Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Lunyungu,

Wewe ni msanii kweli kweli, inabidi ujiunge na The Comedy. Unatunga mambo kuja kuwafurahisha JF?
Na JF ilivyo na wajinga wengi, eti wanapiga makofi.

Huyo jamaa yako hakusema chochote kwenye NEC na alipotaka kusimama alizimwa na akanyong'onyea.

Kwa taarifa yako aliaga hapa Kyela kwamba yeye ni mtu muhimu mno kwenye vikao vya NEC na kwamba afadhali wakosekana akina Prof. Mwandosya na Prof. Mwakyusa kuliko kukosekana yeye.

Pia aliahidi kurudi Kyela Jumatano kuendelea na ziara yake ya kuzima moto wa Mwakalinga. Lakini baada ya kujeruhiwa Dodoma kaingia mitini.

Wapambe wanasema jemadari kajeruhiwa, yuko msituni kutafuta mbinu nyingine.

Kyela hapa ndio mazungumzo pekee; kwamba hawa jamaa kumbe hawajali maslahi yetu maana kama wangelikuwa wanajali maslahi ya wananchi si wangelisema chukueni kadi zenu?

We engineer wewe,

umesahau kale ka msemo ka kiswahili.... "UKISUSA WENZIO TWALA"??

Lakini pia kujali maslahi ya wananchi sio lazima kuwatupia kadi zao, kwani wao tu ndo wenye chama? Suala hapa ni kwamba kwa imani hiyohiyo waliyonayo na chama chao cha kifisadi pamoja na wapambe wao, inabidi waendelee kukabiliana nao humo humo ndani ya ku-CCM.

Huo ushauri wa kuwataka warudishe kadi za CCM, inabidi uanze na Mwakalinga, mshauri arudishe kadi ya kifisadi ajiunge na chama kilicho makini na kinachojali maslahi ya wananchi. Sio mnajifanya kuwashauri wenzenu warudishe kadi ili mpate unafuu na ushindi kiulaini. Jipangeni kisawasawa, mjengoni hamuingii kirahisi ati.
 
Last edited:
hii vita ni ngumu na inahitaji uvumilivu ili kuishinda, kama ni kweli mzee shibuda na wenzie wakawa na misimamo yao isiyo yumba itasaidia kukivunja chama chao na hapo ndipo tutakapopata uhuru wa kweli

Hapa ndipo panaleta shida.
Je, wale wapiga kura kwenye majibo ya hawa miamba,wanayajua haya ama habari zinafika (cinema imeisha)zimechelewa?

Na pia kuna hili la kuwachagulia mtu wa kuwa mbunge isije ikawakwamisha wasirudi tena 2010,.....
 
Hapa ndipo patamu hawa wabunge akina shibuda ndio wanatakiwa kukaza uzi wachonge sana tena sana yani ikiwezekana wawe kama Slaa.Mpaka ccm watakapowatimuwa.Siku wakiwatimuwa hao 11 hapo ndipo uhuru rasmi utapatikana
 
Engineer umesema jambo lakini hukunitendea haki Huwezi kunilinganisha na ze commedy na hakika sijawahi kuwa mpenzi wa Mwakyembe na sitakuwa. Nasema yaliyo jiri. Huwa habari za kumfurahisha mtu soma post zangu zote tangia nimeanza hapa.
 
Hapa ndipo patamu hawa wabunge akina shibuda ndio wanatakiwa kukaza uzi wachonge sana tena sana yani ikiwezekana wawe kama Slaa.Mpaka ccm watakapowatimuwa.Siku wakiwatimuwa hao 11 hapo ndipo uhuru rasmi utapatikana

Hilo nalo neno!
Bravo Mkamap
 
Kwa hali inayoripotiwa hapa jamvini kuhusu yaliyojiri kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM,inaonyesha kuwa bado tuna safari ndefu ya kuwaelimisha watanzania ili waweze kutumia kura zao vizuri.Ni elimu na ufahamu wa mambo halisi yanayoitokea sasa hivi ndivyo vitakavyomkomboa mtanzania aliyeko vijijini.

Kwa mtazamo wa haraka haraka mafisadi wamejipanga vizuri na ianonekana wanauwakilishi wa kutosha ndani ya NEC.Kwa msingi huu inawezekana wapiganaji wengi tunaowaona sasa wasipatiwe nafasi za kugombea tena katika uchaguzi ujao kwa kupitia CCM.

