Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Sitta afyatuka tena
• Amshukia Makamba, Chiligati wanaomshambulia nje ya NEC

na Mwandishi Wetu, Tabora


amka2.gif
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta, amesema anakerwa na kauli za upande mmoja zinazoendelea kutolewa na viongozi wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadhi ya wajumbe wa Halmashari Kuu ya chama hicho (NEC), badala ya kusubiri ripoti ya kamati iliyoundwa na NEC, imalize kazi yake.
Sitta ambaye hii ni mara yake ya pili kuzungumza hadharani tangu aliposulubiwa na NEC, mjini Dodoma wiki moja iliyopita, alisema hayo jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika jimboni kwake Urambo, mkoani Tabora.
Ingawa hakuwataja majina, lakini ni wazi kwamba Sitta alikuwa akimlenga Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Yusuf Makamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Kapteni John Chiligati na baadhi ya wajumbe wa NEC ambao kwa nyakati tofauti, wamekaririwa na vyombo vya habari wakitetea uhalali wa CCM kumshughulikia Sitta na wabunge wanaojifanya wapiganaji wa vita dhidi ya ufisadi wakati wa mkutano wa NEC.
"Nilitarajia watu wa makao makuu ya CCM, kuzingatia na kusubiri uamuzi wa kamati iliyoundwa na NEC ambayo inaongozwa na mzee Mwinyi pamoja na wajumbe wengine, hivyo si busara kwa namna yoyote kwamba kama hutaki malumbano, kwanini unaendelea kutoa maneno?" alihoji Sitta.
Sitta ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akiandamwa na kashfa mbalimbali, huku akijizolea umaarufu kutokana na msimamo wake wa kuliendesha Bunge kwa stahili yake ya viwango, alisisitiza kuwa hataki kujibu lolote, lakini anakerwa na hali ya malumbano inayoendelea sasa.
"Mimi nadhani sasa tuache maneno na kejeli nje ya NEC wakati tayari kuna kamati imeundwa kuchunguza malumbano ndani na nje ya Bunge, ningeshauri watu wa makao makuu ya chama, waiachie kamati hiyo ifanye kazi yake ili ijue tatizo, kama ni mimi au kama kuna tatizo pana zaidi," alisisitiza.
Kuhusu yaliyotokea ndani ya NEC, Sitta alisema kuna kundi la watu linalojaribu kumwekea maneno mdomoni ili kumletea picha mbaya mbele ya jamii na kuonyesha kwamba hafai.
Akitolea mfano wa baadhi ya maneno aliyodai amewekewa mdomoni na kundi hilo la wabaya wake, ni pamoja na kauli kwamba aliomba radhi ndani ya kikao cha NEC, na kwamba kamati iliyoundwa ni kwa ajili ya kuchunguza mwenendo wake.
"Hayo yamekolezwa tu na baadhi ya magazeti, mimi daima nitasimamia katika ukweli na niwaambie tu kwamba tume iliyoundwa ipo kwa ajili ya kusuluhisha makundi yanayohasimiana ndani ya chama, si kwa ajili ya uendeshaji wa Bunge,"
"Mimi sikuomba radhi na kama niliomba, niliomba kwa kosa lipi? Mimi sikuwa na tuhuma yoyote na kama ingekuwapo, wangeipeleka kwenye Kamati ya Maadili, kwani ndani ya CCM, upo utaratibu wa kumtuhumu mwanachama pamoja na kumpelekea barua inayoonyesha tuhuma zake, mimi sikuletewa barua yoyote kwamba ninatuhumiwa kwa yanayoenezwa," alisema Sitta.
