Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

- More Dataz, mwingine aliyezungumza ndani ya NEC ni Kapteni Komba, another joker sasa sikiliza this one, ".....kaka yangu Sitta pole sana, naomba nikuambie wewe na wajumbe wengine wote humu ndani kwamba Lowassa na kundi lake ni marafiki zangu sana na siwezi kuachana nao hata kidogo....."

"...wewe kaka yangu Sitta nimekuambia mara nyingi sana kwamba haya mambo yako na hicho kikundi chako unaenda sana nje ya mstari, lakini hukutaka kunikisia, sasa ona yaliyokukuta ni bora tu urudishe kadi yetu kaka...."

- And more dataz ni kwamba Karume, aliahirisha kuhudhuria dakika za mwisho, yeye na watu wake wa karibu kama kumi, infact aliwapigia simu hata baadhi ya wajumbe wengine waliokuwa Dodoma tayari kurudi Visiwani maramoja, huku akiwaagiza kwa ukali kwamba wasihudhurie kikao hicho cha NEC. The dataz ni kwamba alimfahamisha Mwenyekiti wa CCM kwamba ana homa nzito sana, lakini cha ajabu kesho yake akaenda kukutana na Balozi mmoja wa nje somewhere in Dar.

- Na dataz zaidi ni kwamba sasa tuna a confirmed report kwa 100% kwamba wajumbe 40 in total ndio walioongea kwenye kikao hicho, na Dk. Mwakyembe ni mmojawapo kama tulivyosema mwanzoni, kama mambo yakienda akama yalivyo sasa, then kesho nitakuwa na more dataz za majina yote 40 na waliyoyasema huko NEC.

- Na more dataz ni kwamba hii game ya NEC, Dodoma imetengenezwa na Lowassa, akishirkiana na baadhi ya watu wa idara ambao wamekua wakisikika wakidai kwamba sasa baada ya kikao cha juzi chama kimekua ni imara tena. According to the more dataz ni kwamba the deal ni kumrudisha Lowassa kwenye Cabinet Mwaka 2010, kama waziri wa Nje, au Ulinzi ili Mwaka 2015 achukue kiti cha Urais bila tatizo, kwa hii kasi nina wasi wasi kwamba lisemwalo lipo! na Haya maneno yalitamkwa na Karamagi somewhere, akijaribu kumshawishi mzito mmoja wa CCM kujiunga nao mafisadi.

Wakuu hatujamaliza tutaendelea na hizi dataz kama kawa, as soon as possible! na Mungu Aibariki Tanzania na JF Idumu Millele, where we dare!

Respect.

Field Marshall Es!

Kama muheshimiwa karume aliahirisha kuhudhria hicho kikao muhimu na ujumbe wake mzitona kuamuru waliokuwa Dodoma kurudi Zanzibar basi nimeamini kabisa CCM imefikia ukingoni na tayari kaburi lake limechibwa hawaamini amini lakini ukweli ndio huo huo mgawanyiko na ufa umekuwa mkubwa kupita KIasi

FMES huo waraka uliotumiwa nauona ni wa kweli kutoka kwa watu ambao wanaona kwamba mchango wako unaamusha moyo wa wazalendo kwa wtu wengi huu mtandao una non bloggers na non members ambao wamekuwa wakipata habari na kusoma mambo mengi yanayo postiwa kila siku hapa
Mimi mwenyewe nilishawishika kujiunga mwaka huu baada ya kupokea posts zinazo wekwa kwenye jamvi hili toka mwaka 2007 kwa hiyo wasomaji sio wana JF tu au members tuu watu wengi sana sana tena sana

Endelea kutuhabarisha tuu na hakuna mwenye nchi ,ni yetu wote na hatutakaa kimya na kuacha kukemea maovu eti tukiogopa kufa,bila shaka kila aliyezaliwa na mamaye ipo siku atakuafa kwani kifo ni wajibu.Itakuwa heshima kubwa kama mtu atakufa kwa sababu ya kutetea maslahi ya nchi yake
Nakupongeza sana kwa ujasiri
 
Nyepesi nyepesi zinazojiri kutoka NEC ya CCM Dodoma jana Spika Samwel Sitta kawekwa mtu kati kwa namna anavyolipeleka Bunge mpera mpera.

Miongoni mwa wachangiaji waliomshambulia wazi wazi ni Mwenyekiti wa CCM Shinyanga ambae bila kumung'unya maneno alimwambia Sitta alirudishe kadi ya CCM. Kwa ujumla wachangiaji wengi wameonyeshwa kutoridhiswa na utendaji wa Sitta isipokuwa wawili tu Eng Stellah Manyanya na Mh John Shibuda.

Chungu kimefunikwa na kikao kinaendelea leo ambapo tusishangae kusikia Sitta kasitishwa U-Spika.