Ushauri wangu kwao wawe na plan B endapo wataona wanawekewa mizengwe ndani ya CCM.
 
Kwani Huyo mwenyekiti angefanya nini?......alishawahi kufanya nini?..........historia inaonyesha hajawahi, wala hawezi kufanya kitu chochote.

Yale ya tarime, yale ya pemba, yale ya EPA, yale ya BOT, yale ya Meremeta........amefanya nini? na kwa nini amenye chochote sasa??
 
hii vita ni ngumu na inahitaji uvumilivu ili kuishinda, kama ni kweli mzee shibuda na wenzie wakawa na misimamo yao isiyo yumba itasaidia kukivunja chama chao na hapo ndipo tutakapopata uhuru wa kweli

Naombea hayo hayo.
Hali tuliyo nayo inatisha. Imekuwa kwamba ni lazima EL arudi kuwa Waziri na kwa spid hii ni lazima aingie ikulu.

Maombi yangu kila siku ni kumpata 'Mwanawasa' wetu toka ndani ya CCM.
 
bul2.gif
Amweka kwenye kipindi cha majaribio
bul2.gif
Mengi naye aguswa ndani ya NEC
bul2.gif
Ya Mkapa yawatisha wajumbe


MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amemtega Spika Samuel Sitta ambaye ana muda hadi Novemba mwaka huu kujirekebisha, Raia Mwema imeambiwa.

Mtego huo ambao kwa upande mmoja unapalilia zaidi mpasuko wa ndani baina ya kundi la Sitta na jingine ambalo yeye amekuwa akidai linamtafuta, ulihitimishwa juzi pale Sitta alipotakiwa kujitetea ili asinyang’anywe kadi ya uanachama hatua ambayo dhahiri ingeshusha kila aina ya ndoto aliyonayo.

Baadhi ya wana CCM waliozungumza na Raia Mwema wakirejea Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho ulioanza mwishoni mwa wiki iliyopita wanasema mbali na kumpatiliza Sitta, Kikwete pia aliruhusu kutikiswa kwa mtu wa karibu na Sitta, mfanyabiashara maarufu, Reginald Mengi, ambaye kama Sitta, amekuwa akisema kwamba yumo katika vita dhidi ya ufisadi ili kumsaidia Rais Kikwete anayeiongoza.

Habari za ndani ya CCM kutoka katika vikao rasmi na visivyo rasmi, zinaeleza kwamba Rais Kikwete ameamua, kutumia mtindo wa “kuuma na kupuliza” kwa marafiki zake, Sitta na Mengi kwa kuruhusu mjadala kwenda katika mpangilio ulioandaliwa mahususi kwa ajili ya ‘kuwashughulikia’ Sitta na Mengi, na kwa maana hiyo kundi la wabunge ambalo limekuwa likijitambulisha na Sitta.

Taarifa za ndani zinasema, katika kikao hicho, mbali ya Sitta kujadiliwa, mmoja wa wabunge alibanwa kwa kumshirikisha Mengi katika shughuli za CCM ikidaiwa kwamba mfanyabisahara huyo si mwana CCM.

Hata hivyo, habari zinasema kwamba pamoja na Mengi kuwa mwana CCM na mtu anayekisaidia chama hicho kwa muda mrefu, mfanyabiashara huyo amekuwa karibu na Rais Kikwete na amekuwa akimtaja na kumsifia Rais hadharani.

“Karibu wajumbe 40 walizungumza dhidi ya Sitta. Walikuwa wakitoa wito afukuzwe kwa jinsi anavyoliendesha Bunge ambalo katika siku za karibuni limekuwa likiibana sana Serikali.

“Aliomba sana msamaha, lakini dhahiri hakuna hata mmoja aliyekuwa akimsikiliza, hata wachache waliojaribu kumuunga mkono walizomewa wasiweze kuendelea kusema lolote.

“Kwa hiyo kwa sasa ni kama Sitta yupo katika kipindi cha majaribio. Hatima yake itategemeana na jinsi anavyoliendesha Bunge kati ya sasa na Novemba. Hiyo kamati iliyoundwa imepewa mwanya wa kuitisha kikao cha dharura kama itaona kuwa anakwenda ndivyo sivyo,” anasema mmoja wa wajumbe wa NEC aliyezungumza na Raia Mwema kwa masharti ya kuwa hatajwi kama chanzo cha habari hii.

