Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Wakuu lazima tukumbuke kuwa NEC ni chombo muhimu sana kwa Tanzania, inasikitisha sana kuwa membership ya NEC ya sasa inataia shaka sana. Kuna wajumbe wengi wa NEC ambo hawaqualify au mbali ya sifa ya kuwa na umri unaotakiwa na kuwa wanachama watiifu wa CCM, hawana sifa ya kutosha kuwa na uwezo wa kufanya judgement na kutambua kuwa statements, comments na judgement zao zina umuhimu mkubwa sana kwa maendeleo ya Tanzania. Naona hilo ni kosa moja kubwa tumefanya kuufanya ujumbe wa NEC ununulike kwa pesa.
Inaonekana hata jinzi kikao cha NEC kinavyoendeshwa imebadilika sana ikilinganishwa na kipindi ambacho members wengi walikuwa watu serious, na maslahi ya taifa yalikuwa mbele kuliko maslahi binafsi.
 
Ili kuepukana na haya ni lazima katiba ya tanzania ibadilike na kumfanya Mbunge / spika kuwa mtu huru kwa kumtumikia mpiga kura wake na sio chama chake cha siasa.

Hicho ni kizungumkuti cha katiba. Kwani Spika/ wabunge wanawajibika kwa chama chao na sio wananchi waliowachagua.

Kikatiba inaruhusiwa, na ndio maana wengi wanalilia mgombea binafsi lakini ikitekelezwa hapa TAnzania hiyo ndio itakuwa mwisho wa CCM.

KUna kipindi Sitta mwenyewe alisimamia kidedea kupinga mgombea binafsi naona sasa atajua ni kwanini kipindi kile wajuvi walitaka tuwe na mgombea binafsi.

KUna haja ya kubadilisha vigezo vya kuwa member wa NEC.
Kama kuna member ana list ya wajumbe wa NEC naomba aiweke hapa tujue kama NEC in comprise vichwa au mkusanyiko tu wa watu.
 
Last edited:
Pole Bwana Ngurumo!

Bwana Ngurumo Pole!

Nimesoma hivyo vitisho vya wanaojifanya "kikosi chenyewe". Nadhani ni baadhi ya watu wanaotumiwa na watu waliotikiswa na makala zako za Mswali magumu na wala hawawakilishi msimamo wa Serikali kama wanavyotaka wewe na sisi wasomaji tuamini. Serikali yetu, pamoja na mapungufu yaliyopo, siku zote imekubali upinzani na hata mara moja haijatumia vitisho vya kuwaangamiza ili kuwanyamazisha wanaoikosoa. Wako watu ambao wamewataja kwa majina hata mafisadi...makala zako ndizo iwe nongwa??? Wamejiuzulu mpaka Mawaziri sasa iwe hao nyang'ao! Wangekuwa wametumwa na Serikali watakuitaje "mpambane kwenye jukwaa la siasa" kama unataka kushindana nao? Tena watakubembelezaje eti ukitaka usalama wako wawatume watu mkubaliane? Nadhani imefika wakati watu tukakubali kukosolewa kwa maoni tofauti na hatimaye kupokea changamoto tunazopata na kuzifanyia kazi kuliko vitisho. Huo ndio ustaarabu na ujasiri!!!Wanasema "makaburi ya Kinondoni hayajashiba" huenda wao wenyewe ndio watakuwa wa kwanza kuingia humo kabla yako. Dunia wote tunapita... Ukweli tu ndio utadumu!!!! Uoga wa kufa njaa unawasumbua. Hawajui kwamba hata kwa kutumia Internet wanaweza kukamatwa na kufikishwa katika mkono wa sheria? Serikali gani itawatuma kufanyavitu vya kijinga namna hii!


- Hata ndugu yangu Ngurumo naye alishatishiwa nao huu ujumbe wa nonsense!, naona hawa wameshikwa pabaya na wana wasi wasi sana na ushindi wao huko NEC, sasa dawa ni kuendelea kuwatwanga tu mpaka kieleweke!

Respect.


FMEs!
 
Wakuu lazima tukumbuke kuwa NEC ni chombo muhimu sana kwa Tanzania, inasikitisha sana kuwa membership ya NEC ya sasa inataia shaka sana. Kuna wajumbe wengi wa NEC ambo hawaqualify au mbali ya sifa ya kuwa na umri unaotakiwa na kuwa wanachama watiifu wa CCM, hawana sifa ya kutosha kuwa na uwezo wa kufanya judgement na kutambua kuwa statements, comments na judgement zao zina umuhimu mkubwa sana kwa maendeleo ya Tanzania. Naona hilo ni kosa moja kubwa tumefanya kuufanya ujumbe wa NEC ununulike kwa pesa.
Inaonekana hata jinzi kikao cha NEC kinavyoendeshwa imebadilika sana ikilinganishwa na kipindi ambacho members wengi walikuwa watu serious, na maslahi ya taifa yalikuwa mbele kuliko maslahi binafsi.

- NEC haitakiwi kuwa powerful body katika Jamhuri yoyote inayofuata ubepari kama yetu, hapa kinachofanyika ni ubabaishaji na wizi tu, wanajaribu ku-hold on na mawazo ya Mwalimu kuwadanganyia wananchi kwamba CCM bado ni ile ile ya zamani, lakini ukweli ni kwamba hii NEc sasa umejaa wezi wengi sana.

- Mtu anatumia Millioni 20 kutafuta Uenyekiti wa CCM WA Mkoa, hivi mshahara wake ni hela ngapi kwa Mwezi? kwamba atarudisha hela zake in three months?

Respect.


