wao kuzidi kulindana sioni jinsi gani Tanzania inaweza kupata mapinduzi ya haraka. Nasema hivyo kwa kuwa naamini kuwa kuna matabaka matatu ya wananchi hapa Tanzania. Kuna lile la Watawala la wenyenazo na wanaoshika hatamu na wanaelewana fika. Hawa wanalindana kwa udi na uvumba. Wanaweze kuwa wanasikika wakipiga kelele za kupingana mchana lakini usiku wanakunywa wiski pamoja. Hawa ni ving'ang'anizi wa madaraka na wana fedha nyingi ingawa ni wachache. Kundi la pili ni la wanazuoni wasomi na vijana ambao wanaupeo wa kulinganisha mambo. Hawa wanataka maendeleo ya kweli wanaona jinsi nchi inavyoliwa na jinsi nchi nyingine pamoja na kuwa na rasilimali ndogo zinavyo pinga hatua kimaendeleo...Tazama nchi za Asia hawa kwenye karne iliyopita, walikuwa hohehahe kama sisi. Lakini sasa we acha tu!!.Kundi hili linajumui
sha wanadini wasomi ambao wanachukia ufisadi na utawala gandamizi hata kuamua kutoa waraka......Kundi la Tatu ambalo ndilo la wengi ni lile la walala hoi, masikini, wavujajasho ambao wananunuliwa na kudanganywa na pesa wakati wa uchaguzi. Hawa wanauza utu wao kwa sababu ya njaa...Bado wako kwenye usingizi kuwa bila CCM nchi itaenda pabaya wanahofu hata vivuli vyao..Kwa hiyo wanawapa uongozi watu wale wale mafisadi wenye uwezo mkumbwa kwa kutegemea kula leo na kesho. Hapa ndipo kwenye kazi.. bila hawa hatuwezi kuwa na mapinduzi ya kweli ili kuleta maendeleo ya haraka na haki kwa wote..Hili tabaka la watu wa tatu linataka elimu kwelikweli ili Tanzania iweze kupata maendeleo...Cry my beloved Country....
 
Tatizo la Dodoma ni kumbwa. Kama chama cha CCM kimeshindwa kuzima mafisadi na wao kuzidi kulindana sioni jinsi gani Tanzania inaweza kupata mapinduzi ya haraka. Nasema hivyo kwa kuwa naamini kuwa kuna matabaka matatu ya wananchi hapa Tanzania. Kuna lile la Watawala la wenyenazo na wanaoshika hatamu na wanaelewana fika. Hawa wanalindana kwa udi na uvumba. Wanaweze kuwa wanasikika wakipiga kelele za kupingana mchana lakini usiku wanakunywa wiski pamoja. Hawa ni ving'ang'anizi wa madaraka na wana fedha nyingi ingawa ni wachache. Kundi la pili ni la wanazuoni wasomi na vijana ambao wanaupeo wa kulinganisha mambo. Hawa wanataka maendeleo ya kweli wanaona jinsi nchi inavyoliwa na jinsi nch nyingine pamoja na kuwa na rasilimali ndogo zinavyo pinga hatua kimaendeleo...Tazama nchi za Asia hawa kwenye karne iliyopita, walikuwa hohehahe kama sisi. Lakini sasa we acha tu!!.Kundi hili linajuisha wanadini wasomi ambao wanachukia ufisadi na utawala gandamizi hata kuamua kutoa waraka......Kundi la Tatu ambalo ndilo la wengi ni lile la walala hoi, masikini, wavujajasho ambao wananunuliwa na kudanganywa na pesa wakati wa uchaguzi. Hawa wanauza utu wao kwa sababu ya njaa...Bado wako kwenye usingizi kuwa bila CCM nchi itaenda pabaya wanahofu hata vivuli vyao..Kwa hiyo wanawapa uongozi watu wale wale mafisadi wenye uwezo mkumbwa kwa kutegemea kula leo na kesho. Hapa ndipo kwenye kazi.. bila hawa hatuwezi kuwa na mapinduzi ya kweli ili kuleta maendeleo ya haraka na haki kwa wote..Hili tabaka la watu wa tatu linataka elimu kwelikweli ili Tanzania iweze kupata maendeleo...Cry my beloved Country....
 