Stay tuned...

Hapa ndiyo mwanzo wa habari!
 
- ku-reconcile makundi yaliyoko ndani ya CCM kuelekea uchaguzi wa 2010 kutokana na kauli nzito ya JM, ambaye the dataz ni hakutaka kuhudhuria kikao hiki toka last week amejificha UK,

- Ni mvutano ambao bado unaendelea hadi sasa what to do na makundi, kundi la "mashujaa" likiongozwa na Six, linagoma kata kata any reconciliation
Respect.

FMEs!

Mashujaa, hawa ni mashujaa wa nini? Je lengo lao ni nini? Ultimately wanataka ku-achieve nini?
 
- The dataz ni kwamba jumla ya shillingi millioni 50 zilitumika hasa kuwanunua wajumbe wa visiwani, ambao wote kwa pamoja walililia kichwa cha Spika lakini hela zilizotumika hazikuwa nyingi sana,
Million 50, nani alizitoa, Mengi au Karamagi?



- The dataz pia ni kwamba Muungwana, was caught in the middle lakini the message was very clear na maneno maneno yake ndani ya kikao kwamba Spika anahitaji ku-watch his back na Muungwana, kwa sababu kwa mara ya kwanza hakuwa na maneno mazuri sana kuhusu Spika.
Hii inahitaji ushahidi wa kutosha, tena wenye kujitegemea na wala sio kama ule wa kesi ya zombe.

Duh, kuelekea 2010 tutasikia mengi na mengine ya ajabu.
 
Field Marshall ES;555065]-


Million 50, nani alizitoa, Mengi au Karamagi?





Hii inahitaji ushahidi wa kutosha, tena wenye kujitegemea na wala sio kama ule wa kesi ya zombe.


Respect.

FMEs!

Duh, kuelekea 2010 tutasikia mengi na mengine ya ajabu.[/QUOTE]
Hilo ni trela tu mkuu,tutegemee mambo zaidi ya ajabu aisee...Tutege tu macho na masikio yetu
 
-
Mashujaa wengi wanaponzwa sana na midomo yao mirefu huko pembeni, wengine wanaongea mno kwa kuamini kwamba wanakubalika na kila kiongozi, kumbe hao hao wanaishia kuwauza kwa mafisadi

Ni mashujaa gani hao wenye midomo mirefu, je ni Anne Kilango, Selelii au nani?

- I hope they get the strong message ya hiki kikao ya kufunga midomo yao pasipohusu, au kwa maneno mengine shut up! garademit I am very upset!
Respect!

FMEs!

Wasome alama za nyakati, kama wao wanaona kuwa hawawezi kuwa ndani ya CCM basi ni wakati muafaka waanzishe chama kingine, halafu waingie kwenye uchaguzi washike nchi.
 
Duh, kuelekea 2010 tutasikia mengi na mengine ya ajabu.
Hilo ni trela tu mkuu,tutegemee mambo zaidi ya ajabu aisee...Tutege tu macho na masikio yetu[/QUOTE]

Taratibu naanza kukunbuka maneno ya Mzee Tingatinga kuwa alisema CCM ina mbinu nyingi za kuweza kushinda uchaguzi. Nina wasiwasi na thread hii jinsi inavyoondoa mawazo ya washindani wa CCM katika kuwasiliana na wananchi. Mimi ni CCM damu lakini ninawaonya wale wapinzani wa kweli wa CCM dhidi ya thread hii kwani ina athari kubwa sana kwenye harakati zenu za kisiasa. Makada wapo kazini sasa in full swing to brainwash you. We in CCM tunahitaji upinzani wa kweli na wenye nguvu kutoka kwa watu makini.
Haya ni maoni yangu binafsi
 
Taratibu naanza kukunbuka maneno ya Mzee Tingatinga kuwa alisema CCM ina mbinu nyingi za kuweza kushinda uchaguzi. Nina wasiwasi na thread hii jinsi inavyoondoa mawazo ya washindani wa CCM katika kuwasiliana na wananchi. Mimi ni CCM damu lakini ninawaonya wale wapinzani wa kweli wa CCM dhidi ya thread hii kwani ina athari kubwa sana kwenye harakati zenu za kisiasa. Makada wapo kazini sasa in full swing to brainwash you. We in CCM tunahitaji upinzani wa kweli na wenye nguvu kutoka kwa watu makini.
Haya ni maoni yangu binafsi
Ndio maoni binafsi yasiyona mashiko!!!!!!!!!!!!!! Wala hayasaidii chochote wapinzani wa kweli wa sisi M bali yanaendelea kuwaporomosha ninyi wakina maneno na vinywa wazi.
 