FMEs!
 
duh! yaani ukweli wenyewe utoke kwa Tambwe Hiza? Pundamilia07 stop jokes please, au wewe ndo Tambwe maana comments siku zote zimekaa kipropaganda sana.

mkuu, mimi binafsi nilimsikia Mhe. John Chiligati (msemaji wa CCM) akikiri kwamba spika alishambuliwa kwa sababu bunge limekuwa kama commedy na spika kama kiongozi wa bunge amewaachia na wakati mwingine naye anawa-support. Chiligati aliongea hayo mbele ya waandishi wa habari na bbc/swahili walirusha hewani.

achana na propaganda za Tambwe. Kama wewe unaipenda kweli CCM basi kubali ukweli na muone namna ya kusafisha hali ya hewa lakini siyo kukataa ukweli au kujitahidi kuwadanganya wananchi kwani ndo mnazidi kupoteza heshma na kuonekana wasanii tu.

Mkuu Nemesis,
Moja kati ya sifa kuu ya CCM ni jinsi ilivyo na uwezo wa kujadili mambo yake kwa mapana na marefu katika vikao vyake halali kabisa kwa mujibu wa katiba ya CCM.
Kwa siku kadhaa tumeshuhudia upotoshaji mkubwa katika JF juu ya nini kiliendelea ndani ya kikao cha NEC. Si nia yangu kurudia uwongo huo uliofanywa kwa lengo la kutoa picha tofauti na jinsi kikao hicho kilivyofanyika.
Taarifa rasmi za kikao cha NEC ya CCM zimeshatoka na maelezo yako very clear na yameonesha dhahiri nia na malengo ya mpotoshaji aliyekuwa anamwaga 'dataz' hapa za kwa sababu zake anazozijua yeye mwenyewe.
Nadhani ukihitaji kupata maelezo ya kweli ambayo yana source ambazo ni za kuaminika nenda katika http://www.cms.ccmtz.org/index.php?section=home hapo utapata habari kamili na wala si majungu.
Mleta 'dataz' si mwanaCCM anapata taabu gani kuhangaika kutafuta habari mikutano ya CCM? lengo lake ni nini kama siyo kutafuta habari za uwongo?
CCM ni chama tawala na ambacho kimepewa dhamana ya kuendesha serikali, pia CCM ndiyo chama chenye wabunge wengi katika bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania. CCM kama chama tawala kina haki na wajibu wa kusimamia masuala yote muhimu ya nchi hii kama ambavyo kingekuwa chama tawala kingine chochote.
Anaetaka kuendelea kusikiliza upotoshaji aendelee, 'ruksa' lakini treni la ukweli litamuacha na asije akalalamika hapo baadae.

Kwa kukurahisishia, soma maelezo rasmi ya yale yaliyojiri katika kikao cha NEC 16 - 17 Agosti 2009.


HALMASHAURI KUU YAAZIMIA MSHIKAMANO ZAIDI NDANI YA CHAMA

UTANGULIZI


Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya Mkutano wa kawaida tarehe 16-17 Agosti, 2009 chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika mkutano huu Halmashauri Kuu imejadili masuala mbali mbali kuhusu hali ya kisiasa nchini, maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura, pia imefanya uteuzi wa wagombea katika nafasi mbalimbali.

Baada ya kujadili masuala hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya maamuzi yafuatayo:-

1. MAANDALIZI YA UCHAGUZI
(a) Serikali za Mitaa
Halmashauri Kuu ya Taifa imepitisha ratiba ya CCM kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa; kwa mujibu wa ratiba hiyo muda wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea wa CCM kwa uongozi wa Vitongoji, Serikali za Vijiji na Mitaa ni toka tarehe 10/8/2009 hadi 20/8/2009.
Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito kwa wana CCM na wapenzi wa CCM katika ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Mitaa wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa kuzingatia ratiba ya CCM na pia ratiba ya wasimamizi wa Uchaguzi huu (TAMISEMI).

Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imewahimiza wana CCM na wapenzi wa CCM wajitokeze kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kuanzia tarehe 4/9/2009 hadi 25/9/2009 na kwamba muda ukiwadia wajitokeze kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi hapo tarehe 25/10/2009.

(b) Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura - Pemba

Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kupokea taarifa kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Kisiwani Pemba, imetoa wito kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ihakikishe zoezi hilo linasimamiwa kwa makini, na liendeshwe kwa haki na kwa utulivu; na kwamba Serikali ya Mapinduzi ihakikishe kwamba kila mwenye haki na sifa ya kujiandikisha anapata haki hiyo, na wale wasio na sifa wasiruhusiwe kujiandikisha.

Kimsingi zoezi hili sharti liendeshwe kwa kuzingatia sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na sio vinginevyo.

2. KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI

Halmashauri Kuu ya Taifa imetafakari upya mapendekezo yake ya awali kuhusu utaratibu wa kuongeza idadi ya wanawake katika Bunge la Muungano na katika Baraza la Wawakilishi. Mapendekezo mapya ni kama ifuatavyo:-

(a) Kwamba kwa kuwa idadi ya Wabunge wote kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 66(1)(b) ni 249, viti asilimia arobaini (40%) itengwe kwa ajili ya wanawake, yaani viti 100.

(b) Kwamba ukomo wa viti Bungeni ubaki 360, hivyo pendekezo hili litaongeza idadi ya viti kutoka 323 vya sasa hadi 349, na vitabaki viti 11 kufikia ukomo wa viti (360) Bungeni. Hali hii inawezesha Tume ya Uchaguzi kuongeza idadi ya majimbo mapya 11.

(c) Utaratibu wa asilimia 40 utakapotumika utawezesha kupatikana kwa Wabunge Wanawake 100 kwa viti maalum pekee, idadi ambayo ikijumulishwa na wa kuchaguliwa ambao kwa sasa ni 18, watano wa kuteuliwa na wawili kutoka Baraza la Wawakilishi, tutapata Wabunge wanawake 125. Kiwango hiki ni sawa na asilimia 50 ya Wabunge wote waliotajwa kwenye Ibara ya 66(1) (b) ya Katiba.