Hivi mzee malecela na mama anna kilango wangekuwepo, ingekuwaje?

Hivi wenyeviti hawa tunaosikia wanahofu sana mzee jm wangezungumza kama walivyofanya huku wakijua jm yupo kambi ya six? Natafakari..
 
CCM imeshapoteza mwelekeo siku nyingi,hiki ni chama kinacholinda maslahi ya wachache mafisadi, marafiki na ndugu zao ndani ya chama husika na sio maslahi ya watanzania walio wengi.Kidogo kidogo maji yatajitenga na mafuta na itakuwa dhahiri kwa watanzania wote.
Mimi ninayo hamu ya kuona majibu ya hao mabingwa kubwabwaja kesho ndani ya magazeti!
 
Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, watakapopatana utakuwa na cha kuvuna
 
Ukweli ya yale yaliyojiri katika kikao cha NEC yanapatikana katika tovuti ya CCM http://www.cms.ccmtz.org/index.php?s...ails&newsid=50 the rest ni historia.

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

( Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

Ndugu Pundamilia07,

Kama kweli unaamini kuwa yaliyojiri huko kikaoni ni kama ilivyoripotiwa hapo kwenye tovuti ya CCM, basi Spika Sita asingeweza kuwavaa Makamba na Chiligati kama ilivyoripotiwa hapa chini. Ndiyo maana watu tnasema kuwa tamko la CCM siyo la kuaminika kabisa, na hii inajionyesha pia katika sera zao, kwani waliahidi kuwa serikali ingepambana na rushwa hadi kuundwa kwa Tume kiinimacho ya Warioba lakini ilipofika utekelezaji wakaishia mitini.