Kama muheshimiwa karume aliahirisha kuhudhria hicho kikao muhimu na ujumbe wake mzitona kuamuru waliokuwa Dodoma kurudi Zanzibar basi nimeamini kabisa CCM imefikia ukingoni na tayari kaburi lake limechibwa hawaamini amini lakini ukweli ndio huo huo mgawanyiko na ufa umekuwa mkubwa kupita KIasi

FMES huo waraka uliotumiwa nauona ni wa kweli kutoka kwa watu ambao wanaona kwamba mchango wako unaamusha moyo wa wazalendo kwa wtu wengi huu mtandao una non bloggers na non members ambao wamekuwa wakipata habari na kusoma mambo mengi yanayo postiwa kila siku hapa
Mimi mwenyewe nilishawishika kujiunga mwaka huu baada ya kupokea posts zinazo wekwa kwenye jamvi hili toka mwaka 2007 kwa hiyo wasomaji sio wana JF tu au members tuu watu wengi sana sana tena sana

Endelea kutuhabarisha tuu na hakuna mwenye nchi ,ni yetu wote na hatutakaa kimya na kuacha kukemea maovu eti tukiogopa kufa,bila shaka kila aliyezaliwa na mamaye ipo siku atakuafa kwani kifo ni wajibu.Itakuwa heshima kubwa kama mtu atakufa kwa sababu ya kutetea maslahi ya nchi yake
Nakupongeza sana kwa ujasiri

- Mkuu tupo pamoja sana, huenda utabiri wako ukawa kweli kwamba CCM inakaribia kufika mwisho, ninaanza kuamini kwa pole pole!

Respect.


FMEs!
 
Hii article hapa chini imeeleza vizuri kabisa NEC ya CCM ilijadili nini. Haya mengine watu wanayoyaeneza humu kama 'dataz' ni ya kiushabiki na hayana source zaidi ya kuwa ni mambo ya kupika kwa manufaa binafsi.

Ni vema tukakumbushana baada ya mkutano mkuu wa CCM kupitisha jina la mgombea mmoja wa kiti cha urais 2005 basi kambi zote zilivunjwa na kuwa kambi moja tu ya mgombea wa CCM. Wale ambao wanaona kuwa mgombea aliepo sasa bado hawajaridhika na matokeo yale wakae kimya wasubiri 2015 umshauri baba au mama yako au mjomba au shangazi yako au rafiki yako agombee tena, lakini si kutaka kukipaka matope chama kwa manufaa binafsi.


ABDULWAKIL SAIBOKO, 21st August 2009

THE ruling party, Chama Cha Mapinduzi (CCM), has refuted reports that the just ended party’s National Executive Committee (NEC) discussed and warned the Speaker of the National Assembly, Mr Samwel Sitta, for sloppy performance.

The Party’s Deputy Head of Propagation, Mr Tambwe Hiza, told reporters in Dar es Salaam yesterday that the claims by the opposition officials were unfounded and aimed at tarnishing the party’s image.

“The party has received with great disappointment negative reports that have appeared in the media for the past few days since NEC meeting began in Dodoma. The meeting had no any agenda against the Speaker,” he said. Mr Tambwe further said that what transpired was a general discussion on the political climate and the utterances of some leaders including members of the National Assembly and the House of Representatives.

“In the meeting of over 200 members there might be one of them who said was not happy with the way the Speaker was executing his duties and if such a view is not supported by all other members, we can not therefore conclude as the party’s agenda,” Mr Tambwe clarified.

He said that though the constitution does not specify Speaker as a member of NEC or Central Committee (CC), the party’s constitution demands that he must be a member and while in the party’s meeting he was entitled to obey it.

Meanwhile, the Party’s Lawyer , Mr Glorious Luoga, said that the NEC did not deprive its MPs from practising their constitutional right, that is, freedom of expression, but it rather warned them from trading harsh words.

“The meeting concluded that MPs should have a common stand on topical issues especially those within the party’s manifesto such as fighting corruption, the MPs are not allowed to own these issues.

This approach is used by parties all over the world,” he said. He said that it was bad for the party to tolerate exchange of words among its leaders within and outside the parliament walls because that would end up weakening the party.

It was reported early this week that there was failed attempt to expel Mr Sitta from the ruling party during NEC meeting in Dodoma. The reports had it that some members accused Mr Sitta of sloppy performance as Speaker and that this was dangerous to the survival of CCM.