(d) Ili kufikia lengo la kupata wabunge wanawake 50%, wanawake hawana budi kushindana kwa bidii katika majimbo. Kwa hali hii Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza CCM katika ngazi zote zifanye uhamasishaji wa Wanawake wengi kwenda kugombea katika majimbo ya uchaguzi mwaka 2010 ili kuongeza Wabunge zaidi ya 18 waliopo hivi sasa.




3. UTEUZI WA WAGOMBEA UENYEKITI WA WILAYA

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, imepitisha wana CCM walioomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika Wilaya za Rorya, Tarime na Arumeru.

Nafasi za Tarime na Rorya zimetokana na kugawanywa kwa wilaya ya Tarime na kuwa wilaya mbili na ile ya wilaya ya Arumeru imetokana na kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya hiyo, Ndugu Lucas Lobulu aliyefariki Mei 6, 2009.

Waliopitishwa kugombea nafasi hizo ni:-

Wilaya ya Arumeru
1. Ndugu Jeremiah Saruni Kaaya
2. Ndugu Gabriel Kilale Nnko
3. Ndugu Joseph Ole Loning’o Saivoiye

Wilaya ya Tarime
1. Ndugu George Mkama Chacha
2. Ndugu Bogomba Rashid Chichake
3. Ndugu Peter Keba Wangwe

Wilaya ya Rorya
1. Ndugu Leonard Yodal Ambonya
2. Ndugu Jomoko Mjee Kateti
3. Ndugu Ramadhan A. Nyanganira

Wilaya husika zitafanya uchaguzi kwa ratiba itakayoandaliwa baadaye.

4. CHAGUZI NDOGO BUSANDA, MAGOGONI NA BIHARAMULO

Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa kujadili tathmini ya chaguzi ndogo katika majimbo ya Busanda, Magogoni na Biharamulo, imewashukuru na kuwapongeza wale wote waliofaikisha ushindi wa CCM katika Uchaguzi mdogo wa Majimbo ya Ubunge ya Busanda (Mwanza) na Biharamulo Magharibi (Kagera) pamoja na Uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Magogoni, Zanzibar.

Aidha, Halmashari Kuu pia imetoa pongezi za dhati kwa wana-CCM, wapenzi wa CCM na wananchi kwa ujumla kwa ushindi waliokipatia Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi hizo ndogo za Ubunge, Uwakilishi na za Udiwani katika Kata 10 za Tanzania Bara.

Kutokana na ushindi huo, kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kiliwaomba wana-CCM, wapenzi wa CCM, wakereketwa na wananchi kwa ujumla kuendelea kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee na majukumu ya kumkomboa Mtanzania na kudumisha amani na utulivu.

5. MAHAKAMA YA KADHI

Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhika na hatua zinazochukuliwa na Serikali za kulipatia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara. Moja ya hatua hizo ni uundaji wa Kamati ya mazungumzo baina ya viongozi wa dini ya Kiislam na Serikali kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nje ya mfumo wa Serikali.

Aidha, Halmashauri Kuu imesisitiza kwamba iwapo wapo Waislam wanaona haki zao hazikamiliki bila ya kuwa na chombo cha aina hiyo, wasizuiliwe. Waruhusiwe kuanzisha Mahakama ya Kadhi wao wenyewe na Serikali isijihusishe kuiendesha mahakama hiyo kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imejiingiza katika shughuli za kidini; na kwamba Mahakama hiyo isihusike na kesi za jinai wala madai, bali ihusike na masuala ya ndoa, talaka na mirathi.

6. WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU (RC)

Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuzingatia waraka wa Maaskofu, na hasa malumbano na hisia tofauti zilizojitokeza kuhusu waraka huo, imeelekeza kwamba viongozi wakuu wa nchi wafanye mazungumzo na viongozi wa dini zote ili kutafuta njia tulivu ya kusafisha hali ya hewa na kujenga umoja na utengamano katika jamii yetu.

7. MALUMBANO YA VIONGOZI

Kuhusu tabia iliyozuka hivi karibuni ya baadhi ya Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Viongozi wa Chama kutoa matamshi hadharani yenye mwelekeo wa kuchafuana majina, na yanayoashiria kuvunjika kwa umoja na mshikamano ndani ya CCM na Serikali zetu, na pia yenye mwelekeo ya kudhoofisha muungano wetu, Halmashauri Kuu ya Taifa pamoja na kukemea vikali tabia hii, imetoa maagizo yafuatayo:-

(a) Kwamba kuanzia sasa viongozi wote wa CCM warejee katika nidhamu ya Chama ya kuzungumzia masuala ya Chama katika vikao rasmi vya Chama na sio vinginevyo.




(b) Kamati za Wabunge wa CCM, na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM zitumike kujadili masuala yahusuyo CCM ndani ya vyombo hivyo.

(c) Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watumie taratibu zilizopo katika kushughulikia kero za Muungano badala ya kufanya kwa suala la mafuta kwa upande wa Zanzibar.

(d) Viongozi watakao vunja maadili haya watakuwa wamejibainisha kwamba hawana nia njema na CCM, na watahesabiwa ni wasaliti wa CCM hivyo Chama hakitasita kuwapa adhabu kali, ikiwa ni pamoja ya kuvuliwa uongozi na hata kufukuzwa katika Chama.

(e) Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito kwamba mapambano dhidi ya rushwa na maovu mengine ni jukumu la wana CCM wote na raia wema wote kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ahadi 4 ya WanaCCM. Halmashauri Kuu ya Taifa imeonya kuhusu dhana inayojengeka kwamba vita dhidi ya rushwa na ufisadi inahusu kikundi kidogo tu cha wana CCM, usahihi ni kwamba vita hii ni ya wana CCM wote kwa mujibu wa Katiba ya CCM vita hivi lazima iendelee kuhusisha wana CCM wote na wananchi wote wenye mapenzi mema na nchi yetu.