Sitta afyatuka tena
• Amshukia Makamba, Chiligati wanaomshambulia nje ya NEC

na Mwandishi Wetu, Tabora

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta, amesema anakerwa na kauli za upande mmoja zinazoendelea kutolewa na viongozi wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadhi ya wajumbe wa Halmashari Kuu ya chama hicho (NEC), badala ya kusubiri ripoti ya kamati iliyoundwa na NEC, imalize kazi yake.
Sitta ambaye hii ni mara yake ya pili kuzungumza hadharani tangu aliposulubiwa na NEC, mjini Dodoma wiki moja iliyopita, alisema hayo jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika jimboni kwake Urambo, mkoani Tabora.
Ingawa hakuwataja majina, lakini ni wazi kwamba Sitta alikuwa akimlenga Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Yusuf Makamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Kapteni John Chiligati na baadhi ya wajumbe wa NEC ambao kwa nyakati tofauti, wamekaririwa na vyombo vya habari wakitetea uhalali wa CCM kumshughulikia Sitta na wabunge wanaojifanya wapiganaji wa vita dhidi ya ufisadi wakati wa mkutano wa NEC.
"Nilitarajia watu wa makao makuu ya CCM, kuzingatia na kusubiri uamuzi wa kamati iliyoundwa na NEC ambayo inaongozwa na mzee Mwinyi pamoja na wajumbe wengine, hivyo si busara kwa namna yoyote kwamba kama hutaki malumbano, kwanini unaendelea kutoa maneno?" alihoji Sitta.
Sitta ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akiandamwa na kashfa mbalimbali, huku akijizolea umaarufu kutokana na msimamo wake wa kuliendesha Bunge kwa stahili yake ya viwango, alisisitiza kuwa hataki kujibu lolote, lakini anakerwa na hali ya malumbano inayoendelea sasa.
"Mimi nadhani sasa tuache maneno na kejeli nje ya NEC wakati tayari kuna kamati imeundwa kuchunguza malumbano ndani na nje ya Bunge, ningeshauri watu wa makao makuu ya chama, waiachie kamati hiyo ifanye kazi yake ili ijue tatizo, kama ni mimi au kama kuna tatizo pana zaidi," alisisitiza.
Kuhusu yaliyotokea ndani ya NEC, Sitta alisema kuna kundi la watu linalojaribu kumwekea maneno mdomoni ili kumletea picha mbaya mbele ya jamii na kuonyesha kwamba hafai.
Akitolea mfano wa baadhi ya maneno aliyodai amewekewa mdomoni na kundi hilo la wabaya wake, ni pamoja na kauli kwamba aliomba radhi ndani ya kikao cha NEC, na kwamba kamati iliyoundwa ni kwa ajili ya kuchunguza mwenendo wake.
"Hayo yamekolezwa tu na baadhi ya magazeti, mimi daima nitasimamia katika ukweli na niwaambie tu kwamba tume iliyoundwa ipo kwa ajili ya kusuluhisha makundi yanayohasimiana ndani ya chama, si kwa ajili ya uendeshaji wa Bunge,"
"Mimi sikuomba radhi na kama niliomba, niliomba kwa kosa lipi? Mimi sikuwa na tuhuma yoyote na kama ingekuwapo, wangeipeleka kwenye Kamati ya Maadili, kwani ndani ya CCM, upo utaratibu wa kumtuhumu mwanachama pamoja na kumpelekea barua inayoonyesha tuhuma zake, mimi sikuletewa barua yoyote kwamba ninatuhumiwa kwa yanayoenezwa," alisema Sitta.
Kwa mujibu wa Sitta, kamati iliyoundwa itakuwa na kazi ya kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wabunge wa CCM ili kujua matatizo yao, jambo ambalo litasaidia kujua kiini cha malumbano ili kuchukua hatua za kudhibiti hali hiyo.
Akizungumzia madai ya NEC kwamba amekuwa akipanga watu wa kuzungumza bungeni, Sitta alisema madai hayo si ya kweli, kwani kila mbunge amekuwa akifuata utaratibu ambao ni kujaza fomu kwa Katibu wa Bunge, ambaye naye humpelekea Spika huku kila kitu kikiwa kimekamilika.
"Zipo fomu za kuchangia mjadala, ndizo zinatumika kwa wabunge wanaotaka kuchangia mjadala, hivyo mimi siwezi kujua mbunge anataka kuchangia nini au kwenye swali la nyongeza anataka kuongeza nini," alisema Sitta.
Juzi Sitta aliwasili mkoani hapa na kuweka bayana msimamo wake kwamba ataendeleza kasi ile ya mapambano dhidi ya ufisadi, pasipo kutetereka.
Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika viwanja vya CCM mjini Urambo, Sitta alisema yeye ni mzima wa afya na yuko imara na kusisitiza kuwa ataendelea na kasi ile ile.
Hivi karibuni, Makamba alisema chama hicho kina haki ya kumhoji Sitta na wabunge wote wa chama hicho, kwani wote ni mali ya chama hicho tawala.
Alipoulizwa juu ya mkanganyiko wa kauli mbili za viongozi wa juu wa chama hicho, Chiligati na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda, Tambwe Hizza, zilizotofautiana, Makamba alisema kauli halali ya chama ni ile iliyotolewa na Chiligati.
Wakati Makamba akitamba kuwa chama hicho kina haki ya kumhoji Sitta kama kilivyofanya katika vikao vyake vilivyopita, wiki iliyopita Tambwe alitoa tamko kwa vyombo vya habari linaloonyesha dhahiri kupindisha tafsiri ya maamuzi ya vikao hivyo, baada ya maamuzi hayo kuonekana kupata upinzani mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali nchini.
Katika tamko hilo, Tambwe alisema vikao hivyo havikujadili ajenda yoyote iliyowahusu Sitta na wabunge wenzake, wala iliyomhusu Makamba, aliyedaiwa kuwa ilikuwa nusura ang'olewe.
Wiki moja iliyopita, Sitta alibanwa ndani ya NEC na ilidaiwa aliomba radhi na kunusurika katika hatari ya kupoteza uanachama.
Hatua hiyo ya Sitta kuomba radhi ilikuja baada ya wajumbe takriban wote wa vikao viwili vya juu vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) vya chama hicho kujenga hoja za kumshambulia, wakipinga namna anavyoliendesha Bunge katika mwelekeo wa kukidhalilisha chama hicho na serikali yake.
Tukio hilo baya kabisa kuwahi kumfika Sitta ambaye amekuwa akijinadi kuwa ni spika wa kasi na viwango, lilihitimishwa na uamuzi wa NEC kuunda kamati maalumu kuchunguza kiini cha kufikia hapo.
Kamati hiyo maalumu inaongozwa na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na wajumbe wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa na mwanasiasa mkongwe, Abdulrahman Kinana.
Kwa mujibu wa habari hizo, mwelekeo wa wana CCM hao kutaka kumwadhibu Sitta, ambaye katika siku za hivi karibuni amejizolea umaarufu wa kisiasa ndani na nje ya Bunge, hata kuwa na uwezo wa kumnyoshea kidole mtu au taasisi yoyote, ulianza kujitokeza tangu wakati wa kikao cha Kamati Kuu mjini Dodoma.