The reports claimed that by allowing MPs to debate serious corruption allegations against some top and influential party officials in the House, Mr Sitta had weakened the ruling party which warranted his resignation as Speaker.
 
duh! yaani ukweli wenyewe utoke kwa Tambwe Hiza? Pundamilia07 stop jokes please, au wewe ndo Tambwe maana comments siku zote zimekaa kipropaganda sana.

mkuu, mimi binafsi nilimsikia Mhe. John Chiligati (msemaji wa CCM) akikiri kwamba spika alishambuliwa kwa sababu bunge limekuwa kama commedy na spika kama kiongozi wa bunge amewaachia na wakati mwingine naye anawa-support. Chiligati aliongea hayo mbele ya waandishi wa habari na bbc/swahili walirusha hewani.

achana na propaganda za Tambwe. Kama wewe unaipenda kweli CCM basi kubali ukweli na muone namna ya kusafisha hali ya hewa lakini siyo kukataa ukweli au kujitahidi kuwadanganya wananchi kwani ndo mnazidi kupoteza heshma na kuonekana wasanii tu.
 
pundamilia,
YOU MUST BE OUT OF YOUR MIND!au niseme na wewe upo 'kazini'
 
HALMASHAURI KUU YAAZIMIA MSHIKAMANO ZAIDI NDANI YA CHAMA

UTANGULIZI


Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya Mkutano wa kawaida tarehe 16-17 Agosti, 2009 chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika mkutano huu Halmashauri Kuu imejadili masuala mbali mbali kuhusu hali ya kisiasa nchini, maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura, pia imefanya uteuzi wa wagombea katika nafasi mbalimbali.

Baada ya kujadili masuala hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya maamuzi yafuatayo:-

1. MAANDALIZI YA UCHAGUZI
(a) Serikali za Mitaa
Halmashauri Kuu ya Taifa imepitisha ratiba ya CCM kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa; kwa mujibu wa ratiba hiyo muda wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea wa CCM kwa uongozi wa Vitongoji, Serikali za Vijiji na Mitaa ni toka tarehe 10/8/2009 hadi 20/8/2009.
Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito kwa wana CCM na wapenzi wa CCM katika ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Mitaa wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa kuzingatia ratiba ya CCM na pia ratiba ya wasimamizi wa Uchaguzi huu (TAMISEMI).

Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imewahimiza wana CCM na wapenzi wa CCM wajitokeze kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kuanzia tarehe 4/9/2009 hadi 25/9/2009 na kwamba muda ukiwadia wajitokeze kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi hapo tarehe 25/10/2009.

(b) Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura - Pemba

Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kupokea taarifa kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Kisiwani Pemba, imetoa wito kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ihakikishe zoezi hilo linasimamiwa kwa makini, na liendeshwe kwa haki na kwa utulivu; na kwamba Serikali ya Mapinduzi ihakikishe kwamba kila mwenye haki na sifa ya kujiandikisha anapata haki hiyo, na wale wasio na sifa wasiruhusiwe kujiandikisha.

Kimsingi zoezi hili sharti liendeshwe kwa kuzingatia sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na sio vinginevyo.

2. KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI

Halmashauri Kuu ya Taifa imetafakari upya mapendekezo yake ya awali kuhusu utaratibu wa kuongeza idadi ya wanawake katika Bunge la Muungano na katika Baraza la Wawakilishi. Mapendekezo mapya ni kama ifuatavyo:-

(a) Kwamba kwa kuwa idadi ya Wabunge wote kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 66(1)(b) ni 249, viti asilimia arobaini (40%) itengwe kwa ajili ya wanawake, yaani viti 100.

(b) Kwamba ukomo wa viti Bungeni ubaki 360, hivyo pendekezo hili litaongeza idadi ya viti kutoka 323 vya sasa hadi 349, na vitabaki viti 11 kufikia ukomo wa viti (360) Bungeni. Hali hii inawezesha Tume ya Uchaguzi kuongeza idadi ya majimbo mapya 11.

(c) Utaratibu wa asilimia 40 utakapotumika utawezesha kupatikana kwa Wabunge Wanawake 100 kwa viti maalum pekee, idadi ambayo ikijumulishwa na wa kuchaguliwa ambao kwa sasa ni 18, watano wa kuteuliwa na wawili kutoka Baraza la Wawakilishi, tutapata Wabunge wanawake 125. Kiwango hiki ni sawa na asilimia 50 ya Wabunge wote waliotajwa kwenye Ibara ya 66(1) (b) ya Katiba.

(d) Ili kufikia lengo la kupata wabunge wanawake 50%, wanawake hawana budi kushindana kwa bidii katika majimbo. Kwa hali hii Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza CCM katika ngazi zote zifanye uhamasishaji wa Wanawake wengi kwenda kugombea katika majimbo ya uchaguzi mwaka 2010 ili kuongeza Wabunge zaidi ya 18 waliopo hivi sasa.




3. UTEUZI WA WAGOMBEA UENYEKITI WA WILAYA

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, imepitisha wana CCM walioomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika Wilaya za Rorya, Tarime na Arumeru.

Nafasi za Tarime na Rorya zimetokana na kugawanywa kwa wilaya ya Tarime na kuwa wilaya mbili na ile ya wilaya ya Arumeru imetokana na kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya hiyo, Ndugu Lucas Lobulu aliyefariki Mei 6, 2009.