Kwa mujibu wa Sitta, kamati iliyoundwa itakuwa na kazi ya kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wabunge wa CCM ili kujua matatizo yao, jambo ambalo litasaidia kujua kiini cha malumbano ili kuchukua hatua za kudhibiti hali hiyo.
Akizungumzia madai ya NEC kwamba amekuwa akipanga watu wa kuzungumza bungeni, Sitta alisema madai hayo si ya kweli, kwani kila mbunge amekuwa akifuata utaratibu ambao ni kujaza fomu kwa Katibu wa Bunge, ambaye naye humpelekea Spika huku kila kitu kikiwa kimekamilika.
"Zipo fomu za kuchangia mjadala, ndizo zinatumika kwa wabunge wanaotaka kuchangia mjadala, hivyo mimi siwezi kujua mbunge anataka kuchangia nini au kwenye swali la nyongeza anataka kuongeza nini," alisema Sitta.
Juzi Sitta aliwasili mkoani hapa na kuweka bayana msimamo wake kwamba ataendeleza kasi ile ya mapambano dhidi ya ufisadi, pasipo kutetereka.
Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika viwanja vya CCM mjini Urambo, Sitta alisema yeye ni mzima wa afya na yuko imara na kusisitiza kuwa ataendelea na kasi ile ile.
Hivi karibuni, Makamba alisema chama hicho kina haki ya kumhoji Sitta na wabunge wote wa chama hicho, kwani wote ni mali ya chama hicho tawala.
Alipoulizwa juu ya mkanganyiko wa kauli mbili za viongozi wa juu wa chama hicho, Chiligati na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda, Tambwe Hizza, zilizotofautiana, Makamba alisema kauli halali ya chama ni ile iliyotolewa na Chiligati.
Wakati Makamba akitamba kuwa chama hicho kina haki ya kumhoji Sitta kama kilivyofanya katika vikao vyake vilivyopita, wiki iliyopita Tambwe alitoa tamko kwa vyombo vya habari linaloonyesha dhahiri kupindisha tafsiri ya maamuzi ya vikao hivyo, baada ya maamuzi hayo kuonekana kupata upinzani mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali nchini.
Katika tamko hilo, Tambwe alisema vikao hivyo havikujadili ajenda yoyote iliyowahusu Sitta na wabunge wenzake, wala iliyomhusu Makamba, aliyedaiwa kuwa ilikuwa nusura ang'olewe.
Wiki moja iliyopita, Sitta alibanwa ndani ya NEC na ilidaiwa aliomba radhi na kunusurika katika hatari ya kupoteza uanachama.
Hatua hiyo ya Sitta kuomba radhi ilikuja baada ya wajumbe takriban wote wa vikao viwili vya juu vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) vya chama hicho kujenga hoja za kumshambulia, wakipinga namna anavyoliendesha Bunge katika mwelekeo wa kukidhalilisha chama hicho na serikali yake.
Tukio hilo baya kabisa kuwahi kumfika Sitta ambaye amekuwa akijinadi kuwa ni spika wa kasi na viwango, lilihitimishwa na uamuzi wa NEC kuunda kamati maalumu kuchunguza kiini cha kufikia hapo.
Kamati hiyo maalumu inaongozwa na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na wajumbe wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa na mwanasiasa mkongwe, Abdulrahman Kinana.
Kwa mujibu wa habari hizo, mwelekeo wa wana CCM hao kutaka kumwadhibu Sitta, ambaye katika siku za hivi karibuni amejizolea umaarufu wa kisiasa ndani na nje ya Bunge, hata kuwa na uwezo wa kumnyoshea kidole mtu au taasisi yoyote, ulianza kujitokeza tangu wakati wa kikao cha Kamati Kuu mjini Dodoma.