Mjumbe mwingine aliiambia Raia Mwema kwamba pengine msumari wa mwisho katika jeneza la Sitta utakuwa umepigiliwa na mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru ambaye alimsema Sitta kwamba japo amekuwa akidai kwamba anaendesha Bunge kwa mtindo wa Uingereza (Jumuiya ya Madola), uendeshaji wake haukuwa sawa na huo wa Uingereza.

“Kwanza Ngombale alichanachana Waraka wa Wakatoliki akidai ni ilani ya kisiasa na kwamba haiwezekani nchi ikawa na ilani zaidi ya moja kwa wakati mmoja, kisha akamrukia Sitta.

Yalizungumzwa mengi, pamoja na kumtetea Mkapa (Benjamin) na wapo walioonya kwamba kwa kuruhusu Mkapa kukwaruzwa, Kikwete alikuwa anaandaa kaburi lake mwenyewe,” anasema mjumbe huyo.

Lakini mjumbe mwingine, mfuasi wa kundi moja kati ya makubwa yanayopingana kwa sasa ndani ya CCM ameiambia Raia Mwema hata hivyo kwamba msimamo wa Kikwete katika suala la Sitta unaweza usiwe na maslahi makubwa kwa chama siku za usoni.

“Kikwete anaonekana hataki kuwaudhi marafiki zake wote wakiwamo hata wale ambao alionekana kuwatosa kutokana na kuhusishwa kwao na kashfa mbalimbali ambazo Sitta na kundi lake wamekuwa wakizisemea. Nadhani alipaswa kuwa na msimamo wa wazi katika hili maana linahusu mustakabali wake kisiasa na wa chama chetu.

“Sasa wananchi wana uelewa kuliko wakati mwingine wowote na kwamba mwaka mmoja si mbali kuelekea kwenye uchaguzi mwingine na hii ni hatari sana kama hakutatokea jambo lolote zito,” alisema mwanasiasa huyo katika mazungumzo ya simu kutoka Dodoma alikokuwa akihudhuria vikao hivyo.

Katika vikao vyake vya juu mjini Dodoma vilivyomalizika juzi, CCM imeunda timu ya viongozi wake ndani ya Kamati Kuu yake kuchunguza mwenendo wa uhusiano kati ya chama hicho, Serikali na Bunge, mambo ambayo ndiyo msingi wa tuhuma dhidi ya Spika Sitta na watu walio karibu naye.

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Spika za zamani ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na waziri wa zamani, Abdulrahman Kinana ndio wanaounda timu ya kufuatilia mwenendo wa Sitta.

Mkakati uliotumika katika kumjadili Sitta unashabihiana kwa staili na ambayo amekuwa akiitumia Spika huyo kujadili mambo nyeti ndani ya Bunge kwa kuwapanga wabunge anaowaamini, kuzungumza. Haikuweza kufahamika mara moja orodha hiyo ya wazungumzaji iliandaliwa na nani.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baadaye Sitta alipewa “ushauri wa busara” ili aombe radhi wajumbe hao, ikielezwa kuwa ni hatua ambayo ilikuwa ikiungwa mkono na Rais Kikwete. Kikwete anadaiwa kuunga mkono Sitta kuomba radhi kwa vile hakuwa “tayari kupoteza Spika katika kipindi hiki, na wala CCM haiwezi kupoteza mbunge wakati huu”.

Taarifa zaidi zinasema huu si mwisho wa suala la Sitta na chochote kinaweza kutokea siku za baadaye, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa Rais Jakaya Kikwete amekuwa na kikosi kazi cha siri kinachochunguza mwenendo wa kundi hilo.

Inadaiwa kuwa moja ya kazi zilizokwishafanywa na kikosi kazi hicho ni pamoja na kupima upepo wa kisiasa katika Jimbo la Urambo Mashariki, linaloongozwa na Sitta. Kikosi kazi hicho kilipewa jukumu la kukusanya taarifa huru kuhusu Sitta na wale wanaodaiwa kumwandamana kwa mbinu chafu, na kati ya mambo yanayodaiwa yamepatikana ni kutumiwa kwa mmoja wa mawaziri kufanikisha mbinu hizo zinazodaiwa ni chafu.

