Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

Luhanjo atoa ripoti, Jairo arudishwa kazini

Sasa tumuamini nani? Pinda anaesema angemfukuza, au luhanjo (jk) aliesema jamaa hana makosa????mmh comedy haziiiishi bongo

Mpwa kuijadili serekali hii ni kujitafutia ban ya maisha kwa mods na kujipa presha bure. Tuombe mungu atuongoze vyema 2015.
 
Hii imekaa safi sana.

Chadema mkiwa IGUNGA, chukueni mikanda ya maneno ya PM Pinda na mwisho maneno ya CAG.

Msisahau barua ya Shelukindo aliyoisoma Bungeni na mkiwa huko, muwashitaki kwa Wananchi.

Hadi leo hii, CCM wameona wajifunge goli jingine ili muradi tu waishi siku moja zaidi.
 
BAADA YA MAKAMBA WAPIGANAJI WAPYA WENYE UCHU WA KUIUA KWA HARAKA
ZAIDI SERIKALI YA KIKWETE WAIBUKA UPYA NDANI YA SERIKALI YA CCM!!!


Baada ya kustaafu kwa Mzee wetu Yussuf Makamba na madai kwamba anakiua serikali ya JK kwa kauli zake zenye kukaribia kukosa umakini, hilo lilikua ni pigo kubwa kwa Wapinzani nchini na harakati za ukombozi.

Lakini, Mungu Mkubwa, Makamba wengine hivi sasa wamejitokeza na ni wenye msaada mkubwa mno kuua serikali ya JK kwa kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi.

Watu hawa wenye madaraka na MAAMUZI KERO kwa umma kila kukicha na hivyo kuonekana msaada mpya kwa wapinzani nchini ni pamoja na 'GreyMan' Mzee Luhanjo, Ngeleja, Ndugai, Msekwa na huyu Mwanasheria Mkuu 'Jina'.

Chonde, ongezeni juhudi zaidi ya zile za Yusuffu enzi zile!!!!!!!!!!!!
 
habari zimeniharibia siku, natamani nisiendelee kuwa mlipa kodi wa nchi hii
 
Pengine ulikuwa uongo hazikuchangiwa 1 billion, sawa; lakini wanatakata kutuambia ni watendaji wangaji walioenda bungeni na kutumia shs milioni 500? Milioni mia tano kwa watendaji kuenda kuhudhuria bungeni?
Hizo taasisi zilizochangia, wamezitoa wapi? Mifukoni mwao au pesa za walipa kodi?
Magamba, wacheni usanii, tafadhalini! Tumeshachoshwa!

Mkuu nadhani ni vyema tukapata taarifa yote kwa usahihi. Kuna vitu vya kujiuliza hapa:
  • Je pesa zilizochangishwa zilitolewa benki na kulipwa?
  • Je hizo pesa zililipwa kwa watu na kama ni watu ni kiasi gani kwa kila mtu na kwa muda gani?
  • Kama hazikulipwa kwa watu zililipwa wapi? Kama ni kwenye mahoteli je hao watu hawakuwa wamelipwa posho kwenye idara zao?
  • Kama EWURA walichangia gharama za chakula na malazi hayo mamilioni yalikuwa ya nini?
  • n.k
Report ya CAG inabidi iwe hadharani. Naye pia anaweza kuhojiwa tu si ni mtumishi wa umma. Report yake haiwezi kuwa ndiyo alfa na omega.
 
kwa hiyo huyu luhanjo kasikiliza yale maneno aliyosema yule shelukindo beatrice sio??....... hii ndo bongo
 
Tulitaraji majibu ya namna hiyo...hakuna jipya hapo? Mungu Ibariki Tz na sana sana wabariki viongozi wake ili wajue namna ya kuwatumia wananchi wao!...na wote na tusema Amen!
 
Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo,ametoa ripoti na kusema Jairo anarudishwa kazini kuanzia kesho.

