Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

- More dataz ni kwamba baada ya kuwa cornered na mashambulizi ya non-stop na hasa kutoka kwa wa-Zanzibari ambayo tutayaweka hapa pindi tukishayapata tu, na huku akishinikizwa na Rais Mwinyi na Rais Kikwete, Mheshimiwa Spika alizungumza machache sana,

- Kwa kifupi Spika alisema kwamba:- ".....kwa mtumzima kama mimi kushambuliwa namna hii na watu wazima wengine, maana yake ni moja kwamba huenda kuna tatizo, na mimi kama mtumzima naomba tusameheane jamani...."

-Hapa ukumbi mzima ulinyamaza kimyaaa, huku washambuliaji wakionyesha kutoridhika na majibu ya Spika, lakini Mwenyekiti wa CCM ambaye sasa alikuwa serious tena, aliashiria kuridhika na maelezo ya Spika.

Respect.

Field Marshall Es!
 
- Hivi huyu Mahanga, kwa nini asijitoe kwenye hiki chama kinachofuga wasema hovyo na waropokaji, akajiunga na chama kisichokuwa nao, kama kweli anakereketwa sana na hawa wapiganaji au waropokaji?

- Hawa viongozi wetu wengine sijui walifikaje hata huko juu! Hivi huyu si Doctor naye kama Mzindakaya, na Nchimbi au?

Respect.

FMEs!
 
hapa ndipo ninapoithibitisha kauli yako fmes kwamba MUUNGWANA HAELEWEKI!yupo somewhere in between.
 
- Hivi huyu Mahanga, kwa nini asijitoe kwenye hiki chama kinachofuga wasema hovyo na waropokaji, akajiunga na chama kisichokuwa nao, kama kweli anakereketwa sana na hawa wapiganaji au waropokaji?

- Hawa viongozi wetu wengine sijui walifikaje hata huko juu! Hivi huyu si Doctor naye kama Mzindakaya, na Nchimbi au?

Respect.

FMEs!

Huyu ni Doctor kama Nchimbi, unafiki na kubebwa na mafisadi ndio vimemfikisha juu ili wamtumie kwenye uchafu wao
 
Mahanga anaumwa mafua ya nguruwe (H1N1) huyo. Aunganishwe na wale wanafunzi wa IST haraka sana. Vibaraka utawajua tuu. Hili si lile lilishinda ubunge Ukonga kwa kudura ya mwenyezi Mungu baada pia ya kupenyezewa msaada wa manoti na Mafisadi??? Lisubiri mwakani.

Kwa upande wa Mh. Shibuda, kweli huwa napenda majibu yake na msimamo kuhusu mafisadi. SSM walishamuona ni tatizo kuanzia awali, na mtakumbuka katika kura za maoni ya CCM alipata alama E. He is their threat!! Sasa kwa mwakani ni lazima wahakikishe kuwa harudi Bungeni. Kwa bahati mbaya jamaa hajajiimarisha sana kifedha sasa inabidi naye apate manoti ya t-shirt, ubwabwa, khanga, n.k maana ndivyo wapiga kura wengi waliozoea, tena wale ambao hawajui watakula nini kesho. Na ninashangaa maana wanawachagua hawa vilaza na bado hali ya maisha ni duni kama kawaida. Ni kwa nini sasa wasipokee hizo takrima halafu wafanya mapinduzi?? Tatizo wanatishiwa kuwa usipomchagua fulani alietoa ubwaba basi atakufahamu na watakuudhuru. Jamani elimu ya uchanguzi itafanyika lini??? Hizi NGO zetu za kisanii nao wanaogopa nyau hawathubutu kujiingiza katika elimu ya demokrasia. Je tutafika?
 
- Hivi huyu Mahanga, kwa nini asijitoe kwenye hiki chama kinachofuga wasema hovyo na waropokaji, akajiunga na chama kisichokuwa nao, kama kweli anakereketwa sana na hawa wapiganaji au waropokaji?