Sitta ambaye amekuwa akijigamba kwa wanasiasa wenzake akiwataka wawe na ngozi ngumu ya kuhimili mikikiki ya siasa, mikakati iliyosukwa safari hii ndani ya NEC imedhihirika kumtoa jasho na hata kumweka katika mtazamo mpya kuwa anayo kazi kubwa ya kufanya dhidi ya mikakati mingine ijayo.

“Kwa kweli tukubali kuwa hali si nzuri katika chama chetu, si nzuri kwa sababu zimejitokeza hoja za kupingana…hapana hata kidogo, ni kwamba si nzuri kwa sababu nguvu ya fedha imeteka busara za baadhi ya wajumbe wa vikao muhimu kama NEC. Na kama Watanzania wataamua vinginevyo basi vikao hivi vya NEC na hata CC vitazidi kupoteza maana.

“Itakapofikia hivyo, itakuwa hatari zaidi kwa CCM kwani vikao kama hivyo ndivyo vinavyopitisha majina ya wagombea nafasi za ubunge, na urais. Watu wakipoteza imani na wajumbe wa NEC, inayopitisha mgombea urais maana yake chama ndiyo kinang’oka madarakani,” alisema mjumbe mmoja wa CCM, ambaye hakutaka kutajwa jina kuelezea kwa ujumla mazingira ya NEC ya wiki iliyopita.

Kabla ya kuanza kwa vikao vya CC na NEC, ambayo safari hii Rais mstaafu Benjamin Mkapa alihudhuria, miongoni mwa wanachama wa CCM walioonyesha mtazamo wao wa kutaka Sitta ang’oke ni pamoja na Mbunge wa Ukonga, Dk. Makongoro Mahanga, ambaye si tu alimlenga Sitta, bali pamoja na wabunge wengine wanaodaiwa kupiga vita ufisadi.

Siku chache baada ya Bunge kumalizika, viongozi wa wakuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mwenyekiti Hamadi Yusuf Masauni na Katibu Mkuu, Martin Shigela, walikutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuwaeleza mambo mbalimbali likiwamo suala la kuwapo baadhi ya viongozi kujipatia umaarufu kwa kudai kupinga ufisadi na kusisitiza kuwa kinara wa vita dhidi ya ufisadi ni Rais Jakaya Kikwete.

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa mjini Dodoma wanaamini kuwa tishio la sasa dhidi ya Sitta linalenga kuzima makali ya Bunge katika mkutano wake ujao, ambako Serikali itapaswa kutoa taarifa kadhaa ikiwamo ya kuhitimisha sakata la Richmond.

Katika mkutano uliopita wa Bunge, taarifa ya Richmond ilikataliwa na Bunge kwa madai kuwa ililenga kuwasafisha watuhumiwa badala ya kutekeleza maazimo ya mhimili huo wa taifa.
 
2010 around the corner!! Tutasoma wee mpaka tuvae miwani ya mbao ili tuone na kusoma vizuri!!! Hapo bado magazeti mapya hayajajisajili na mara baada ya uchaguzi kapuni!!! Tutafika???
 
Hivi zama hizi ni za kuwa na viongozi kama hawa akina kusila? mambo ya kufurahisha vikao eti kujifanya unajua kuongea kwa hoja zisikuwa na maana sijui kama tutajikomboa kweli, jamani Rais Obama alipokuwa Ghana aliwaambia Africa sasa haihitaji "strong leaders", inahitaji "strong institutions". hivi zama za akina kusila zimekwisha, unadhani ukimponda mwenzio mbele rais utaonekana wewe ndio unafaa?kwa fikra na nidhamu yako ya woga? watu kama hawa ni wakupiga chini, hawatufai, na bahati mbaya sana tunao wengi sana na CCM ndiyo wamejaa, haya ndiyo wakati wa Nyerere yalikuwa hayaongei kwa sababu yaliogopa kuitwa mapumbavu, sasa hivi kwa sababu umri na njaa zimezidi basi yanturudisha enzi za nidhamu ya woga.
 
Tunataka watu kama hawa, unatoa hoja siyo kama akina kusila wanamfurahisha rais!!!Shibuda is good.Tunataka watu wanojua tunakotaka kwenda kama shibuda, uko juu kaka endelea kufumbua macho ya viongozi wenzio waliolala!!
 
ndo maana huwa nakataa kuingia ktk siasa maana magugu ni mengi kiasi kwamba yanafunika mwangaza wa jua unaoleta virutubisho vya ukuaji.