Waliopitishwa kugombea nafasi hizo ni:-

Wilaya ya Arumeru
1. Ndugu Jeremiah Saruni Kaaya
2. Ndugu Gabriel Kilale Nnko
3. Ndugu Joseph Ole Loning’o Saivoiye

Wilaya ya Tarime
1. Ndugu George Mkama Chacha
2. Ndugu Bogomba Rashid Chichake
3. Ndugu Peter Keba Wangwe

Wilaya ya Rorya
1. Ndugu Leonard Yodal Ambonya
2. Ndugu Jomoko Mjee Kateti
3. Ndugu Ramadhan A. Nyanganira

Wilaya husika zitafanya uchaguzi kwa ratiba itakayoandaliwa baadaye.

4. CHAGUZI NDOGO BUSANDA, MAGOGONI NA BIHARAMULO

Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa kujadili tathmini ya chaguzi ndogo katika majimbo ya Busanda, Magogoni na Biharamulo, imewashukuru na kuwapongeza wale wote waliofaikisha ushindi wa CCM katika Uchaguzi mdogo wa Majimbo ya Ubunge ya Busanda (Mwanza) na Biharamulo Magharibi (Kagera) pamoja na Uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Magogoni, Zanzibar.

Aidha, Halmashari Kuu pia imetoa pongezi za dhati kwa wana-CCM, wapenzi wa CCM na wananchi kwa ujumla kwa ushindi waliokipatia Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi hizo ndogo za Ubunge, Uwakilishi na za Udiwani katika Kata 10 za Tanzania Bara.

Kutokana na ushindi huo, kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kiliwaomba wana-CCM, wapenzi wa CCM, wakereketwa na wananchi kwa ujumla kuendelea kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee na majukumu ya kumkomboa Mtanzania na kudumisha amani na utulivu.

5. MAHAKAMA YA KADHI

Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhika na hatua zinazochukuliwa na Serikali za kulipatia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara. Moja ya hatua hizo ni uundaji wa Kamati ya mazungumzo baina ya viongozi wa dini ya Kiislam na Serikali kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nje ya mfumo wa Serikali.

Aidha, Halmashauri Kuu imesisitiza kwamba iwapo wapo Waislam wanaona haki zao hazikamiliki bila ya kuwa na chombo cha aina hiyo, wasizuiliwe. Waruhusiwe kuanzisha Mahakama ya Kadhi wao wenyewe na Serikali isijihusishe kuiendesha mahakama hiyo kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imejiingiza katika shughuli za kidini; na kwamba Mahakama hiyo isihusike na kesi za jinai wala madai, bali ihusike na masuala ya ndoa, talaka na mirathi.

6. WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU (RC)

Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuzingatia waraka wa Maaskofu, na hasa malumbano na hisia tofauti zilizojitokeza kuhusu waraka huo, imeelekeza kwamba viongozi wakuu wa nchi wafanye mazungumzo na viongozi wa dini zote ili kutafuta njia tulivu ya kusafisha hali ya hewa na kujenga umoja na utengamano katika jamii yetu.

7. MALUMBANO YA VIONGOZI

Kuhusu tabia iliyozuka hivi karibuni ya baadhi ya Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Viongozi wa Chama kutoa matamshi hadharani yenye mwelekeo wa kuchafuana majina, na yanayoashiria kuvunjika kwa umoja na mshikamano ndani ya CCM na Serikali zetu, na pia yenye mwelekeo ya kudhoofisha muungano wetu, Halmashauri Kuu ya Taifa pamoja na kukemea vikali tabia hii, imetoa maagizo yafuatayo:-

(a) Kwamba kuanzia sasa viongozi wote wa CCM warejee katika nidhamu ya Chama ya kuzungumzia masuala ya Chama katika vikao rasmi vya Chama na sio vinginevyo.




(b) Kamati za Wabunge wa CCM, na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM zitumike kujadili masuala yahusuyo CCM ndani ya vyombo hivyo.

(c) Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watumie taratibu zilizopo katika kushughulikia kero za Muungano badala ya kufanya kwa suala la mafuta kwa upande wa Zanzibar.

(d) Viongozi watakao vunja maadili haya watakuwa wamejibainisha kwamba hawana nia njema na CCM, na watahesabiwa ni wasaliti wa CCM hivyo Chama hakitasita kuwapa adhabu kali, ikiwa ni pamoja ya kuvuliwa uongozi na hata kufukuzwa katika Chama.