(f) Kwa kutambua kuwepo matatizo ya matamshi na vitendo visivyoridhisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi, Halmashauri Kuu ya Taifa imeamua kuunda Kamati Ndogo ya kutafuta undani wa matatizo hayo na kupendekeza kwa Kamati Kuu njia za kuyatatua. Aidha, Kamati hiyo pia itaangalia utendaji kazi wa Kamati za Chama katika Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa nia ya kubaini upungufu uliopo ili kupendekeza kwa Kamati Kuu kuhusu njia za kurekebisha. Pia, Kamati itaangalia masuala ya uendeshaji wa shughuli za Bunge na Baraza la Wawakilishi na kushauri namna ya kuimarisha, pale panapostahili.

Kamati hiyo itaongozwa na Mzee Alli Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Wajumbe wengine ni Mzee Pius Msekwa Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) na Ndugu Abdulhaman Kinana.

8. KUHESHIMU VIONGOZI WASTAAFU

Halmashauri Kuu ya Taifa imewakumbusha wana CCM, Viongozi na Watanzania kwa jumla kuhusu umuhimu wa kudumisha utamaduni wa kuwaheshimu na kuwaenzi viongozi wastaafu, hususan Marais wastaafu.

Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imesikitishwa sana na hali iliyojitokeza Bungeni ya kutoa maneno ya kejeli dhidi ya Mzee Benjamin W. Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu.

Halmashauri Kuu ya Taifa imesisitiza kwamba Mzee Mkapa katika kipindi chake ameliongoza Taifa letu kwa ufanisi mkubwa, aliinua hali ya uchumi, aliendeleza miundombinu, aliendeleza huduma za kijamii hasa elimu, afya, maji na kwa jumla alilijengea heshima kubwa Taifa letu.

Mzee Mkapa anastahili pongezi sio kejeli, anastahili heshima na sio dharau, anastahili kuenziwa na sio matusi.

Kwa kuzingatia hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa inatoa wito kwa wana CCM na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yetu waache mara moja kumchafua na kumkejeli Mzee Mkapa na badala yake apewe heshima anayostahili na aachwe apumzike kwa amani.



9. UTEUZI WA MAKATIBU WAPYA WA MIKOA

Halmashauri Kuu ya Taifa imewateua wafuatao kuwa Makatibu wa Mikoa:-

(1) Ndugu Sauda Mpembalyoto (Katibu wa Wilaya ya Hai)
(2) Capt. (Mst) Frarten Kiwango (Katibu wa Wilaya ya Kibaha Mjini)

Hawa wanajaza nafasi zilizoachwa wazi na Ndugu Amina Makilai aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Pwani na sasa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT, pia Ndugu Salum Msabah aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Kigoma na sasa amerejeshwa Makao Makuu ya CCM kuongoza Kitengo cha Propaganda.

10. UCHAGUZI WA MJUMBE WA NEC KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI

Nafasi hii iliachwa wazi na marehemu Richard Nyaulawa na ilikuwa inawaniwa na wagombea watatu.

Kutokana na kura za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa aliyechaguliwa ni Ndugu Jasson Rweikiza aliyepata kura 88.

Wengine waliogombea nafasi hii ni Ndugu Ramadhani Maneno kura 85 na Ndugu Sifa Swai kura 46.

Imetolewa na:-

Capt. (Mst) John Z. Chiligati (Mb),
KATIBU WA HALMASHARI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
17/8/2009
18 Aug 2009
 
1. Baija Bolobi
user_offline.gif

Baija Bolobi Narrow Pundit
Senior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png

green.png

green_right.png


icon1.gif
Spika Sitta hakuomba radhi
Wazee na Waheshimiwa wana jamvi

Nikiwa mjumbe wa NEC nisiye na kundi lolote, nawajibika kuweka sawa rekodi moja katika mjadala unaoendelea kuhusu Spika Sitta na kilichotokea ndani ya ukumbi wa mkutano wa NEC.

Baada ya mjadala mrefu ulioshabikiwa sana na wajumbe wengi huku hoja zao zikijiwa bila jazba na wajumbe wachache lakini wanaoheshimika, Spika Sitta alikutana faragha na Mwenyekiti JK, Rais Mwinyi na Kinana. Baada ya faragha ile ambayo bado ni siri, Spika Sitta alipopata nafasi alisema maneno machache sana yenye pointi mbili. Kwanza, aliwashukuru wajumbe kwa kutumia uhuru wao kutoa maoni yao. Pili, alisema anaiachia meza kuu kutafakari yaliyosemwa na pande zote. Kisha alimaliza na kukaa.

Hata kama sikubaliani na baadhi ya misimamo yake, siwezi kusema kuwa aliomba radhi. Lakini pia siwezi sema alikosa watetezi kama inavyoripotiwa. Kulikuwa na hoja nzito, tena nyingine kutoka visiwani zilizomtetea.

Kiroja cha mjadala alikuwa Guninita, Mwenyekiti wa Mkoa wa DSM aliyechemka lakini JK akamzodoa kwa kumwambia "kama ana uchungu na chama mbona alikiacha na kwenda CHADEMA na kuitukana CCM kwa miaka miwili?"

Habari ni hiyo.

Baija
2.
Mkuu Nemesis,

Taarifa rasmi za kikao cha NEC ya CCM zimeshatoka na maelezo yako very clear na yameonesha dhahiri nia na malengo ya mpotoshaji aliyekuwa anamwaga 'dataz' hapa za kwa sababu zake anazozijua yeye mwenyewe.

Mleta 'dataz' si mwanaCCM anapata taabu gani kuhangaika kutafuta habari mikutano ya CCM? lengo lake ni nini kama siyo kutafuta habari za uwongo?