CCM imejaa wahuni tena wahuni waliokulia ndani ya chama. hawa wanaosema kwamba wanaotetea maslahi ya taifa ni wasaliti nawaambia kwamba wao ndo wahaini wakubwa. Watanzania eleweni kwamba hawa jamaa ambao tunaona wamesoma hamna lolote zaidi ya kumiliki vyeti kwani mpaka sasa zaidi ya kusaini mikataba ambayo hata Mangungo angeistukia hamna lolote waliloifanyia nchi zaidi ya kuchota na kufisadika bila aibu.

shenzi zao kabisa (samahani nina hasira sana)

Ila namshauri Muungwana awe mwangalifu anapowabeba hawa watwana wake kwani ndio wataomkimbia na kumuwamba mambo yakimharibikia. ajue anazo kura zetu na si za hao wachache. Kama sisi wananchi tunamuunga mkono ajue hakuna wa kumtisha wala kumkwamisha. kundi lililomzunguka ni wachache tena hawamwambii ukweli halisi zaidi ya kudanganyana tu!!! kudadadeki
 
Kwa kweli kilichojitokeza kutoka kwenye hicho kikao kama yaliyosemwa ni ukweli, basi we are in a stinking shit! Ninachoweza kutamka ni we are in mafioso hands! Ni vipi haya yanaweza kutendeka kwenye nchi inayojiita ya kidemokrasia na yakapewa thumbs up na the top brass?
Kama yamekuwa hayo,na kama tuko serious, tunatakiwa tuchukue hatua ya haraka. Namna pekee ya kuangamiza hawa mafisadi ni kupitia kura zetu 2010! Ikumbukwe hawa walipiga kelele sana ulipoleak ule waraka wa kanisa katoliki juu ya kuhamasisha wananchi kuchagua viongozi waadilifu. Ukweli njia pekee kwa sasa hivi ni kuunga mkono huo waraka wa kanisa na tufanye bidii ya kuelimisha wananchi wenzetu umuhimu wa kupiga kura kwa makini kuhakikisha tutakaowachagua ni waadilifu na wanaweka mbele masilahi ya wananchi. Kwa njia hii, tutawaondoa mafisadi wote kwenye uongozi wote kuanzia juu mpaka chini. Ni muhimu kutoa elimu kwa kuwa wananchi wengi wamekata tamaa na wameshaamua hawapigi kura tena wasijue kufanya hivyo ni kuwasafishia njia mafisadi wajichague wenyewe tukibaki kulia na kusaga meno!Tukifanikiwa
hili mafisadi watakwenda na maji and a what beautiful country Tanzania will be! ALMIGHTY LORD HELP US ON THIS.
 
Kauli za Shibuda zaniacha hoi sana....namjua huyu jamaa vizuri tu, wakati mwingine huwa yuko kama confuser fulani....angalizo tuwe makini na anachokisema wakati mwingine haimanishi hivyo!
 
Huyu Kusilwa ni waziri wa zamani katika serikali ya Mzee Ruksa. Ni rafiki sana wa Mzee Paschal Ndejembi aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kwa muda mrefu pale Dodoma. Ndejembi ni hasimu wa kiasa wa Mzee John Malecela. Wanaosemwa (kimafumbo) naye hapa ni Melecela na mke wake Anna Kilango!! Very weird guy
 
Ni dhahiri kuwa JK ameshazidiwa nguvu. kama anashindwa kutoa msimamo katika chama, basi hatuna kiongozi wa nchi
 
Date: 8/20/2009

Wabunge CCM kuendelea kupambana na ufisadi

Mahanga, bila ya kuwataja waliomuunga mkono Malecela, alisema wale wanaotoa tuhuma za ufisadi bila ya kuwataja majina watuhumiwa, au kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria au kuwashtaki ndani ya chama, wanafanya kazi ya upinzani ya kuichafua CCM na hivyo akawashauri wajitoe kwenye chama hicho tawala.