http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=8034
 
ccm wanakumbuka shuka wakati kumekucha,wananchi tumejua kila kitu sasa mnataka kumtisha ili iweje.Tumesikia,tumeona na tumeshuhudia hali halisi ya mambo.ccm chama hiki kikongwe kinafikiri mpaka sasa watz wanamawazo ya kikongwe.Tuliisha amka mapema wanapoamua kuwatiisha majemedali wa vita kama spika Six wanaendelea kuchemka zaidi kwani hata wale ambao hawakauwa na uelewa wowote kuhusu ufisadi na mafisadi na watetezi wa mafisadi sasa wanaendelea kufunguka akili kuwa kumbe mbaya wa nchi hii ni system nzima ya ccm.Kumekucha jamani tuchangamke tusikubali kulala tena tukaendeklea kuibiwa kwani tumeibiwa vya kutosha.
Naamini nimesomeka............
 
Watajuuuuuuuuta! kumfahamu Six

KAzi kwelikweli.... vita ya uchaguzi yanukia mapema wenye kutoa misaada jimbonikwa six mpoooooo.... yetu macho hadi october mwakani

VITA YA PANZI .........
 
Wabeja sana ng'wana wane.
Mambo mengi gawiza tunayajua hadololo hadololo. Bado tutayasikia mengi tu. Tunaelekea kufanana na siasa za kenya ambapo mtu akishindwa kuanika hoja hadharani akaeleweka, atatumia msuli (maguvu). Sasa CCM ina misuli kichama, ndio maana utawasikia Pemba CUF wakilalamika lakini Masheha ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo serikali yenyewe na kwa maana hiyo diyo CCM wanatunisha msuli. Kesho na keshokutwa CUF nao wakikalia kiti watatunisha msuli hivyohivyo na itakuwa zamu ya CCM watakaoitwa kwa jina jipya maarufu "Wapinzani" Patamu hapo! Angalia KANU ya Kenya na kina NARK (Sijui NARC?), na Malawi na Zambia.

Jamani CCM, mwenzako akinyolewa si wewe utie maji kichwani? Unataka mfano ukufikie mwenyewe tu? Yose makoye gete aha.

Leka.
 
Wakati maonevu haya yote yakitokea kwa manufaa ya wachache, sisi wananchi tunafanya nini? Tunafurahia tu kuangalia kama watazamaji wa sinema? Tutajikomboaje?

Nashindwa kuelewa kama Six angeng'olewa na kuwekwa EL au Chenge, mijadala bungeni ingekuwaje?
 
Wameshachelewa Six atawapiga bao mpaka wakome.
EL na RA walitumia fedha nyingi kuwanunua wajumbe dhaifu ili kufanikisha njama zao za kutaka kujisafisha baada ya kushindwa pale mjengoni.

Kamati ya Mzee Ruksa haitakuwa na kazi kubwa kubaini kelele zote za NEC ulikuwa mpango wa Richadmonduli & Co.
 
mimi nilidhani spika angetulia kwanza!hii vita ya maneno haina maana yoyote!i remember the same scenario ilikuwa kwa Nnauye,mafisadi finally walishindwa.

mimi naamini sitta atashinda
 
Six alisema tangu mwanzo kuwa yeye ni standard na speed, walitakiwa kumzuia tangu mwanzo, sasa wamechelewa,

Namshauri aje chadema aongeze nguvu za kupambana na mafisadi. chukua chako mapema wanaweza kum-kolimba tukapata hasara kubwa
 
Ugali mtamu ukiwa wa bado wa moto. Mwache atoe dukuduku lake kabla watu hawajasahau. Watanzania tuna ugonjwa sugu wa kusahau. Hawa mafisadi walimpiga terror mbaya huyu spika.
 
Wakati maonevu haya yote yakitokea kwa manufaa ya wachache, sisi wananchi tunafanya nini? Tunafurahia tu kuangalia kama watazamaji wa sinema? Tutajikomboaje?

Nashindwa kuelewa kama Six angeng'olewa na kuwekwa EL au Chenge, mijadala bungeni ingekuwaje?

......Ingekuwa hivi:
Mh Spika: Baada ya Kingunge atafuataa Mahanga, namuona na Chenge naye amenyosha mkono, wafuatao nao wajiandae katika mtiririko huu, Edward Lowasa, Nazir Kalamagi, Mudhihir mudhihir, jackson Makweta.....................!!
 