- Hawa viongozi wetu wengine sijui walifikaje hata huko juu! Hivi huyu si Doctor naye kama Mzindakaya, na Nchimbi au?

Respect.

FMEs!

Mkuu heshima mbele, kutokana na taratibu za kutoanza kampeni kwenye majimbo mpk muda muafaka uwadie, sasa hivi naona wabunge wengi hasa wa CCM ambao kwa kiasi kikubwa wailijisahau ndio wanatumia nafasi ya yaliyojiri NEC kuwa kama ndio kampeni na kuonekana mbele ya macho ya wapiga kura wao.

Mahanga ni mnafki fulani hivi na ameshasoma alama za nyakati jimboni kwake hali si nzuri ndio maana anajishebedua kwenye magazeti.

Kuhusu udaktari wake kwakweli............no comment labda mpk nitakapokuwa na uhakika na support ya Game Theory hahahha....
 
Huyu Shibuda ni mpambanaji wa kiukweli, ana kawaida ya kuita koleo kwa jina lake hapindishi ukweli hata kidogo huyu, yule fisadi Mgeja anautambua mziki wake vizuri.
 
nafikiri hakuna sifa maalumu za kumfanya mtu kuwa M-NEC zaidi ya kuwa mwanachama na kuchaguliwa kwa kura....naona kuna mchanganyiko wa followers wa makundi yaliyopo sisiemu i.e. khadija kopa(i guess yumo),mh Komba(alikuwemo tokea akiwa kiongozi wa TOT), Jongo n.k .....kwenye maamuzi mazito kunahitaji watu serious na wenye utashi wa kisiasa. sisiemu wanavitumia vibaya vikao hivi hasa kwa kuwapa airtime kubwa vibaraka waliotumwa kuvuruga nchi....inaumiza sana watu wote wanaoshabikia na wanaoendesha hujuma .

Hawa uliowataja Kopa na Jongo ni wajumbe wa Mkutano Mkuu ila Komba ni Almashauri kuu tena siku nyingi enzi za Mwl kabla hajafa kama sikosei.

Tunamshukuru FME kutuhabalisha ila naulizia kitu kimoja kwenye huu mkutano Mzee Malicela alihudhuria kweli? au siyo mjumbe
 
Nafikiri Mzee Jongo alifariki dunia miaka kadhaa imepita
 
Mkulu FMES
Kwa kusaidia tu ni kwamba baada ya hao alikuja Simba Mwakyembe.Mie simafagilii sana lakini hili nasimama naye .Alimwambia haya maneno direct ndugu Mwenyekiti wa CCM.

Mwenyekiti all these folks wanaongea nonsense we unaona ni jambo la maana una waachia wana endelea tu .Unakumbuka how we did help you kwa kuzima moto wa wananchi juu ya mawaziri wako kusakamwa na kuzmewa kila kona ya Nchi hadi kufanya hali iwe shwari , hata sasa ,Je haya ndiyo malipo ambayo umetuandalia kwa kashfa na kuombwa kuwa tried kama wahaini na kutakiwa kurudisha kadi eti twende Chadema?

JK hakujibu kitu hadi mida hii naandika haya .

Tuendelee kukanyaga mafuta twende .

Lunyungu,

Wewe ni msanii kweli kweli, inabidi ujiunge na The Comedy. Unatunga mambo kuja kuwafurahisha JF?
Na JF ilivyo na wajinga wengi, eti wanapiga makofi.

Huyo jamaa yako hakusema chochote kwenye NEC na alipotaka kusimama alizimwa na akanyong'onyea.

Kwa taarifa yako aliaga hapa Kyela kwamba yeye ni mtu muhimu mno kwenye vikao vya NEC na kwamba afadhali wakosekana akina Prof. Mwandosya na Prof. Mwakyusa kuliko kukosekana yeye.

Pia aliahidi kurudi Kyela Jumatano kuendelea na ziara yake ya kuzima moto wa Mwakalinga. Lakini baada ya kujeruhiwa Dodoma kaingia mitini.