Anaetaka kuendelea kusikiliza upotoshaji aendelee, 'ruksa' lakini treni la ukweli litamuacha na asije akalalamika hapo baadae.



- Haya mkuu sisi yetu ni macho tu, maana you must be a very intelligent person kuliko sisi wote humu ndani ya JF, yaani dataz ulete mwenyewe kwamba ulikuwa kwenye kikao, halafu tena ugeuze kibao kwamba dataz zako wenyewe ni za uongo Aaaahhhhhhggggrrrr!, sasa sisi watazamaji ngoja tujaribu kuku-figure out exactly what you are?

- But hii byitself ni Ze-comedy kuliko hata hicho kikao cha NEC

Respect.


FMEs!

 
“Sisi ndio tunaotawala, tunayo haki ya kumhoji na kumuuliza namna anavyoliongoza Bunge. Serikali ni yetu, mnataka nani amuulize?” alihoji Makamba na kuongeza:

........Duh!!!! Kwa hiyo siyo kweli kuwa serikali ya Tanzania ni ya wananchi wa Tanzania. Ndiyo maana serikali hiyo inatoa maamuzi ambayo hayana manufaa kwa wananchi wa wa Tanzania ila labda kwa watu wachache kama akina Makamba na NEC yao.
 
1. Baija Bolobi
user_offline.gif

Baija Bolobi Narrow Pundit
Senior Member

red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png


green.png

green_right.png



2.

- Haya mkuu sisi yetu ni macho tu, maana you must be a very intelligent person kuliko sisi wote humu ndani ya JF, yaani dataz ulete mwenyewe kwamba ulikuwa kwenye kikao, halafu tena ugeuze kibao kwamba dataz zako wenyewe ni za uongo Aaaahhhhhhggggrrrr!, sasa sisi watazamaji ngoja tujaribu kuku-figure out exactly what you are?

- But hii byitself ni Ze-comedy kuliko hata hicho kikao cha NEC

Respect.

FMEs!


Ukweli ya yale yaliyojiri katika kikao cha NEC yanapatikana katika tovuti ya CCM http://www.cms.ccmtz.org/index.php?section=news&cmd=details&newsid=50 the rest ni historia.

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
 
Dah!

Kusila alikuwa mwalimu wa Physics, na alikuwa bright sana. Hivi kumbe siasa zinaweza kuwafanya watu wawe wa ajabu kabisa?

Hapa umegongelea kwenye UTOSI. Kama politiksi haipandi ni vyema akarudi kwenye physics. Na si ajabu hiyo physics sasa hivi itakuwa imesha-evaporate from his UBONGO.
 
Ukweli ya yale yaliyojiri katika kikao cha NEC yanapatikana katika tovuti ya CCM http://www.cms.ccmtz.org/index.php?section=news&cmd=details&newsid=50 the rest ni historia.

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

Kwa CCM ambayo inatanguliza political interests, tamko rasmi la CCM siyo reflection sahihi ya yaliyojiri kikaoni. Huo ndio ukweli ukitaka tutakuletea mifano mingi sana ku-prove hivyo ukianzia na uchaguzi wa Mkapa kuwa mgombea wa uraisi mwaka 1995
 
Kwa CCM ambayo inatanguliza political interests, tamko rasmi la CCM siyo reflection sahihi ya yaliyojiri kikaoni. Huo ndio ukweli ukitaka tutakuletea mifano mingi sana ku-prove hivyo ukianzia na uchaguzi wa Mkapa kuwa mgombea wa uraisi mwaka 1995

Ukweli ya yale yaliyojiri katika kikao cha NEC yanapatikana katika tovuti ya CCM http://www.cms.ccmtz.org/index.php?s...ails&newsid=50 the rest ni historia.

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
 
Ukweli ya yale yaliyojiri katika kikao cha NEC yanapatikana katika tovuti ya CCM http://www.cms.ccmtz.org/index.php?s...ails&newsid=50 the rest ni historia.

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

Punda enzi za propaganda zimekwisha. Hatutaendelea kuishi kwa propaganda na nyimbo za Komba. Tunahitaji mabadiliko ya kweli.

Ukweli wa yaliyojili kwenye vikao vya sisi M hatuwezi kuyapata kwenye mtandao wa Sisi M kwa kuwa vikao vyenyewe havikuwa transparent.

Kwa nini hawakutaka hata waandishi wa habari wawepo, maana yake walitaka viwe vya siri, na hatutaki watupe hizo siri bali wacha sisi wenyewe tuzitafute hizo siri.

Yaliyoandikwa jf ndiyo ya kweli maana siri yoyote ikishahusisha zaidi ya mtu mmoja si siri tena.
 
CCM: Breaking the law?


THERE is growing consensus among top independent legal experts in the country that stalwarts of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) may have broken a number of laws of the land in their latest controversial attempt to exert strict control over parliamentary proceedings by reining in rebel legislators from within the party ranks.

Several legal analysts have told THISDAY in separate interviews that this week’s move by the party’s national executive committee (NEC) to threaten CCM members of parliament with expulsion from the party, ostensibly for ”embarrassing” the government over various allegations of grand corruption, was basically in violation of the national constitution.

”How can CCM try to prevent its MPs from freely expressing their views in parliament? That is insane,” University of Dar es Salaam (UDSM) senior law lecturer Dr Sengondo Mvungi said.

According to Mvungi, a specialist on constitutional law, the attempts by CCM to put its parliamentary representatives on a tight leash also represents a breach of several standing legislations, including the Political Parties Act Number 5 of 1992.

�This law requires all registered political parties in Tanzania - CCM included - to be run on democratic principles. As such, what NEC is trying to do is in defiance of this law,” asserted the former dean of the UDSM faculty of law.

He explained that universally-accepted principles of democracy require political parties to give freedom to all members, including MPs, to openly criticize government policies, decisions and even individual government leaders, without fear of restriction.