- Ukweli ni kwamba hata hiyo kamati ya kina Mwinyi iliyoundwa na NEC nayo ni ukiukaji wa sheria ya Jamhuri, kama hiyo kamati ikifanya kweli walichotumwa basi ni haki kabisa kwa wananchi kuwafikisha kwenye mkono wa sheria,

- Na ikibidi kumu-impeach Mwenyekiti wa CCM, aliyeruhusu ambaye pia ni rais wa Jamhuri.

Respect.


FMEs!

mh...kumu-impeach si hadi bungeni!! Bunge ndo hilo wanataka kulishika kwa mkono wa chuma. Yani hapa tulipo hapajatulia kabisa. Chama kinajipima nguvu na bunge. Kinachoendelea hapa si kitu kidogo. Atakayeshinda hii pima nguvu, ndo atakaye kuwa mbabe kwa muda mrefu ujao. Bunge lazima lijitokeze as an institution lisimamie uwezo wake na upana wa nguvu yake. Ama sivyo tutaendelea kuumia kila siku. Uhuru wa bunge = uhuru wa wananchi. Uhuru wa chama = uhuru wa mafisadi!!!
 
Kilichotokea Dodoma katika Mkutano wa Kamati Kuu na NEC ya CCM kimethibitisha mambo matatu ambayo wataalam wamekuwa wakiyahofia kwa muda mrefu: (1) Kwamba CCM haiwezi kulinda maslahi ya taifa bali kimegeuka kuwa chama kinachotumiwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi. Mafisadi, wauza unga na matapeli wa kimataifa wamegundua udhaifu huo na wameweza kuutumia kuiteka CCM kama njia nyepesi na ya uhakika ya kuiteka serikali na hivyo kuiteka nchi. Awamu ya Tatu iliwakaribisha hadi uvunguni, na sasa Awamu ya Nne imejikuta ni mfungwa wao.
Kinachowaponza viongozi leo ni tamaa ya "shanga na kaniki" kama zilivyowaponza akina Mangungo, Sultani wa Msovero, zama za kuuza nchi na kuuza wananchi utumwani. Historia inajirudia nasi tunaiangalia kijingajinga tu.
Kilichotokea Dodoma ni "dress rehearsal" ya mwaka 2010, na kimethibitisha kwamba kwa mfumo huo wa CCM na mtindo ulioko sasa wa kujadili na kufikia maamuzi, siyo CC wala NEC wala Mkutano Mkuu wa CCM unaoweza kuwazuia mafisadi, wauza unga na matapeli kuwasimika vibaraka wao katika uongozi wa chama na serikali, ikiwa ni pamoja na/au hasa nafasi ya urais. Dodoma imeonyesha wazi kuwa kikundi kidogo chenye pesa za wizi na dhamira kikijipanga vizuri kinaweza, tena kwa ulaini kabisa, kuiburuza CC na NEC na hivyo serikali na nchi nzima na kuzitumia wanavyotaka
 