Wapambe wanasema jemadari kajeruhiwa, yuko msituni kutafuta mbinu nyingine.

Kyela hapa ndio mazungumzo pekee; kwamba hawa jamaa kumbe hawajali maslahi yetu maana kama wangelikuwa wanajali maslahi ya wananchi si wangelisema chukueni kadi zenu?
 
Hawa uliowataja Kopa na Jongo ni wajumbe wa Mkutano Mkuu ila Komba ni Almashauri kuu tena siku nyingi enzi za Mwl kabla hajafa kama sikosei.

Tunamshukuru FME kutuhabalisha ila naulizia kitu kimoja kwenye huu mkutano Mzee Malicela alihudhuria kweli? au siyo mjumbe

Margreth,

Mzee Malecela aliona hatari akakimbia na mkewe kwenda kufaidi pesa za Watanzania London. Wewe unategemea Malecela aisaliti CCM?

Nimeambiwa wapiganaji walimtafuta sana mama Kilango lakini kwa makusudi mazima alizima simu mpaka baada ya kikao. Akina mwakyembe wanalalamika chini chini kwamba mama Kilango kawasaliti.
 
FMES,

Nimepitia hii tokea umeianzisha mpaka sasa hivi ni kweli nashukuru ila bado namkubali SAID KUBENEA kwenye gazeti lake la Mwanahalisi wiki hii kwani kila kitu kimeongelewa jinsi NEC ilivyokuwa inaendeshwa, tena vizuri bila kukata kata maneno, kwakweli ametoa makala kwa kutupa picha kamili tena jina kwa jina. Simshabikii, Kizuri Kinasifiwa.
 
Mahanga anaumwa mafua ya nguruwe (H1N1) huyo. Aunganishwe na wale wanafunzi wa IST haraka sana. Vibaraka utawajua tuu. Hili si lile lilishinda ubunge Ukonga kwa kudura ya mwenyezi Mungu baada pia ya kupenyezewa msaada wa manoti na Mafisadi??? Lisubiri mwakani.

Kwa upande wa Mh. Shibuda, kweli huwa napenda majibu yake na msimamo kuhusu mafisadi. SSM walishamuona ni tatizo kuanzia awali, na mtakumbuka katika kura za maoni ya CCM alipata alama E. He is their threat!! Sasa kwa mwakani ni lazima wahakikishe kuwa harudi Bungeni. Kwa bahati mbaya jamaa hajajiimarisha sana kifedha sasa inabidi naye apate manoti ya t-shirt, ubwabwa, khanga, n.k maana ndivyo wapiga kura wengi waliozoea, tena wale ambao hawajui watakula nini kesho. Na ninashangaa maana wanawachagua hawa vilaza na bado hali ya maisha ni duni kama kawaida. Ni kwa nini sasa wasipokee hizo takrima halafu wafanya mapinduzi?? Tatizo wanatishiwa kuwa usipomchagua fulani alietoa ubwaba basi atakufahamu na watakuudhuru. Jamani elimu ya uchanguzi itafanyika lini??? Hizi NGO zetu za kisanii nao wanaogopa nyau hawathubutu kujiingiza katika elimu ya demokrasia. Je tutafika?
shibuda ni mfanyakazi wa usalama siku nyingi tu
na wafanyakazi wa usalama siku zote wanarudi bungeni....
 
Mimi bado nasubiri Spika mwenyewe aseme angalau neno moja tu na roho yangu itapona. Siamini jinsi alivyo "MBABE" mjengoni afike CC na NEC ya CCM anywee kiasi hiki!
 
Jamani hata mimi naona ni afadhali CCM ikufukuze, kuliko wewe kuondoka. Kwa sasa hali iliyomo ndani, ni mbaya sana, kwa hiyo hata tupingwe namna gani, hatuondoki.
"Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa".

Wewe ulisema humpendi Sitta na yeye anapingana na Rushwa sasa mbona ni contradiction ?
 