Mvungi strongly criticised CCM-NEC for threatening the Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta, and other so-called rebel CCM lawmakers with expulsion from the party if they do not tow the party line.

He noted that Sitta appeared to have come under attack from forces of corruption within the ruling party primarily because of his tough stance against grand corruption.

”This Speaker will never put up with scandals of the scale of Richmond, Kiwira and Meremeta...That’s why they want him removed from that post,” said Mvungi, a presidential candidate on an opposition NCCR-Mageuzi ticket back in 2005.

In what can be construed as a rare move by an opposition leader, Mvungi went to the extent of saluting Sitta as ”the best Speaker of the National Assembly in Tanzania’s entire history.”

On his part, respected lawyer and former opposition MP Mabere Marando backed an opinion already expressed by another prominent local legal expert, Tundu Lissu, to the effect that CCM has also breached specific parliamentary legislation in moving to control future Bunge proceedings by gagging its own MPs.

”It is a fact that in this instance, the ruling party has gone against the Parliamentary Immunities, Powers and Privileges Act of 1988 in particular,� Marando said when contacted for comment.

He advised CCM lawmakers who have been vocal in opposing corruption and abuse of public office to resign from the ruling party, rather than accept such a prohibitive and condescending gag order.

Yet another prominent legal expert and university lecturer, Prof. Abdallah Saffari, also described the latest CCM-NEC ploy to control parliamentary proceedings as ”unconstitutional” and a violation of parliamentary powers and privileges, designed to turn the Bunge into a ”mere committee of the ruling party.”

”If this thing is allowed, members of parliament will effectively lose their independence,” Prof. Saffari noted.

The Legal and Human Rights Centre (LHRC) issued a strongly-worded statement yesterday castigating both CCM-NEC and the ruling party’s central committee for attempting such an �unconstitutional� step, and at the same time praising Speaker Sitta for �his firm and independent leadership of parliament.�

”The LHRC also praises other MPs who have courageously spoken out against corruption,” said the statement.

At the just-concluded CCM top level meetings in Dodoma, ruling party MPs were warned in no uncertain terms to lay off the burning subject of corruption allegations levelled against former president Benjamin Mkapa, as well as other pending grand graft scandals, or ultimately have their party membership annulled.

Meanwhile, CCM’s propaganda specialist Richard Tambwe Hiza told a news conference in Dar es Salaam yesterday that Sitta was not targeted at the Dodoma meetings of the ruling party big guns.


SOURCE: http://www.thisday.co.tz/News/6217.html
 
- Ukweli ni kwamba hata hiyo kamati ya kina Mwinyi iliyoundwa na NEC nayo ni ukiukaji wa sheria ya Jamhuri, kama hiyo kamati ikifanya kweli walichotumwa basi ni haki kabisa kwa wananchi kuwafikisha kwenye mkono wa sheria,

- Na ikibidi kumu-impeach Mwenyekiti wa CCM, aliyeruhusu ambaye pia ni rais wa Jamhuri.

Respect.


FMEs!
 
Ukweli ya yale yaliyojiri katika kikao cha NEC yanapatikana katika tovuti ya CCM http://www.cms.ccmtz.org/index.php?s...ails&newsid=50 the rest ni historia.

AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

Mkuu Pundamilia07, huo ni ukweli wa yale yaliyoandikwa. Yaliyosemwa, kujadiliwa na kupangwa mengi ni tofauti.

Yaliyoandikwa kwenye Ilani ya CCM yote yangefatiliwa ipasavyo au yangelikuwa ndiyo hayo yanayosemwa kwenye vikao vyake vikuu, nchi yetu ingelikuwa ni nchi ya kipato cha kati kwenye uchumi by now. Yanayosemwa na yanayoandikwa wanachama na wananchi wajisomee ni TOFAUTI!!
 
wabunge watambue kuwa wamapata wadhifa huo kupitia chama cha mapinduzi,hivyo chama ni kama baba na mama yao,kina wajibu wakusimamia nidhamu zao ndani na nje nya chama,kama baba ,mama na watoto wake.
 
Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amewashukia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, kuzungumzia maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) nje ya utaratibu wa chama hicho.

Pia Sitta, amekanusha taarifa zinazodai kwamba aliomba msamaha ili 'asisulubiwe' katika mkutano huo wa NEC uliofikia kilele chake Agosti 18, mwaka huu mjini Dodoma.

Akihojiwa na waandishi wa habari kwenye maktaba iliyopo nyumbani kwake mjini hapa jana, Sitta alisema maamuzi yaliyofikiwa na NEC yalipaswa kuheshimiwa ili kutoa fursa kwa kamati iliyoundwa ikiongozwa na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kutoa taarifa kuhusu mpasuko unaodaiwa kuwepo miongoni mwa wabunge kupitia CCM.

"NEC iliteua kamati ya watu wenye uwezo, Rais mstaafu Mzee Mwinyi, Spika aliyepita Pius Msekwa na aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdulrahman Kinana, tusubiri watangudua kasoro ni nini, kama tatizo ni Sitta ama tatizo lipo kwa wigo mkubwa zaidi," alisema.

Hivi karibuni viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Makamba, Chiligati na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda cha chama hicho, Hiza Tambwe, walikaririwa wakizungumzia uamuzi uliofikiwa na NEC, huku wakikiepusha chama hicho na kashfa ya kuingilia uhuru na mamlaka ya Bunge.

"Nilitegemea viongozi wa makao makuu wangeheshimu uamuzi wa NEC, lakini inanikera mara unasikia Chiligati kasema hivi mara Makamba kasema hivi, ninawashangaa wajumbe wa sekretarieti wanapotoa maneno hayo yanayochapishwa na kutangazwa na vyombo vya habari," alisema. Sitta, alisema maamuzi yaliyofikiwa na NEC yamechochewa na taarifa nyingi zisizokuwa za kweli zenye lengo la kumchafua huku akitoa mfano wa ripoti zilizoenezwa kwamba aliomba msamaha baada ya kubanwa katika kikao hicho.