Date::8/24/2009

Spika: Nitapambana na mafisadi hadi kifo
*Mkewe asema maisha ni mpito, kifo ni faida
John Dotto, Tabora
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amesema kamwe hawezi kutetereka katika maamuzi yake, kwa kuwa anaamini kuwa Mungu yuko naye katika kila jambo jema analolifanya.
Akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara ulioandaliwa na wenyeviti wa makanisa ya Mkoa wa Tabora, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora jana, Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Magharibi, alisema hatatetereka katika maamuzi yake kwa kuwa anaamini anayatekeleza kwa nia njema.
"Katika maamuzi ninayochukua daima ninaamini kuwa ni mambo mema na ninajua kuwa Mungu peke yake ndiye anayenilinda, kwa hivyo sitatetereka hata kidogo,"alisema Spika Sitta ambaye siku za nyuma aliapa kupambana na mafisadi hadi ushidi upatikane.
Alisema hivi sasa kumeibuka tabia ya baadhi ya watu nchini, kulazimisha yale wanayoyafanya wao yaonekane kuwa ndiyo ya ukweli kabisa hata kama wanayoyafanya ni ya uongo.
"Katika nchi yetu kumeibuka tabia ya waovu wanaosambaza uongo uliopakwa asali, hugeuza uongo huo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo, siwezi kukubaliana nao sababu ni waovu,"alisisitiza kauli ambayo imetafsiriwa kuwa anawalenga wale ambao walitaka avuliwe uanachama wa CCM katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho.
Kauli hiyo iliungwa mkono na mkewe ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margaret Sitta, ambaye alinukuu kauli ya Askofu Norbert Mtega wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Songea, ambaye alisema kuwa maisha ni mpito na kifo ni faida, alipokuwa akizungumza katika msiba wa baba wa Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama.
"Kauli ile ya Askofu Mtega tunaichukua na sasa tunaifanya kuwa falsafa ya maisha yetu, kwa maana hiyo kwetu sisi sasa maisha ni mpito tu na kifo kwetu ni faida,"alisema waziri huyo.
Kwa upande wake mume wake (Sitta) alisema taifa linaelekea kubaya kwa sababu baadhi ya watu wanajaribu kulazimisha yale wanayoona kuwa ni sawa na kwamba wanatumia gharama kubwa kufanya hivyo.
Mwenyekiti wa umoja wa makanisa mkoani Tabora, William Lusito, alisema umoja huo umetokana na azimio kuwa nyuma ya Spika na kwamba, hawatakubali kumuona akiyumbishwa na kundi la aina yoyote.
Spika huyo pia alielezea kusikitishwa kwake juu ya hatua ya baadhi ya watu, kusambaza maeneo yasiyokuwa na ukweli kuhusu yeye, wakidai kuwa aliomba radhi kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).
Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, aliyasema hayo jana nyumbani mjini Urambo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, akiwa katika ziara yake aliyoianza rasmi jana.
Mamia ya watu wa jimbo hilo, walijitokeza kwa wingi kumlaki mbunge wao.
"Kwa kuwa mimi niliwekwa katika kikao cha kujieleza, mimi ninarudisha swali kwa hao wanaosambaza hayo, waeleze niliomba radhi kuhusu kipi,"alisema.
Alisema hataki kuzungumzia yaliyotokea ndani ya kikao, lakini kwa kuwa kuna watu wamejitokeza kuzungumzia hayo, kuna haja kwa watu hao kueleza sababu za yeye kuomba radhi katika kikao cha siku mbili cha NEC.
"Ninachokisema ni hivi, kwa kuwa kikao cha NEC kimefikia mwisho na chama chetu kikatoa maamuzi ya kuunda jopo la watu watatu wenye busara wakaangalie hali ya Bunge letu, watawahoji wabunge, wanachama na kisha tutayasikia maamuzi yao Oktoba basi ni bora tusubirie matokeo yao,"alisema.
Alisema yeye kama mtu mwenye subira atakuwa mtu wa ajabu mno, kuzungumzia yaliyotokea ndani ya kikao cha NEC na CC na kwamba, kauli na maelezo yanayotolewa na baadhi ya watu kutaka kubadilisha picha halisi ya kile kilichotokea ni upotoshaji na inasikitisha.
"Nasikitishwa na makao makuu ya CCM Dodoma kwa ambavyo wanavyoshughulikia baadhi ya mambo, kwani ingekuwa kwa mara moja, kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chilligati, ilitosha kumaliza mambo.
Alisema, hata hivyo, inashangaza kuona mambo hayo yanarudiwa wakati yanapaswa kushughulikiwa na na kamati maalumu.
"Inashangaza kuona mara anazungumza Katibu Mkuu, mara anazungumza mwanachama tu wa CCM, tena mambo ambayo ni dhahiri yanayoonekana kuwa ni tuhuma bila ya kuacha vyombo vilivyoundwa na chama vifanye maamuzi yake," alisisistiza Sitta.
"Nimesikitishwa na wakuu wa chama ambao waliruhusu, Chenge (Andrew) na Lowassa (Edward) wapokelewe, lakini wanazuia katibu na mwenyekiti wasinipokee, ingawa wanachama walijitokeza kunipokea, hii ndiyo inatufanya wanachama tuamini kuwa kuna wanachama wenye haki na wasio na haki, hii si dalili nzuri,"alisema.
Alielezea kushangazwa na hatua ya makao makuu ya CCM ya kuuzuia uongozi wa mkoa wake usimpokee.
Alisema hivi karibuni amesikia kauli zilizotolewa na viongozi wakuu wa CCM zikionyesha kuegemea upande mmoja, jambo ambalo si dawa na linaonekana kutotumika kwa busara katika wakati huu ambapo kikao cha NEC kimemalizika .
Hata hivyo, aliwashukuru wanachama wa CCM wa Jimbo la Urambo Magharibi, waliojitokeza kwa wingi kumlaki na akawataka kutokata tamaa na waendelee na moyo huo.
Kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kuwa amekuwa akiendesha Bunge kwa kuwapanga wabunge, alikanusha na kwamba, utaratibu wa Bunge unafahamika.
"Vikao vya Bunge vinaendeshwa kwa taratibu na kanuni, kila mbunge anayetaka kuchangia anapitisha hoja zake kwanza kwa Katibu wa Bunge na au kutoa taarifa kwa katibu huyo, hivyo hakuna ukweli wowote kwamba nimekuwa nikipanga mambo,"alisema.
Spika Sitta juzi huko Urambo alipata mapokezi makubwa baada ya kuwasili jimboni humo ikiwa ni mara ya kwanza tangu apate msukosuko kutoka kwenye vikao vya chama chake.
Mwandishi wetu aliyekuwa huko, alisema Sitta alipokelewa na wapigakura wake wakiwa na pikipiki zaidi ya 100 na kutembea naye kwa maandamano kwa umbali wa kilometa moja.​