Mimi bado nasubiri Spika mwenyewe aseme angalau neno moja tu na roho yangu itapona. Siamini jinsi alivyo "MBABE''; mjengoni afike CC na NEC ya CCM anywee kiasi hiki!

Tusitegemee kama Spika Sitta atajibu lolote kuhusiana na yaliyojiri kwenye vikao vya CC na NEC kwa sababu vikao hivyo ni vya siri, yote yanayozungumzwa ni kuvuja kwa siri, taarifa rasmi ni ile ya Chiligati, haukumtaja Sitta, hivyo Sitta kamwe hawezi kuibuka kucomment kuhusu taarifa za siri zilizovuja.Sitta kitu atakachokifanya kesho mjini Urambo, ni kuwahakikishia wana Urambo na mashabiki wake wasiwe na wasiwasi, waipuuze minong'ono kuhusu yeye inayosambazwa na mafisadi ili kumhujumu, na kutoa msisitizo kuwa yeye bado yuko imara.Kama ni kujibu mapigo, atayajibu kwenye kikao cha bunge cha November, tena atayajibu kwa vitendo by 'hitting them hard' right in their faces.
 
Hii nchi mpaka tupigane ndo tutaheshimiana, hawa wote wanatwanga maji kwenye kinu tu wataongea saaaana mwisho wa siku hakuna utelekezaji,toka wameanza kuongea we unaona nini kimebadilika?"The only thing neccessary for the trumph of evil is for good men to do nothing" EDMUND BURKE
 
Jamani hata mimi naona ni afadhali CCM ikufukuze, kuliko wewe kuondoka. Kwa sasa hali iliyomo ndani, ni mbaya sana, kwa hiyo hata tupingwe namna gani, hatuondoki.
"Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa".

Baija Bolobi nikuulize. Hivi nyie ambao mko NEC ya CCM mmechunguza kwa undani na kuona hizi nguvu kubwa zinazokiyumbisha chama chenu kupitia Ufisadi chanzo chake ni nini? Nina uhakika mtakuwa mnajua nani anafanya nini katika harakati hizi kama vile waliokuwa wanawagongea usiku lakini nguvu hii hasa inatoka wapi? Nina wasi wasi kwamba uenda tunawafikiria watu wachache waliooko kwenye siasa na tukasahau kwamba nyuma yao wako watu wenye nguvu ya kipesa ndio wanaowatuma hawa wanasiasa wachache wakivuruge chama alafu wa "take over" na kuweka vibaraka wao. Mkiwabaini hawa basi mtakuwa mmeshinda nusu vita.

Nina wasi wasi sasa kwamba mapambamo haya ni makubwa kuliko tunavyofikiri.You may think you are fighting a few corrupt individuals within CCM not knowing that this battle is "class' issue. Kule Gayana (South America) wahindi walichukua nchi kwa kupandikiza vibaraka katika chama tawala ( chama cha watu weusi) kwanza wakakidhoofisha na hatimaye kuchukua madaraka hadi leo! Nani hasa wanafaidika na ufisadi nchi hii kama sio tabaka moja la raia hapa nchini? Ukipiga vita ufisadi ujue unayagusa maslahi ya kundi hili lenye nguvu za kiuchumi. Nyie mlioko NEC msikubali kundi hili liteke chama chenu otherwise mtakuwa wasaliti wa nchi hii na watanzania watawaadhibu vilivyo.
 
Pasco,
Akichelewa hivi hadi Novemba kisiasa ina madhara yake. Yeye ni Spika popote alipo. Asitoe mianya ya aina hii. Kwanza ameshindwa kuwa "hit hard" mle kwenye vikao halafu atoe muda wote huu waendelee kujiona washindi!
 
Kinachonishangaza mimi ni kwamba ukisema CCM ni Chama Cha Mafisadi akina Makamba na Mahanga wanakwambia mafisadi ni watu wachache sio CCM. Ukiwasema mafisadi hadharani unaambiwa fuata nidhamu ya CHAMA. Njoo uwaseme kwenye vikao vya siri vya CCM!
 
Back
Top Bottom