Hivi kweli ni mpaka utaje majina ndipo haki ya kusema kuwa kuna Mafisadi ndani ya chama inapotimia? Inatakiwa mtu anaesema kuna mafisadi ndie achukue hatua za kushitaki pekee, au kila mtu ana haki ya kufanya hivyo? Kuna njia nyingi za kupambana na ufisadi na uovu mwingine. Moja ya njia hizo ni kukemea kwa sauti kubwa. Ni haki ya kila mmoja kuamua atakomesha matendo maovu kwa njia gani. Haina mantiki yoyote kulazimishana kufungua mashitaka mahakamani kama mtu anaetakiwa kufanya hivyo haoni manufaa ya kufanya hivyo. Itabidi wanasiasa wazoee tu kuona watu wakitumia haki zao kujielezea.

Zimeundwa tume nyingi, kuna ripoti nyingi zinazoelezea matukio mbalimbali na kuyahusisha na ufisadi. Walau wangekemea tu ufisadi uliotajwa katika ripoti hizo (hata kama hawataki kutaja majina ya wahusika) badala ya kukemea wanaoziamini ripoti hizo na kuweka visa kwa wajumbe wa tume zilizoundwa na kugundua uozo huo.

Jana Dk Mahanga, ambaye ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, alisema suala hilo lilikuwa linamkera na kwamba uamuzi wa Nec wa kudhibiti wanaopinga ufisadi hadharani, ikiwa ni pamoja na kwenye vikao vya Bunge, umeunga mkono yale aliyoyaeleza.

Kukemea wanaopinga ufisadi nje na ndani ya Bunge hakuwezi kuiokoa CCM. Nadhani inatakiwa wanasiasa hawa wajue kuwa Panadol haitibu Malaria. Kama wanataka wananchi waendelee kuwaamini na kuwapa kura zao, ni vyema wakatafuta tiba halisi ya magonjwa yanayosumbua chama chao badala ya kupambana na daktari.

“Yaani kila mtu anafanya mambo yake mwenyewe, hali ambayo inaweza kusababisha watu kurushiana hata viatu ndani ya ukumbi wa bunge. Sasa hali hii maana yake nini? “Kwa hiyo tumesema inatosha, hapo tulipofikia tusiendelee mbele. Wanaoropoka hovyo ni walevi na tumeona kuna kundi dogo ambalo limejiona kama ni wateule wa kuzungumzia sakata hilo (la ufisadi) bila ya kujua wabunge wote wana haki ya kuzungumzia suala hilo, lakini kwa utaratibu tena kwa kupitia katika vikao vya kamati za wabunge.”

Nadhani kama waheshimiwa hawa wanaona Bunge linakwenda kinyume na matarajio yao, wangeweza kuelezea hivyo ndani ya Bunge (au kutuma wabunge wao kufanya hivyo) badala ya kujadili utendaji wa Bunge kwenye vikao vya chama pekee.

Sina uhakika kama ni sahihi kwa chama chochote kudhani kuwa kwa kuwa kinashika dola, basi kina mamlaka ya kuamua Bunge la Jamhuri liweje bila kufuata kanuni za Bunge. Ingefaa zaidi wakajadili na kutoa mapendekezo yao juu ya namna wanavyoona Bunge likiendeshwa, na baada ya hapo wakayatoa mapendekezo hayo ndani ya Bunge ili yajadiliwe na waBunge wote na hatimaye uamuzi wa mabadiliko ya kanuni na sheria za Bunge ufanyike ili Bunge liendeshwe kama wanavyotaka. Utaratibu huu wa kuamua Bunge liweje, kumshinikiza Spika kutii maazimio yao (nje ya Bunge), si tu hauna tija, bali pia si sahihi na unakiuka Katiba, kanuni za Bunge na unatoa picha mbaya kwa wananchi. Nadhani utaratibu wa hansard na mijadala migumu ndani ya Bunge ndivyo vinavyo watisha kufanya hivyo Bungeni. Waende wakajadili Bungeni kama kweli wanataka kubadilisha chochote kinachofanywa na Bunge.

Kwa mtazamo wangu NEC imefanya lobbying isiyofaa kabisa kisiasa.
 
Kiongozi wa nchi yupo,ni hatari sana kama nchi haina kiongozi!

Maana kama nchi haina kiongozi inabidi turudi tena kwa wananchi watupe ridhaa yao,ina maana bunge pamoja na baraza la mawazri livunjwe!nchi iwe kama jaji mkuu kama sijakosea.

Tuwe makini katika kutekeleza katiba na kanuni za nchi hata wakati wa kuchangia hoja iwe kimaandishi au kimaneno
 
Back
Top Bottom