www.mwananchi.co.tz

Rekebisha bandiko lako mkuu, punguza papara
 
Naunga mkono sana sana ni kweli ni chama cha wachache wenye kulindana kwa gharama yeyote......imenisikitisha sana....Vijana tuungane tulete mabadiliko ya kifikra na kiutendaji na kuwang'oa kabisa hasa hili genge la mahafidhina......wa bara...hatuwezi kufika nchi ya ile...kwa mwendoo huu
 
Kilichotokea Dodoma katika Mkutano wa Kamati Kuu na NEC ya CCM kimethibitisha mambo matatu ambayo wataalam wamekuwa wakiyahofia kwa muda mrefu: (1) Kwamba CCM haiwezi kulinda maslahi ya taifa bali kimegeuka kuwa chama kinachotumiwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi. Mafisadi, wauza unga na matapeli wa kimataifa wamegundua udhaifu huo na wameweza kuutumia kuiteka CCM kama njia nyepesi na ya uhakika ya kuiteka serikali na hivyo kuiteka nchi. Awamu ya Tatu iliwakaribisha hadi uvunguni, na sasa Awamu ya Nne imejikuta ni mfungwa wao.
Kinachowaponza viongozi leo ni tamaa ya "shanga na kaniki" kama zilivyowaponza akina Mangungo, Sultani wa Msovero, zama za kuuza nchi na kuuza wananchi utumwani. Historia inajirudia nasi tunaiangalia kijingajinga tu.
Kilichotokea Dodoma ni "dress rehearsal" ya mwaka 2010, na kimethibitisha kwamba kwa mfumo huo wa CCM na mtindo ulioko sasa wa kujadili na kufikia maamuzi, siyo CC wala NEC wala Mkutano Mkuu wa CCM unaoweza kuwazuia mafisadi, wauza unga na matapeli kuwasimika vibaraka wao katika uongozi wa chama na serikali, ikiwa ni pamoja na/au hasa nafasi ya urais. Dodoma imeonyesha wazi kuwa kikundi kidogo chenye pesa za wizi na dhamira kikijipanga vizuri kinaweza, tena kwa ulaini kabisa, kuiburuza CC na NEC na hivyo serikali na nchi nzima na kuzitumia wanavyotaka

