- Wakuu tuende mbele na nyuma, hebu tuangalie kwa mapana na marefu kilichotokea kwenye hii NEC na implications zake kwa taifa, na hasa wananchi walalahoi, kwenu wapiganaji na sisi wananchi tunaowaunga mkono kwa 100% hebu tuangalie tena tathmini ya hii NEC, ukweli ni kwamba hawa mafisadi this time wametupiga vibaya sana,
- Wamemtisha Spika wa bunge la Jamhuri, anayeshika nafasi ya tatu katika mstari wa katiba yetu kwenye kushika madaraka ya urais, iwapo Rais na Makamu hawatakuwepo, hawa mafisadi wameweza kumtisha na kumbana koo, huku rais wa jamhuri amekaa pale akicheka as if it is funny, wakuu this is serious!
- Ninasema JF hatujashindwa hivi vita, tutaendelea kumkoma nyani mpaka kieleweke, lakini huko kwenye taifa tumepigwa jamani huu ni ukweli usiopingika, kama wameweza kumbana koo Spika wa Jamhuri, nani atakayewashinda tena under Spika? Nasema nani? Halafu ukweli ni kwamba hatujawahi kuwashinda hawa mafisadi kwa 100%, siku zote they play us arround, tulipowakaba koo kwenye Mwenyekiti wa UV-CCM, still wakatuzunguka na kumpitisha Makamu Mwenyekiti, Tulipotaka kuwanasa kwenye NEC ya Richimonduli na Kiwira, bado wakatuzunguka na maneno ya Lowassa kuonewa, na Mkapa aachwe apumzike!
- Wakati umefika sasa wa kumgeuzia kibao Rais Kikwete, yes I said it Mheshimiwa Rais somebody is not telling the truth hapa na hii vita, either wewe, wapiganaji, au sisi wananchi, lakini haiwezekani tukawa tunazunguka hapo hapo kila siku as if hatuna akili ya kutosha, wote tunajua kwamba Lowassa na genge lake ni wezi ndio maana mpaka wakakimbia uongozi wa juu bila kufukuzwa, sasa inakuwaje tena hao hao ndio wanakuwa na nguvu ya kutaka kuwaondoa kina Spika ambao hatuna proof yoyote kama ni wezi kama kina Lowassa, ambao proof zipo?
- Mheshimiwa Rais get real, acha hii two faces game unalimaliza taifa hili leo na la kesho, I mean this is not real kwamba eti Lowassa na kina Rostam, sasa wanajaribu kumuondoa Spika na wapiganaji na wewe upo pale mbele unacheka kama vile ni mazuri sana ni dalili za mufilisi wa maadili ya uongozi, hili sasa ni taifa la Sodoma na Gomora, yaani sasa wezi wanaweza kuwaonea wasio wezi linakua taifa gani hili sasa? Yaani watuwazima na akili zenu mmekubali kufikia mahali pa kumruhusu huyu Rostam kutuchezea akili taifa zima? Yaani Rais mzima umesimama ndani ya NEC, unasema hujali hela za kukisaidia chama zinatoka wapi au kwa nanil, au wanaotupa wamezipataje that is a joke! yes a big joke!
- Ingekua ni katika nchi zilizoendelea hapa palitakiwa Spika kufikishwa kwenye sheria, kisa CCM wanadai anakiuka sheria za bunge, ingechukuliwa maneno yote ya kina Kusila kama ushahidi, halafu wote huko NEC mngeitwa kwenye sheria kutoa ushahidi, na ku-face cross examination ya advocates, ndio jasho lingewatioka wote hao wapuuzi wa huko NEC!
Wallahi sasa ninafikiria kurudisha kadi yenu CCM, maana haiwezi ku-get worse than this kikao!
Respect.
Field Marshall Es!