Maadhimisho ya siku ya Wanawake wilaya ya Mbogwe za tarehe 7/3/2024 bado takwimu za unyanyasaji wa kijinsia zipo juu

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,548
3,460
Wilaya ya Mbogwe Leo inaadhimisha siku ya Wanawake Duniani chini ya kaulimbiu " WEKEZA KWA WANAWAKE KUHARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA NA USTAWI WA JAMII" huku takwimu za unyanyasaji zikionesha wanawake waliofanyiwa unyanyasaji na kutoa taarifa zikiwa 1309 na wasichana zikiwa 50.

Taarifa iliyosomwa mbele ya Mkuu wa wilaya Mh. Sakina Jumanne Mohamed bado inaonesha idadi mdogo ya Wanawake wanaofanikiwa kumaliza shule (Darasa la saba na kidato cha nne).

Baada ya kukaribishwa Mkuu wa wilaya alianza Kwa kusema kuwa "Kaulimbiu ya mwaka huu ni pana sana na ni vizuri sana watoto nao wakishiriki kwenye maadhimisho ya aina hii Ili kuweza kuwajengea msingi wa kujifunza mazuri". Aliendelea kusema masikitiko yake kutokana na mwitikio duni wa Wanawake kwenye maadhimisho ya aina hii. Lazima akina Mama wahamasishwe nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na tuhakikishe tunaweka na kliniki za kupokea kero mbalimbali za Wanawake. Kliniki itamsaidia kuongeza tija ya siku hii badala ya kuwa siku tu ya kusheherekea na kuondoka.

Taifa linapokuwa na nguvu ikumbukwe lina nguvu ya Mama. Sharti tukubali kuwa nguvu ya Mama ni kubwa. Wanawake wana thamani kubwa sana na wakitumia nguvu ya upendo vizuri watafanikiwa. Wanawake wanapaswa kufahamu ndoa inapaswa kuwa na huruma na upendo na siyo kunyanyaswa.

Mwanamke anaponyimwa uhuru wa kiuchumi, kujadiliana na wenzake Kwa misingi yoyote ile anakosa haki ya msingi. Wanawake wamekuwa wakiacha au wakichelewa kuchukua hatua Kwa kisingizio cha subira

Mwanamke jikubali kabla hujakubaliwa, jipende kabla haujaoendwa. Wanawake wengi wananyanyasika majumbani wanabumilia tu. Ukiona mwanamke upo kwenye ndoa na una mateso ujue bado haujampata mwenzi wako, omba Mungu akusaidie.

Lakini ikumbukwe pia adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzako, waangalie sana marafiki zako wenye nia ovu. Ukiweza acha urafiki nao "delete".
 
Back
Top Bottom