Sultani wa Msovero hakuuza nchi. Acha kudanganya hapa na acha kutumia siasa.
 
Sultani wa Msovero hakuuza nchi. Acha kudanganya hapa na acha kutumia siasa.

Kuna mtu mmoja maarufu alikuwa kitumia usemi "Hoja hujibiwa kwa hoja", sasa kama huna hoja ya kujibu hoja ya mwenzako kwani ni lazima uchangie hoja yake?. Regardless na unavyoona wewe huyu mwanzisha thread ameeleza kitu ambacho kila mtu makini atakuwa anakifikiria japo katika uwakilishi wa hoja yake hakuwa consistent kwani katika vitu vitatu ameeleza kimoja tu.

Ila Hoja yake ni nzito na ina ukweli. Ya mangungo au Karl Peters et al ni katika kuweka kivumishi cha hoja yake tu. sasa kama wewe ni mwalimu wa historia ilikuwa ni busara kuweka ukweli badala ya kushutumu
 
mie naamini kwamba mabadiriko ya jinsi nchi yetu inavyoongozwa inaweza kutokea ndani ya ccm kutokana mitafaruku kama hii ndani ya chama chao.kwahio tuombe mungu wana ccm waendelee kugawanyika hili wale wachafu wataogopa kufanya maovu yao kuepukana na kuwekwa wazi mbele ya jamiii.nisichoomba mie kutokea ni kwamba wale wachafu wakawazidi nguvu wale wasafi kwani mpaka sasa hivi naona kama sisi wananchi hatujaonesha vya kutosha jinsi gani tunawaunga mkono viongozi wasafi wanaotetea haki zetu.kazi hipo 2010.
 
Pundamilia07,
Mkuu mimi natoka nje kidogo ya hoja ya Mh. Sitta ila napenda kuelewa nini maana ya maamuzi haya ya chama CCM - wanaposema:-

8. KUHESHIMU VIONGOZI WASTAAFU
Mzee Mkapa anastahili pongezi sio kejeli, anastahili heshima na sio dharau, anastahili kuenziwa na sio matusi.
Kwa kuzingatia hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa inatoa wito kwa wana CCM na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yetu waache mara moja kumchafua na kumkejeli Mzee Mkapa na badala yake apewe heshima anayostahili na aachwe apumzike kwa amani.

Mkuu haya maneno yanaonyesha wazi kama ni vitisho kwa wananchi! kisha inaonyesha wazi chama hiki hakielewi kabisa nini msimamo wa wananchi na wanachosema kuhusu UFISADI kiasi kwamba malalamiko yao yanaonekana kuwa ni MZAHA na KEJELI..

Hivi kweli kikao kile kinafikiri wananchi wanamkejeli Mkapa kuhusiana na Ufisadi?.. Sidhani kama chama hiki kinaelewa uzito wa Ufisadi wananchi wanaozungumzia..
Ndio maana kila kitu kwao ni mzaha mzaha tu na kutumia maguvu badala ya elimu..Hivi kweli kuna jambazi au criminal yeyote kwa tafsiri fulani, anayeweza kusamehewa mauaji au wizi wake kwa sababu tu aliwahi fanya mazuri fulani before kabla ya ujambazi wake..Na wapi hili neno linasimama mkuu wangu tunaposema - NO one is above the Law!
 
Last edited:
Back
Top Bottom