(e) Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito kwamba mapambano dhidi ya rushwa na maovu mengine ni jukumu la wana CCM wote na raia wema wote kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ahadi 4 ya WanaCCM. Halmashauri Kuu ya Taifa imeonya kuhusu dhana inayojengeka kwamba vita dhidi ya rushwa na ufisadi inahusu kikundi kidogo tu cha wana CCM, usahihi ni kwamba vita hii ni ya wana CCM wote kwa mujibu wa Katiba ya CCM vita hivi lazima iendelee kuhusisha wana CCM wote na wananchi wote wenye mapenzi mema na nchi yetu.

(f) Kwa kutambua kuwepo matatizo ya matamshi na vitendo visivyoridhisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi, Halmashauri Kuu ya Taifa imeamua kuunda Kamati Ndogo ya kutafuta undani wa matatizo hayo na kupendekeza kwa Kamati Kuu njia za kuyatatua. Aidha, Kamati hiyo pia itaangalia utendaji kazi wa Kamati za Chama katika Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa nia ya kubaini upungufu uliopo ili kupendekeza kwa Kamati Kuu kuhusu njia za kurekebisha. Pia, Kamati itaangalia masuala ya uendeshaji wa shughuli za Bunge na Baraza la Wawakilishi na kushauri namna ya kuimarisha, pale panapostahili.

Kamati hiyo itaongozwa na Mzee Alli Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Wajumbe wengine ni Mzee Pius Msekwa Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) na Ndugu Abdulhaman Kinana.

8. KUHESHIMU VIONGOZI WASTAAFU

Halmashauri Kuu ya Taifa imewakumbusha wana CCM, Viongozi na Watanzania kwa jumla kuhusu umuhimu wa kudumisha utamaduni wa kuwaheshimu na kuwaenzi viongozi wastaafu, hususan Marais wastaafu.

Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imesikitishwa sana na hali iliyojitokeza Bungeni ya kutoa maneno ya kejeli dhidi ya Mzee Benjamin W. Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu.

Halmashauri Kuu ya Taifa imesisitiza kwamba Mzee Mkapa katika kipindi chake ameliongoza Taifa letu kwa ufanisi mkubwa, aliinua hali ya uchumi, aliendeleza miundombinu, aliendeleza huduma za kijamii hasa elimu, afya, maji na kwa jumla alilijengea heshima kubwa Taifa letu.

Mzee Mkapa anastahili pongezi sio kejeli, anastahili heshima na sio dharau, anastahili kuenziwa na sio matusi.

Kwa kuzingatia hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa inatoa wito kwa wana CCM na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yetu waache mara moja kumchafua na kumkejeli Mzee Mkapa na badala yake apewe heshima anayostahili na aachwe apumzike kwa amani.



9. UTEUZI WA MAKATIBU WAPYA WA MIKOA

Halmashauri Kuu ya Taifa imewateua wafuatao kuwa Makatibu wa Mikoa:-

(1) Ndugu Sauda Mpembalyoto (Katibu wa Wilaya ya Hai)
(2) Capt. (Mst) Frarten Kiwango (Katibu wa Wilaya ya Kibaha Mjini)

Hawa wanajaza nafasi zilizoachwa wazi na Ndugu Amina Makilai aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Pwani na sasa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT, pia Ndugu Salum Msabah aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Kigoma na sasa amerejeshwa Makao Makuu ya CCM kuongoza Kitengo cha Propaganda.

10. UCHAGUZI WA MJUMBE WA NEC KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI

Nafasi hii iliachwa wazi na marehemu Richard Nyaulawa na ilikuwa inawaniwa na wagombea watatu.

Kutokana na kura za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa aliyechaguliwa ni Ndugu Jasson Rweikiza aliyepata kura 88.

Wengine waliogombea nafasi hii ni Ndugu Ramadhani Maneno kura 85 na Ndugu Sifa Swai kura 46.

Imetolewa na:-

Capt. (Mst) John Z. Chiligati (Mb),
KATIBU WA HALMASHARI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
17/8/2009
18 Aug 2009



Source: Tovuti ya CCM​
 
Makamba: CCM ina jeuri ya kumbana Sitta

• Mapokezi mazito ya Spika Sitta Tabora leo

na Deogratius Temba

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni mstaafu Yusuf Makamba, amesema chama hicho kina haki ya kumhoji Spika wa Bunge, Samuel Sitta na wabunge wote wa chama hicho, kwani wote ni mali ya chama hicho tawala.
Kauli hiyo ya Makamba imekuja siku chache baada ya wadau mbalimbali, wakiwemo wasomi na wanasiasa wa vyama vya upinzani, kuhoji uhalali wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kumuonya Spika Sitta, kutokana na hatua yake ya kutoa uhuru kwa wabunge wa chama hicho kuinyanyasa serikali na chama hicho tawala.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, muda mfupi mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Manzese Bakheresa, Wilaya ya Kinondoni, Makamba alisema CCM ina haki ya kumhoji mbunge yeyote wa chama hicho, na hata Spika wa Bunge, kwani Bunge hilo ni mali ya chama tawala.

