GE2025 Luhaga Mpina ajiunga na ACT Wazalendo akitokea CCM

GE2025 Luhaga Mpina ajiunga na ACT Wazalendo akitokea CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sasa rasmi anaenda kupambana na Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi, Polisi, CCM, mpinzani wake wa CCM na TISS.

CCM, Rasimu ya katiba ya warioba imependekeza mgombea binafsi, mambo kama haya yangekuwa rahisi sana kwa kila mtu.. Tukumbushane.

Kisesa ndipo patakuwa na uchaguzi kwingine kuna maigizo, Kila ka heri kwake.
 
Kama ilivyo kwa CHADEMA AMBAO chama cha Roman Catholic.
Nakumbuka 2010 Kanisa lilimsimamisha Padri Slaa kupitia CDM na walimpigia kampeni nchi nzima huku JK akisaidiwa na mwanae na Mkewe tu kwa sababu ht wanaCCM wagalatia walimtenga. Na Mwaka huu Kanisa limemwandaa Mkatoliki mwingine Tundu Lissu. Kanisa likampeleka Padri Slaa na Padri Kitima kuongoza mashambulizi kuhakikisha Mbowe anatoka Madarakani
Kuna mkutano Mmoja mlifanya pale diamond jubilee enzi za akina basalahe, na kapumgu ambao mlimwita bwana yule ambaye mlidhani ndio profesa kuliko wote nchini mkasema ndio tegemeo lenu, siku zilipoenda akapigia GIA hewani ndio Lile jopo lote likasambaratika wengine wakamfuata bwana manvi akawanunulia kanzu mpya wakiwa wanaambatana naye huko kwenye chama Cha vidole na wengine ndio wamepeleka Kambi uzambarauni.Mpo mnazuga wanasiasa
 
Kwani wakina Mbowe, Lissu na wengineo walikuwa wanashindaje kuwa wabunge?
Inabidi umshinde sana sana sana mpinzani wako hadi kura zako zishindikane kuibika ndio utatangazwa mshindi.

Lakini pia kwa siasa ya wakati ule watumishi kibao wa Serikali walikuwa wapinzani wa waziwazi kabisa, mfano (wakurugenzi wa manispaa, miji, majiji ambao ni wakurugenzi wa uchaguzi ) walikuwa hawaogopi kuchukua risk ya kupambania upinzani tofauti na sasa, Ambapo kila mtu ni chawa wa mwenyekiti.

Pia zamani kulikuwa na matajiri ambao hawaogopi kusapoti siasa za upinzani kwa maana ya fedha za kuendeshea mchakato, tofauti na sasa kila mtu kajificha uvunguni walivyoona wenzao walivyoshugulikiwa na Magufuli, RIP.
 
Mimi nasubiria tu wakati wa kampeni ukianza, jinsi watakavyokuwa wanaropoka matusi na kumwaga siri za kambi yao ya MCC
 
Kwenye siasa kuna baadhi ya watu nimeshuhudia wanajiona ni wakubwa kuliko hali halisi. Jambo hilo huwafanya kudharau ma boss zao kwa kujiona wapo sawa nao. Baadaye huchukua maamuzi magumu ambayo huwa ndio mwisho wa safari yao kisiasa maaana majibu huja tofauti na walivyotarajia na zile platform za kutambia zinapotea
 
Back
Top Bottom