Lucas Selelii ajiunga CHADEMA, kugombea Ubunge Nzega

Lucas Selelii ajiunga CHADEMA, kugombea Ubunge Nzega

Hii move ya Selelii kuhamia Chadema, inataka kututibulia mambo yetu, mgombea wa Chadema Nzega ni Bashe!. Selelii amepoteza mvuto!.

Pasco

Mkuu Pasco bashe yuko nzega mjini, selelii yuko nzega vijijini akipambana na kigwangala
 
Last edited by a moderator:
Chama chako au cha mbowe? Utaishia kulalamika tu

Wote mtaingia kwenye kupigiwa kura ukimshinda unatangazwa. Hazipo nafasi za bwerere chadema. Na wewe kama kuku mwenye kideri hujaulizwa chama kinamilikiwa na nani. Leo Lumumba hulipwi kwa bandiko la hivi.
 
Weeee Selelii ni jembe sana, aliisumbua sana ccm bungeni kwakuondoa shilingi kwenye mijadala. Huyu ndie alikuwa kundi lakina Lembeli, nahuyu ndie alikuwa mmoja wa wajumbe waliotengeneza report ya Richmond. Ni hardcore flani yaani ni type yakina lembeli. Alitolewa na mafisadi sema tu niwale wazee waliokulia ccm ambao walikuwa wanaona hamna chama kingine kinaweza kuwa bora zaidi ya ccm. Ila kwa upepo na mambo waliyoyafanya wapinzani bungeni miaka kumi hii wamejenga taswira nzuri sana kwa wananchi ndomaana usishangae kila mtu sasa anajisikia proud kuwa upinzani. Akaribie tu naaingie kundini aoambane
Hata Shibuda alikuwa jembe kweli. Alikuwa akimlipua Mkapa kila bunge likikutana. Amekuja chadema akawa wa hovyo kupita kawaida.
 
chanzo ni kipi si CHADEMA wana msemaji? na je watarudi Mwanza kwa kishindo?
 
Wakuu, habari tulizozipata hivi punde ni kwamba, aliyekuwa Mbunge wa Nzega kisha akaangushwa na Bashe Katika kura za Maoni ila Kamati kuu wakampa Kigwangallah Ubunge wa zawadi, katimukia CHADEMA.

Ana mpango wa kujaribu kulitetea jimbo hilo kupitia chama hicho cha makamanda wakukomaa hadi kieleweke CHADEMA.



selelii hata aende chama gani Nzega wamemchoka !!! au anataka aongeze majumba mengine yale ya uzunguni hayakutoshi mr. selelii?
 
Hata Shibuda alikuwa jembe kweli. Alikuwa akimlipua Mkapa kila bunge likikutana. Amekuja chadema akawa wa hovyo kupita kawaida.

Nadhani watu watakuwa wamejifunza kutokana na mifano km iyo yakina Shibuda na wengine waliojifanya undumila kuwili kujipendekeza ccm ....nini kimewakuta? Cheyo, Mrema Zitto maana wananchi wanaona
 
Ambao wanaolifahamu Bunge la Sita(la spidi na viwango,sio hili la katiba,sijui yule alikua Sita version ipi)watakubaliana na mm huyu jamaa alikua type ya Filikunjombe alikua mwiba kwa ccm though alikua ccm wakamfitini na kumuangusha ,ni mzalendo wa kweli.
 
Jana alikuwa akiisifia ccm na akasema Magufuli atamtumia vizuri, leo imetangazwa wapo redio asubuhi, muda huu unatwambia kajiunga chadema, duh sidhani kama ni kweli
 
Hiyo ni tamaa ya madaraka. Jimbo la nzega mjini hawezi kupita asijidanganye
 
Lembeli, Bulaya na hawa madiwani inabidi waanzie benchi na watoe maoni na ushauri wa namna ya kuishinda CCM.

Ni mapema mno kuwaamini na kuwaruhusu kuchukua fomu za kuteuliwa!
 
Hivi yule Seleli aliyeshindwa kwenye kura za maoni juzi kwenye jimbo jipya la Manonga sio huyu?
 
Ni kipindi cha kutafuta urahisi wa maisha kwa miaka mitano ijayo watu wanachakarika
 
Back
Top Bottom