Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,415
- 12,622
Hao hawakosekani.
Sure mkuu, acha tunaoinjoi Bongo Movie tuendelee kuinjoi.
Hao hawakosekani.
KweliSure mkuu, acha tunaoinjoi Bongo Movie tuendelee kuinjoi.
Bongo Movie Mungu anawaona!Mdada amekufa alafu wemembeba skert ikifunuka anjifunika vizuri
Me napenda kuangalia manyamanyama tu yaleKuna ktu k1 tu ambacho huwa knanfanya kuchek bongo muv,kuangalia watoto wa nguvu wakiwa kene pamba za kjanja
iv ile muvi ya majuto na wenzie inaitwa inye plus nayo sion kama ina maadili kabisa..wala haichekeshi cha zaid ipo kama ponograph..

Bongo movie ni takataka na makelele tu,kitu bora hujiuza chenyewe na si kwa kushikiwa bangoInakadiriwa kwamba kiasi cha shillingi bilioni 12 hutumiwa kila mwezi na wa-Tanzania wa kipato cha kati na cha juu kwa ajili ya kuangalia imported movies kutoka Hollywood katika cinama halls mbalimbali hapa jijini. Hii inasikitisha kwa kiwango flani kwani pesa hizi zote zinakwenda nje ili hali tuna Movies (Bongo movies) za hapa ndani ambazo zinazidi kupanda ubora siku hadi siku, hivyo ingefaa sana movie hizi nazo zingeonyeshwa kwenye Cineama halls muone jinsi watu watakavyofurika na madem zao kuziangalia.., hii ingeinua sana uchumi wa industry yetu na uchumi wetu kwa ujumla. Nawasilisha.
Tutaenda kuangalia mikoa mingine,kule Tunduma watu huvuka mpaka kwenda kunywa viroba huku wakiwapungia mikono polisi wa TZ na wakishalewa hurudi TZ.Kwa watu waliofika Tunduma nadhani wanujua huo mpaka ulivyo ,Hongera RC kwa kuonyesha uzalendo japo ni maamuzi magumu kuzuia filamu za nje na si wote tulio furahia, twende kazi.
king majuto yupo vizuri Sanaa tatzo ni production mbovuHuyu majuto ni moja ya waigizaji wapuuzi kupata kutokea dunian.angekuwa baba yangu ningemkana anaigiza movie za kipumbavu sana na hazina maadili. Ingawa yeye na watu wenye akili kama zake wanaamin ndo anachekesha.kiukwel sikuwah kuona anachochekesha ni nini zaid ya utoto utoto.
Kitu hicho!Eti soko la kimataifa wakati zile subtitles ni vituko mwanzo mwisho!! Ki-english cha hurry hurry no blessing!! Bongo movie bado sanaaaaaa, wao waendekeze ngono tu ndicho wanachoweza!!
Umeongea point mwanzo mwishoNionavyo mimi Bongo Movie wanahitaji kufanya utafiti kwanza kabla ya kulalamika. Dunia ya sasa ni ya ushindani kwa kila kitu, suala la kutegemea kubebwa kwa uzalendo halipo. Wanatakiwa wajiulize tatizo lipo wapi? Ubora wa filamu? Maudhui? Waigizaji? Watanzania wanataka nini?
Kimsingi Bongo Movie kuna kundi ambalo siyo wabunifu kabisa na hawaijui film industry ikoje. Kwa mfano filamu nyingi za magharibi zinabase aidha kwenye vitabu vilivyotungwa na waandishi mahiri au matukio halisi kwenye jamii ( angalia sinema za James Bond zinabase kwenye novel za Ian Flemings au sinema iitwayo John Q ya Dezel Washington inayoakisi maisha ya tabaka fulani). Kwa kufuata hivyo mtu anahamasika kuangalia filamu.
Tulikuwa na tunao waandishi mahiri wa vitabu hapa nchini kwa mfano marehemu Elvis Musiba ( Njama, Kikosi cha Kisasi nk), Hammie Rajabu, Ben R Mtobwa ( Tutarudi na Roho Zetu?) na akina Eric Shigongo ( Rais anampenda mke wangu) na wengine wengi, lakini hakuna mwigizaji aliyethubutu kuigiza kutoka vitabu hivyo. Hivi ni nani hatoshawishika kuangalia filamu ya Willy Gamba?
Watazama filamu hushawishika na stori kwanza kisha kujua nani aliyeigiza (Angalia Bourne Identity, Bourne Ultimatum). Bongo movie wao wanang'ang'ania stori ambazo hazivutii, hivyo hata kama itaigizwa na gwiji JB itaonekana hovyo tu.
Teknolojia pia inawaangusha Bongo Movie. Wanatumia vifaa duni sana kutengeneza filamu. Camera, editing, production ni kama za kurekodi harusi, kweli jamani?
Ushauri wangu ni kuwa wasijipe umaarufu kama vile wameshafanya kazi kubwa sana kwenye film industry, wakae chini na kubuni vitu vitakavyosisimua watazamaji na siyo kutoa kitu kisicho na mashiko halafu kulazimisha watu waangalie. Wawashirikishe wasomi katika taaluma hii ili kuwakwamua hapa waliponasa.
This made my morning. Huyo jini vipi Anagongeka na gari??? Daah.