===========
UPDATES:

Luhanjo anasema tuhuma zilikuwa za uwongo
Anasema taasisi za Wizara hazizidi 7 na si zaidi ya 20 kama ilivyodaiwa
Taasisi nne tu ndizo zilizochangia na zilichanga karibu TZS 500mil na si zaidi ya 1bil kama ilivyodaiwa
Pesa zilichangwa ili kuwawezesha watendaji watakaoenda kwenye bunge la bajeti
REA walichangia 50mil
TANESCO walichangia 40mil
EWURA waliombwa 40mil lkn hawakutoa, walichangia gharama za chakula na malazi kwa watendaji wa Wizara
Idara ya Uhasibu ya Wizara ilitoa 150mil
Idara ya mipango ya Wizara ilitoa 278mil

More updates to follow

Kuwawezesha watendaji???

Hapa ndio ninapochoka na wana Magamba.....
 
Pia nataka kujua hayo mamilioni wanaaccount vipi katika vitabu vya serikali au ndio kwa mgongo wa posho?
 
yaani mahasira ambayo ninayo waswahi9li wanasema one day yes kikinuka tutafutana humu what fk i hate this country
 
nilipo wapa muono juu ya Luhanjo kumsafisha Jairo mlisema hakuna, haiwezekani tunasubiri report, haya sasa endeeleni kusubiri.
 
Kwa mawazo yangu nafikiri Pinda angejiuzulu tu. Alishatoa msimamo wake bungeni kwamba Jairo anastaili kufukuzwa kazi na sasa wengine wamesema hana hatia!!!! Ili Pinda ajiondoe katika hukumu hii bora ajiuzulu tu.
 
Shiiiiit..!, luhanjo can not be serious.! Is it to say kwamba yule mbunge ndo alikuwa mwongo?! Ooh ghoosh.! Its eating me, i'm fed up with dis thngs
 
Usiamini neno lolote lisemwalo na serikali ya magamba. Ni wahuni na wanafiki wa kupitiliza. Hivi kweli wakuu wote wa hapa Jamii Forums na akili zenu mliamini kabisa kwamba Luhanjo au CAG au PCCB au sijui upuuzi gani mwingine wa serikali wanaweza kabisa kufanya uchunguzi halisi wa kisayansi na kitaaluma wa kumtia Jairo kwenye hatia? Tokea mwanzo hii issue ilishaonekana kiini macho. Rais alijua, Ngeleja alimwagiza Jairo, Jairo akatekeleza, by the way Jairo na Jk ni Aki na Ukwa halafu eti mnashangaa Jairo kusafishwa! Wabongo bwana.
 
Wabunge wa CHADEMA watoe hoja ya kutokuwa na imani na mh pinda.anakinzana na mawazo ya bosi wake,mambo hayataenda vizuri,atakuwa ameumizwa kisaikolojia hvyo atashndwa kazi...
 
Tanzania bureee..kichwa cha mwendawazimu, na mwili wake ndo watanzania. inauma sana kwa serikali kupitisha upumbavu huu.
 
KWA NINI IMEKUA NI LAZIMA IKULU YETU MAGOGONI ITUTAPIKIE USONI KWA MAKUSUDI HIVI SISI WALAZWAHOI NCHI JUU YA JAIRO NA SAKATA LA KUTEMBEZA RUSHWA BUNGENI?

Mzee Luhanjo,Greyman wa Ikulu, ni sawa na MPIGA NGUMI UKUTA kwa kitendo chake cha kutudharau sisi wananchi na kero za Jairo KUPENYEZA RUSHWA hadi ndani ya bunge letu tukufu.

Kwa mtaji wa maamuzi haya, ni wazi kwamba serikali ya Kikwete imedhamiria kutuambia ya kwamba JUHUDI ZA JAIRO KUTEMBEZA RUSHWA BUNGENI kusaidia kupitisha miswada kero kwa wananchi wala haikua ni Mradi wake binafsi bali ni kwamba 'NI SISI WAKUU WA HAPA IKULU' ndio tuliomtuma hivyo tunamrejeshea madaraka yake kamili kama ifuatavyo; wenye kujinyonga na mjinyonge tu!

Sasa kwa mtaji huu, hivi sasa ligi ya kisiasa sasa inahamia kuwa ni timu ya Magogoni Vs Timu ya Walazwahoi nchini kusema hapana!

yaani mahasira ambayo ninayo waswahi9li wanasema one day yes kikinuka tutafutana humu what fk i hate this country
 
Back
Top Bottom