http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=8034






- Ukweli ni kwamba hata hiyo kamati ya kina Mwinyi iliyoundwa na NEC nayo ni ukiukaji wa sheria ya Jamhuri, kama hiyo kamati ikifanya kweli walichotumwa basi ni haki kabisa kwa wananchi kuwafikisha kwenye mkono wa sheria,

- Na ikibidi kumu-impeach Mwenyekiti wa CCM, aliyeruhusu ambaye pia ni rais wa Jamhuri.


Respect.


FMEs!

Mkuu FMES,

Uko sahihi kabisa. Inaelekea watu hao wa CCM-NEC hawajui mamalaka aliyonayo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

(1) Hata wakimtoa kwenye CCM, yeye ataendelea kuwa Spika hadi Bunge limalize kipindi chake kwa vile kisheria Spika hahitajiki kuwa chini ya mwavuli wa chama chochote.

(2) Spika ana madaraka yake kuwaita Bungeni (subpoena) wana CCM-NEC wote walionigilia madaraka ya Bunge na kuwaadhibu kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kuwatupa gerezani. Adhabu itolewayo na spika haiwezi kukatiwa rufaa mahala popote.

(3) Spika ana madaraka ya kuanzisha motion ya kum-impeach na kumwondoa madarakani rais wa jamhuri ya Muungano. Rais hana ubavu wa kumwondoa spika madarakani labda avunje bunge zima ili wote (pamoja na rais mwenyewe) waanze upya.
 
Ndugu Pundamilia07,

Kama kweli unaamini kuwa yaliyojiri huko kikaoni ni kama ilivyoripotiwa hapo kwenye tovuti ya CCM, basi Spika Sita asingeweza kuwavaa Makamba na Chiligati kama ilivyoripotiwa hapa chini. Ndiyo maana watu tnasema kuwa tamko la CCM siyo la kuaminika kabisa, na hii inajionyesha pia katika sera zao, kwani waliahidi kuwa serikali ingepambana na rushwa hadi kuundwa kwa Tume kiinimacho ya Warioba lakini ilipofika utekelezaji wakaishia mitini.










Mkuu FMES,

Uko sahihi kabisa. Inaelekea watu hao wa CCM-NEC hawajui mamalaka aliyonayo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

(1) Hata wakimtoa kwenye CCM, yeye ataendelea kuwa Spika hadi Bunge limalize kipindi chake kwa vile kisheria Spika hahitajiki kuwa chini ya mwavuli wa chama chochote.