“Sisi ndio tunaotawala, tunayo haki ya kumhoji na kumuuliza namna anavyoliongoza Bunge. Serikali ni yetu, mnataka nani amuulize?” alihoji Makamba na kuongeza:

“Chama hakitaacha kuwahoji wabunge wanaotoka nje ya misingi ya chama na kutoa maneno yanayosababisha kukichafua. Kama wana maneno yao wayalete ndani ya chama, kwanini wakapige kelele za ufisadi nje ya chama?

“Ukijichanganya ukatoa maneno ambayo hatuyataki, wenye chama chao watakuita na kukuuliza yanayohusu chama… kama ni ufisadi wayaseme ndani ya chama. Kama ni ya Bunge wayaseme ndani ya Bunge na si kwenda kuzungumza mitaani.”

Alipoulizwa juu ya mkanganyiko wa kauli mbili za viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Kapteni mstaafu, John Chiligati na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda, Tambwe Hizza, zilizotofautiana, alisema kauli halali ya chama ni ile iliyotolewa na Chiligati.

“Kauli halali ni ile ya Chiligati… hizo nyingine unazoniuliza sizijui mimi, ninachojua kauli ya NEC ni ile ya Chiligati, kwa sababu tulikuwa wote Dodoma, hizo nyingine mimi sizijui,” alisema Makamba kwa mkato.

Makamba ambaye jana hakuwa tayari kutoa maelezo marefu kwa maswali aliyokuwa akiulizwa na waandishi wa habari, alisema kumekuwepo na wanasiasa wengi ndani ya chama hicho wanaojitokeza na kutoa maoni mbalimbali ya kupinga maamuzi ya chama.

Wakati Makamba akitamba kuwa chama hicho kina haki ya kumhoji Sitta kama kilivyofanya katika vikao vyake vilivyopita, juzi Tambwe alitoa tamko kwa vyombo vya habari linaloonyesha dhahiri kupindisha tafsiri ya maamuzi ya vikao hivyo, baada ya maamuzi hayo kuonekana kupata upinzani mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali nchini.

Katika tamko hilo, Tambwe alisema vikao hivyo havikujadili ajenda yoyote iliyowahusu Sitta na wabunge wenzake, wala iliyomhusu Makamba, aliyedaiwa kuwa ilikuwa nusura ang’olewe.

‘‘Katika NEC hakukuwa na ajenda yoyote iliyomjadili Sitta na wala hayo yaliyoandikwa eti wajumbe walitaka Sitta anyang’anywe kadi ya CCM hayakutokea. Na hakukuwa na ajenda yoyote katika Kamati Kuu wala NEC iliyomjadilli Makamba. Kwanza wakati wao wanasema hivyo, ndiyo kwanza vikao vilimpongeza Makamba kwa kufanya kazi zake vizuri,” alisema Tambwe.

Akizungumza na wananchi wa Manzese katika mkutano huo, Makamba aliwataka viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mkoa kuwasimamisha wagombea wanaopendwa na wapiga kura na kuacha upendeleo wa kindugu na kupokea rushwa.

“Ninawataka mhakikishe viongozi wanaopewa nafasi ya kugombea ni wale wenye sifa, na ambao wanapendwa na wananchi, nyie viongozi muache kula rushwa, upendeleo wa kindugu katika uchaguzi acheni.

“Kama wewe humpendi mtu, lakini chama kinamtaka mpe nafasi asimame na agombee, usitunyime ushindi CCM. Tumekuwa tukishindwa sana katika chaguzi nyingi kutokana na kuwasimamisha wagombea wasio na sifa.

“Huyo mtu unayemuona wewe kuwa anakufaa wewe, kwetu CCM hatufai, huyo unayemuona kuwa hakufai wewe, kwetu anatufaa, tupatie huyo mwambie humpendi, lakini unamtoa kwa ajili ya chama,” alisema.

Alisema ubaguzi ndani ya chama hicho umekuwa chanzo cha kushindwa kila chaguzi, na kama utaachwa katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi wa serikali za mitaa, kitaweza kushinda mitaa mingi.

Makamba aliyekuwa amefuatana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa, Sofia Simba, jana alikibomoa Chama cha Wananchi (CUF), ngazi ya taifa, baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Taifa - CUF, Ashura Amanji, kukihama chama hicho na kukabidhiwa kadi ya CCM.

Ashura ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wanawake wa CUF Taifa, alisema amekuwa kiongozi mkubwa ndani ya chama hicho, lakini amegundua kuwa anateseka bure kutumikia chama ambacho hakina demokrasia.

“Viongozi wetu wa makao makuu wamekuwa wabaguzi, nimekitumikia chama sana katika ngazi za juu, lakini sijaona mafanikio kutokana na ubaguzi na baadhi ya wakubwa wa chama. Mkubwa mmoja akikutaka ndipo utapewa cheo la sivyo hupati,” alisema Ashura na kusababisha watu kucheka.

