Mkandara said:
Jokakuu,
Mkuu hata wewe ungetegemea kupata kinga ya rais ikiwa umeifanya kazi ulopewa ipaswavyo..
Tunachokosea sisi Watanzania tunafikiria kwamba kiongozi bora ni yule Mbunifu wa idea na kisha mtendaji mkuu yaani Mwakyembe ndiye angeanzisha vagi la Ufisadi na kulifikisha hapo lilipo.. Hapana mkuu wangu kapewa kazi na kaifanya kwa uadilifu kama ilivyotakiwa, sasa inapofikia kushutumiwa na wabunge wakati JK mwenyewe alimpongeza wakati mapazia ya Ikulu yamefunikwa, ulitemegea Mwakyembe aseme kitu gani!.
Kwanza hakuna mtu mwenye guts za kusimama pale akamwambia JK kama alivyosema Mwakyembe... Sii Spika wala Malecela wote walikuwa wakitazama sinema na popcorn zao pembeni..
Now, alichotaka kuzawadiwa Mwakyembe ni JK kuonyesha kuridhika na kazi aloifanya Mwakyembe hadharan, na hakuna sehemu ya muhimu kama pale ..yeye ndiye alowatuma kusafisha vagi la Richmond na kazi ilikamilika..ila asichokifahamu Mwakyembe ni kwamba yeye ni Chale wa rais, kama wale machale wa sinema za Kichina.
JK hajawahi kusema in Public kusifia tume zake au mtu yeyote katika maswala yote ya Ufisadi, lakini kisha defend baadhi ya watu in public pamoja na kwamba anajua kuwa Ufisadi upo na majina yao yote yako mezani kwake Ikulu.
Mkandara,
..kwa jinsi nilivyoiangalia hii picha nadhani JK yuko upande tofauti na Mwakyembe.
..tatizo letu wengi tunatafuta kila njia ya kujiaminisha kwamba JK yuko upande wa kina Mwakyembe, Mengi, na Kilango.
..kama JK angekuwa anapinga ufisadi, basi angewasafisha mara moja, kwasababu Raisi wa Tanzania ana madaraka makubwa sana.
..kama JK alimpongeza Mwakyembe kwa kazi nzuri wakati wa faragha ni nini kinachomshinda na kumpongeza na kumlinda ktk vikao rasmi kama NEC.
..serikali ya JK imeshindwa hata kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Mwakyembe. kwangu mimi hicho ni kithibitisho kwamba JK hakubaliani na kazi iliyofanywa na Mwakyembe na wenzake.
..tatizo langu na Mwakyembe ni kuendelea kwake kumbembeleza na kujikomba kwa JK wakati anaona kabisa kwamba JK alimtapeli kama ni kweli kama unavyodai kwamba alimpongeza kwa kazi nzuri.
..alichopaswa kufanya Mwakyembe kama kweli yeye ni mpiganaji ni kuita a spade a spade. he needs to come out and tackle JK head on kwamba yeye[JK] sasa ndiyo kikwazo cha kuwashughulikia mafisadi.
..sasa hapo ndipo unapoona kwamba hata hawa tunaoita Mashujaa ni wabangaizaji tu. walitaka malipo fulani, ambayo mimi nadhani ilikuwa ni kukaribishwa ktk mlo wa mafisadi.
..as long as hakuna anayemtishia JK kuchukua hatua, basi hii inayoitwa vita ya mafisadi ni makelele matupu.
..JK hawezi kuchukua hatua wakati Mengi,Kilango,Malecela,Mwakyembe siku zote wakifungua midomo yao wanaimba sifa za jinsi JK alivyo Jemedari Mkuu wa vita dhidi ya mafisadi. hatua gani anazochukua wakati amekataa kutekeleza mapendekezo ya tume ya Mwakyembe? hivi hamuoni kwamba ni USANII tu unaendelea hapa?