(2) Spika ana madaraka yake kuwaita Bungeni (subpoena) wana CCM-NEC wote walionigilia madaraka ya Bunge na kuwaadhibu kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kuwatupa gerezani. Adhabu itolewayo na spika haiwezi kukatiwa rufaa mahala popote.

(3) Spika ana madaraka ya kuanzisha motion ya kum-impeach na kumwondoa madarakani rais wa jamhuri ya Muungano. Rais hana ubavu wa kumwondoa spika madarakani labda avunje bunge zima ili wote (pamoja na rais mwenyewe) waanze upya.

Nafikiri hoja yako kuhusu uspika na uanachama si sahihi japo sina uhakika halisi wa mambo.

Rais si mbunge lakini akijivua uanachama wa ccm outomatically na urais unakoma hii ni kwa sababu aligombea urais kwa ticketi ya chama.Na hisi ndivyo vivyo kwa spika.
 
Aliongeza kuwa Sitta "Amechapisha hata kitabu, tena nje ya nchi kinachoitwa, 'Bunge lenye meno.' Haya ni meno dhidi ya serikali ya CCM," amenukuliwa na akisema.
Duuh, fanya kosa lolote ila documentation huwa inawatesa sana watu wababaishaji. Na kwa usemi huu wa Kingunge ndo maana sishangai kuona hakuna vitabu vya yanatokea Tanzania, even the basic history of what we had done during the liberatio of aFRICA.
Dawa yao hawa ni kuandika vitabu tena vingi vya kila linalofanyika ili na vizazi vijavyo visome na kujua madudu tunayoyalinda baada ya kuyafanya
 
Kingunge bwana ni mshenzi tu wa tabia mzee yule .Siku zote akiwa Bungeni huwa amelala hana maana ila huko kwenye CC na NEC yao huko macho na hata kulia lia na waraka .Shame on him na akifa ataacha legacy yake ni ufisadi .JK ku comment on debate ya mafisadi Bungeni kwamba iwe kwenye vyama sijui kama inawezekana .Wafanye basi kiwe Chama kimoja na wasiwe wana enda LIVE na kuruhusu waandishi maana yote yatajulikana .Halafu mnasema JK ana nia ya kupambana na rushwa na ufisadi .You are not serious hakika .
 
Nafikiri hoja yako kuhusu uspika na uanachama si sahihi japo sina uhakika halisi wa mambo.

Rais si mbunge lakini akijivua uanachama wa ccm outomatically na urais unakoma hii ni kwa sababu aligombea urais kwa ticketi ya chama.Na hisi ndivyo vivyo kwa spika.


Ingawa mtu ambaye ni mwanachama wa chama chenye wabunge wengi ana nafasi nzuri ya kuchaguliwa kuwa spika, hakuna ulazima wowote wa mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa ili kuchaguliwa kuwa spika. Nadhani kuna mantiki katika hilo.

Wabunge na raisi huomba kura kwa wananchi wakiwaahidi kutekeleza sera za vyama vyao, kwa hiyo wakipoteza uanachama wa vyama vyao hivyo basi wanakuwa hawana sifa za kutekeleza sera walizoahidi kwa wananchi, ndiyo maana wanapoteza viti vyao pia. Kwa upande wake, spika haombi kura kwa ahadi ya kutekeleza sera za chama chochote; kwanza spika siyo lazima awe mbunge.

Kama spika anatakiwa kuwa mwanachama wa chama fulani basi labda sheria hiyo imebadilishwa siku za hivi karibuni tu, kwani nakumbuka kuwa mwaka 1995 na 2000 kuna watu kadhaa kutoka mitaani tu waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ambayo wakati huo ilikuwa inachukuliwa na Msekwa.
 
Back
Top Bottom