"Haya maneno wananitungia tu, hapakuwa na kitu hicho kwa sababu CCM ina taratibu zake za kushughulikia shutuma dhidi ya wanachama wake, haya mambo yanayoenezwa yaliibuliwa tu kwa hoja ambazo sioni sababu ya kuzizungumza kwa vile zipo kwenye NEC," alisema.

Alisema mtuhumiwa katika kadhia ya kuisaliti ama kuiathiri CCM kwa namna yoyote, wanafikiwa shutuma zao kwa njia ya maandishi na kuhojiwa kwenye vikao vya kamati za maadili na ulinzi, jambo ambalo halijafanyika kwake. Badala yake, Sitta alisema kilichogundulika na kujadiliwa katika NEC ni uhusiano miongoni mwa wabunge wa CCM, kazi itakayofanywa na kamati ya Mwinyi ili kupata ukweli.

"Kamati ya Mwinyi itawahoji wabunge mmoja mmoja na hapo ukweli wa tatizo lililopo litajulikana," alisema Spika Sitta ambaye jana alishiriki tamasha la nyimbo za injili mjini Tabora.

Aidha, Sitta alieleza kusikitishwa na taarifa za kuwepo viongozi wa CCM makao makuu na mkoani Tabora kuwazuia viongozi wa chama hicho wilayani Urambo kutoshiriki mapokezi yake na mkutano wa hadhara uliofanyika juzi mjini hapa.

"Nimepata taarifa kwamba viongozi wa wilaya wametishiwa na kuzuiwa kutoshiriki mapokezi na mkutano wangu, mbona akina Chenge na Lowassa waliporejea majimboni kwao walipata mapokezi yaliyowashirikisha hadi viongozi wa mikoa yao, kwa nini iwe nongwa kwa Sitta," alihoji.

Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi aliyekuwa Waziri wa Miundombinu ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa ya kuhusishwa na kashfa ya kuhifadhi mabilioni ya fedha nje ya nchi.

Fedha hizo zinaendelea kuchunguzwa na mamlaka ya uchunguzi nchini Uingereza (SFO), ili kubaini kama zilitokana na rushwa kwenye mradi wa ununuzi wa rada, ambapo baada ya kujiuzulu kwake, Chenge alirejea jimboni na kupokelewa kwa shangwe na watu mbalimbali, akiwemo Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Hamis Mgeja.

Naye Lowassa alijiuzulu Uwaziri Mkuu kutokana na kashfa ya mkataba tata kati ya Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambapo alirejea jimboni kwake Monduli na kupata mapokezi makubwa. Sitta, aliishauri CCM kuhakikisha kuwa mikutano ya kamati ya wabunge wa CCM ambayo haijafanyika kwa miaka minne sasa, ifanyike ili kunusuru hoja 'nzito' zinazowagawa wabunge kifikra na mitazamo kujadiliwa ili kupata msimamo wa pamoja.

Mwenyekiti wa kamati ya wabunge wa CCM ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu wake ni Ali Ameir Mohammed.

"Wanaodai kwamba hoja nyingine zilistahili kuzungumzwa kwenye kamati ya wabunge wa CCM, kama Spika sina mamlaka ya kuitisha vikao hivyo na hoja zinapoletwa bungeni sina uwezo wa kutabiri ipi itakuwa nzito kiasi cha kuitikisa serikali, lakini Bunge linasimamia kanuni zake na hilo ndilo linalofanyika," alisema Spika Sitta ambaye hakutaka kuzungumzia kwa undani masuala ya NEC.

Kuhusu shutuma za kuwapendelea wabunge wanaojulikana katika vita dhidi ya ufisadi kuchangia hoja bungeni, Sitta alisema kanuni na taratibu za Bunge hazimpi fursa ya kutoa upendeleo huo na kwamba hoja hiyo ni sehemu ya muendelezo wa hoja zenye lengo la kumtungia uongo.

Alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge, watoa hoja bungeni wanajiandikisha kupitia fomu maalumu zinazowasilishwa kwa Katibu wa Bunge, anayemfikishia (Spika) mtiririko wa majina ya wachangiaji isipokuwa kwa wabunge wanaouliza maswali ya nyongeza.

"Vikao vya Bunge siyo mkutano wa holela kwa mtu mmoja kufanya udikteta, hivyo kuchagua wazungumzaji bungeni si suala la Spika, watu wajue hivyo," alisema.


