Lucas Selelii ajiunga CHADEMA, kugombea Ubunge Nzega

Lucas Selelii ajiunga CHADEMA, kugombea Ubunge Nzega

Kwa kweli watanzania kama tunahitaji maendeleo,tujiunge pamoja kuiondoa CCM Madarakani.Bila ya hivyo tutaendelea kuibiwa maliasili zetu na kuwa Maskini mpaka mwisho wa Dahari.Hongera sana Seleliii!!!!.

kumbe mnaelewa kwamba sababu kubwa inayowafanywa mshindwe kuiondoa ccm ni kule kutokuungana kwenu,lakini huwa mnatuaminisha sababu ni kuibiwa kura.
mwaka huu sijui mtatoka na sababu gani
 
Tabora ni ngumu sana ina wafia magamba na elimu ni ndogo, panahitaji mtu mzoefu na aliyewahi kuwa ndani ya ccm kama lucas

Selelii hataiweza spidi ya Chadema, atatusumbua tu kama shibuda. Labda ahamie chadema atulie awe mwanachama wa kawaida akitaka ubunge asubiri 2020
 
Lakini huyu sijui kama ana mapenzi ya kweli na chama chetu.

Ninaanza kupata hofu na hili wimbi la hawa wanachama "chotara"-wenye damu ya CCM kwa wingi na kwa mbali wana damu ya CHADEMA.

Mkuu hapa ni kutafuta ratio ya kutosha kuitoa CCM madarakani. Baada ya hapo kama mtu haendani na chama ANAKATWA kama alivyo fanywa kigingi Ayatu.lla ambaye watu walisema akifukuzwa chama kitayumba badala yake watu tukajuta kwa nini hakufukuzwa mapema? Maana baada ya kufukuzwa chama kilikuja juu kwa kasi ya uyoga.
 
Hii move ya Selelii kuhamia Chadema, inataka kututibulia mambo yetu, mgombea wa Chadema Nzega ni Bashe!. Selelii amepoteza mvuto!.

Pasco
 
hivi sura yake ikoje?

Lucas Seleliii huyo hapo akiwa na Pinda na Sendeka!!!



Seleleiii.JPG Selelii.jpg
 
Selelii hataiweza spidi ya Chadema, atatusumbua tu kama shibuda. Labda ahamie chadema atulie awe mwanachama wa kawaida akitaka ubunge asubiri 2020

Weeee Selelii ni jembe sana, aliisumbua sana ccm bungeni kwakuondoa shilingi kwenye mijadala. Huyu ndie alikuwa kundi lakina Lembeli, nahuyu ndie alikuwa mmoja wa wajumbe waliotengeneza report ya Richmond. Ni hardcore flani yaani ni type yakina lembeli. Alitolewa na mafisadi sema tu niwale wazee waliokulia ccm ambao walikuwa wanaona hamna chama kingine kinaweza kuwa bora zaidi ya ccm. Ila kwa upepo na mambo waliyoyafanya wapinzani bungeni miaka kumi hii wamejenga taswira nzuri sana kwa wananchi ndomaana usishangae kila mtu sasa anajisikia proud kuwa upinzani. Akaribie tu naaingie kundini aoambane
 
anapoteza muda tu. miaka yote hiyo alikuwa anasubiri nini?

Kwa kweli hili swali hata mie najiuliza sana.kuhusu hawa watu,angekuja mapema angekuwa ameshakitumikia sana chama.Ila sasa anakuja tu kutafuta nafasi hili jambo sio zuri sana
 
Kuna dogo anaitwa ali ndee nae anagombea huko aliwakimbiza hapakati sijui wananchi mnaamuwaje
 
Kwa iyo watu waliokilea chama hapo awali ye akiwa ccm, wananafasi gn Chadema za kugombea?!
Hii tabia ya siku izi siipendi kabisa.
 
Seleli ndio alikuwa kwenye tume iliyomuondoa lowassa madarakani kwenye Richmond, sasa sijui watakutana huko na lowassa
 
jamani point ni kuiondoa ccm acheni waje tukishindwa mwaka huu watu watakata tamaa na upinzani pamoja sana.
 
Lakini huyu sijui kama ana mapenzi ya kweli na chama chetu.

Ninaanza kupata hofu na hili wimbi la hawa wanachama "chotara"-wenye damu ya CCM kwa wingi na kwa mbali wana damu ya CHADEMA.

Kweli aisee maana wanaingia hatua za kugombea alikuwa muda wote kufanya maamuzi, atakuwa amesoma upepo ameona utamshinda, ila kiukweli lilikuwa jembe enzi hizo aisee
 
Huyu anaweza kua mwanamabadiliko wa kweli manake walimtenda huko magambani... Amekaa benchi mda mrefu huenda kashatubu

Hana anachotubu kwani alipokuwa ccm alikuwa matata sana. Kundi la kupiga vita ufisadi. Kundi lake la wapinga ufisadi ni pamoja na Sitta Mwakyembe Kilango na Ole Sendeka. Kosa kubwa la Seleli kama wanavyoamini wengi ni kumsema vibaya Lowassa. Nae kamwekea Bashe na kumwezesha kwani anafanya kazi kwenye kampuni zao. Kigwangala nae kawezeshwa na Salma Kikwete kama wanavyoamini wengi na pia Kigwangala alikuwa anafanya kazi kwenye foundation yake. Sasa ili Kigwa apenye jina la Seleli likakatwa na Bashe katafutiwa kashfa ya uraia nae jina likafyekwa na Kigwa kupeta. Mwaka huu Seleli akigombea kwa tiketi ya chadema anaweza kupita. Uchaguzi 2010 kura za za ccm na cdm tofauti yao ilikuwa kura moja tu iliyoleta vurugu kubwa hadi jengo la halimashauri kuchomwa moto. Hata hivyo amechelewa sana kujiunga sasa akikuta wameshateuana atamlaumu nani?
 
Back
Top Bottom