Wengine ni Fatuma Aly Sadiq, ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu Taifa (wanawake), Sara Babavua, Mjumbe wa Baraza la Uongozi wa Taifa Wanawake, na Zainab Yusuf, Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Mkoa wa Kigoma.

Mbali na viongozi hao wa kitaifa, pia chama hicho pamoja na Chama cha Tanzania Labor (TLP) vilipata pigo, kwani wanachama wake zaidi ya 220, walirudisha kadi na kukabidhiwa za CCM.

Wakati huo huo, Kituo cha Msaada wa Kisheria nchini (LHRC), jana kilitoa tamko la kulaani hatua ya NEC na Kamati Kuu – CC kutaka kumwengua uanachama wa CCM, na kumvua madaraka ya uspika, Spika Sitta.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, kituo hicho kimeona kuwa hayo ni matokeo ya mfumo mbaya wa utawala ambao nchi imeridhia kutoka kwa Wakoloni.

“Haya ni matokeo ya mfumo mbaya tuliorithi kutoka kwa Wakoloni, ambao tunauendeleza ambapo kiranja wa shughuli za Bunge anatoka katika chama fulani cha siasa.

“Kinachotokea kwa Spika Sitta, ni kwamba anasongwa na chama chake kutokana na malalamiko ya kutokilinda chama chake bungeni, hasa wakati huu ambao nchi inakumbwa na matukio mengi ya ufisadi,” ilisema taarifa hiyo.

Wakati kituo hicho kikitoa tamko hilo la kumtetea Sitta, leo Spika huyo anatarajiwa kupata mapokezi makubwa atakapowasili mkoani Tabora.

Habari ambazo zimepatikana na kuthibitishwa na viongozi mbalimbali wa CCM mkoani humo, zinasema kuwa Sitta atawasili kwa ndege ya kukodi, ambayo pia itakuwa na viongozi na waandaaji wa tamasha la nyimbo za injili litakalofanyika kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Mara baada ya kuwasili mjini Tabora, Spika ataelekea moja kwa moja wilayani Urambo lilipo jimbo lake la uchaguzi, ambako ameandaliwa mapokezi makubwa yatakayopambwa na pikipiki na teksi na baadaye kufanya mkutano wa hadhara.

Hata hivyo, viongozi wa kisiasa wilayani humo walipohojiwa kwa njia ya simu kuhusu mapokezi ya kiongozi huyo, hawakuwa tayari kuelezea ratiba ya mapokezi na maandalizi ya ugeni huo, kwa madai kuwa wao wamesikia juu ya ujio huo kupitia vyombo vya habari.

Haya, maneno ya Katibu wako Mkuu hayo hapo, amempinga Tambwe na kuungana na Chiligati. Sasa wewe bado upo na Tambwe ambaye hata hicho kikao hakuwa mjumbe. masiki Pundamilia07, hiyo ndo CCM yenu, kama hukubaliani na kilichotokea, usijifariji kuwa hakikutokea, pole sana.
 
Duuuh ! Mkuu Balantanda hiyo font color haiko user-friendly, naomba uibadilishe tuweze kuona maandishi.
 
Duuuh ! Mkuu Balantanda hiyo font color haiko user-friendly, naomba uibadilishe tuweze kuona maandishi.
Nimebadilisha mkuu,niliicopy kama ilivyo toka website ya CCM(Wazee wa kijani na njano),hope yaonekana fresh now.......
 
Wale ambao wanaona kuwa mgombea aliepo sasa bado hawajaridhika na matokeo yale wakae kimya wasubiri 2015 umshauri baba au mama yako au mjomba au shangazi yako au rafiki yako agombee tena..
Hangover hizi! Tatizo umeamka mapema !!
 
Kumbe wanajua kuupdate website zao za serikali mbona wanaziacha muda mrefu bila kuwa updated?
 
Ili kuepukana na haya ni lazima katiba ya tanzania ibadilike na kumfanya Mbunge / spika kuwa mtu huru kwa kumtumikia mpiga kura wake na sio chama chake cha siasa.

Hicho ni kizungumkuti cha katiba. Kwani Spika/ wabunge wanawajibika kwa chama chao na sio wananchi waliowachagua.
 
Tuanaambiwa staili anayotumia spika sitta kujadili hoja kali bungeni ndo iliyotumika kumsulubu kwenye kikao cha NEC huko DODOMA kupanga wachangiaji, je mbali na GUNINITA na KINGUNGE ni wajumbe gani wengine waliomtemea mkwara spika wetu mpendwa? Nasikia walikuwa zaidi ya 40 waliosimama.
 
Back
Top Bottom