CHANZO: NIPASHE
 
Date::8/24/2009
Spika: Nitapambana na mafisadi hadi kifo
*Mkewe asema maisha ni mpito, kifo ni faida
John Dotto, Tabora
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amesema kamwe hawezi kutetereka katika maamuzi yake, kwa kuwa anaamini kuwa Mungu yuko naye katika kila jambo jema analolifanya.
Akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara ulioandaliwa na wenyeviti wa makanisa ya Mkoa wa Tabora, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora jana, Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Magharibi, alisema hatatetereka katika maamuzi yake kwa kuwa anaamini anayatekeleza kwa nia njema.
"Katika maamuzi ninayochukua daima ninaamini kuwa ni mambo mema na ninajua kuwa Mungu peke yake ndiye anayenilinda, kwa hivyo sitatetereka hata kidogo,"alisema Spika Sitta ambaye siku za nyuma aliapa kupambana na mafisadi hadi ushidi upatikane.
Alisema hivi sasa kumeibuka tabia ya baadhi ya watu nchini, kulazimisha yale wanayoyafanya wao yaonekane kuwa ndiyo ya ukweli kabisa hata kama wanayoyafanya ni ya uongo.
"Katika nchi yetu kumeibuka tabia ya waovu wanaosambaza uongo uliopakwa asali, hugeuza uongo huo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo, siwezi kukubaliana nao sababu ni waovu,"alisisitiza kauli ambayo imetafsiriwa kuwa anawalenga wale ambao walitaka avuliwe uanachama wa CCM katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho.
Kauli hiyo iliungwa mkono na mkewe ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margaret Sitta, ambaye alinukuu kauli ya Askofu Norbert Mtega wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Songea, ambaye alisema kuwa maisha ni mpito na kifo ni faida, alipokuwa akizungumza katika msiba wa baba wa Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama.
"Kauli ile ya Askofu Mtega tunaichukua na sasa tunaifanya kuwa falsafa ya maisha yetu, kwa maana hiyo kwetu sisi sasa maisha ni mpito tu na kifo kwetu ni faida,"alisema waziri huyo.
Kwa upande wake mume wake (Sitta) alisema taifa linaelekea kubaya kwa sababu baadhi ya watu wanajaribu kulazimisha yale wanayoona kuwa ni sawa na kwamba wanatumia gharama kubwa kufanya hivyo.
Mwenyekiti wa umoja wa makanisa mkoani Tabora, William Lusito, alisema umoja huo umetokana na azimio kuwa nyuma ya Spika na kwamba, hawatakubali kumuona akiyumbishwa na kundi la aina yoyote.
Spika huyo pia alielezea kusikitishwa kwake juu ya hatua ya baadhi ya watu, kusambaza maeneo yasiyokuwa na ukweli kuhusu yeye, wakidai kuwa aliomba radhi kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).
Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, aliyasema hayo jana nyumbani mjini Urambo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, akiwa katika ziara yake aliyoianza rasmi jana.
Mamia ya watu wa jimbo hilo, walijitokeza kwa wingi kumlaki mbunge wao.
"Kwa kuwa mimi niliwekwa katika kikao cha kujieleza, mimi ninarudisha swali kwa hao wanaosambaza hayo, waeleze niliomba radhi kuhusu kipi,"alisema.
Alisema hataki kuzungumzia yaliyotokea ndani ya kikao, lakini kwa kuwa kuna watu wamejitokeza kuzungumzia hayo, kuna haja kwa watu hao kueleza sababu za yeye kuomba radhi katika kikao cha siku mbili cha NEC.
"Ninachokisema ni hivi, kwa kuwa kikao cha NEC kimefikia mwisho na chama chetu kikatoa maamuzi ya kuunda jopo la watu watatu wenye busara wakaangalie hali ya Bunge letu, watawahoji wabunge, wanachama na kisha tutayasikia maamuzi yao Oktoba basi ni bora tusubirie matokeo yao,"alisema.
Alisema yeye kama mtu mwenye subira atakuwa mtu wa ajabu mno, kuzungumzia yaliyotokea ndani ya kikao cha NEC na CC na kwamba, kauli na maelezo yanayotolewa na baadhi ya watu kutaka kubadilisha picha halisi ya kile kilichotokea ni upotoshaji na inasikitisha.
"Nasikitishwa na makao makuu ya CCM Dodoma kwa ambavyo wanavyoshughulikia baadhi ya mambo, kwani ingekuwa kwa mara moja, kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chilligati, ilitosha kumaliza mambo.
Alisema, hata hivyo, inashangaza kuona mambo hayo yanarudiwa wakati yanapaswa kushughulikiwa na na kamati maalumu.
"Inashangaza kuona mara anazungumza Katibu Mkuu, mara anazungumza mwanachama tu wa CCM, tena mambo ambayo ni dhahiri yanayoonekana kuwa ni tuhuma bila ya kuacha vyombo vilivyoundwa na chama vifanye maamuzi yake," alisisistiza Sitta.
"Nimesikitishwa na wakuu wa chama ambao waliruhusu, Chenge (Andrew) na Lowassa (Edward) wapokelewe, lakini wanazuia katibu na mwenyekiti wasinipokee, ingawa wanachama walijitokeza kunipokea, hii ndiyo inatufanya wanachama tuamini kuwa kuna wanachama wenye haki na wasio na haki, hii si dalili nzuri,"alisema.
Alielezea kushangazwa na hatua ya makao makuu ya CCM ya kuuzuia uongozi wa mkoa wake usimpokee.
Alisema hivi karibuni amesikia kauli zilizotolewa na viongozi wakuu wa CCM zikionyesha kuegemea upande mmoja, jambo ambalo si dawa na linaonekana kutotumika kwa busara katika wakati huu ambapo kikao cha NEC kimemalizika .
Hata hivyo, aliwashukuru wanachama wa CCM wa Jimbo la Urambo Magharibi, waliojitokeza kwa wingi kumlaki na akawataka kutokata tamaa na waendelee na moyo huo.
Kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kuwa amekuwa akiendesha Bunge kwa kuwapanga wabunge, alikanusha na kwamba, utaratibu wa Bunge unafahamika.
"Vikao vya Bunge vinaendeshwa kwa taratibu na kanuni, kila mbunge anayetaka kuchangia anapitisha hoja zake kwanza kwa Katibu wa Bunge na au kutoa taarifa kwa katibu huyo, hivyo hakuna ukweli wowote kwamba nimekuwa nikipanga mambo,"alisema.
Spika Sitta juzi huko Urambo alipata mapokezi makubwa baada ya kuwasili jimboni humo ikiwa ni mara ya kwanza tangu apate msukosuko kutoka kwenye vikao vya chama chake.
Mwandishi wetu aliyekuwa huko, alisema Sitta alipokelewa na wapigakura wake wakiwa na pikipiki zaidi ya 100 na kutembea naye kwa maandamano kwa umbali wa kilometa moja.

www.mwananchi.co.tz
 
Back
Top Bottom