Taarifa kutoka Bungeni Dodoma kwamba DAWASCO/Wizara ya Maji na Umwagiliaji imemwomba radhi Mbunge wa Kyela na Mwenyekiti wa Richmond kwa kumpakazia na kumdhalilisha kuwa mwizi wa maji kumbe sivyo, zimetufanya baadhi yetu tumwangalie mwandishi wa habari mwenzetu, Badra Masoud, kwa jicho la udadisi zaidi. Badra alikuwa Meneja Uhusiano wa DAWASCO ambaye aliwakusanya waandishi mbalimbali wa habari na kuwapeleka kwenye kiwanja alichodai cha Dk. Mwakyembe.
Kabla ya kujiunga DAWASCO Badra alikuwa mhariri wa gazeti la Mtanzania, moja ya magazeti lukuki yanayomilikiwa na Rostam Aziz. Waandishi wengi wananong'ona kuwa Badra, mbali ya kuwa karibu sana na Rostam, ni nanihii ya Lowassa. Achana na hilo, la msingi ni kuwa "alipelekwa" DAWASCO na Rostam/Lowassa kufanyakazi mbili:1) kumwokoa Kaaya, mtu aliyeteuliwa na Lowassa kuiongoza DAWASCO na ambaye alikuwa kwenye hali ngumu ya kushinikizwa na wafanyakazi aachie ngazi mara tu baada ya Lowassa kutangaza kujiuzulu Uwaziri Mkuu mapema mwaka huu. Kazi ya Badra ilikuwa kuwapooza wafanyakazi na kumpamba sana mpambe huyo wa Lowassa, Kaaya. 2) kuendesha mapambano ya Kamati Maalum ya Waandishi wa Habari ya KALOKIRO (Karamagi, Lowassa, Kingunge, Rostam) akiwa nje ya vyombo vya habari lakini kwa kushirikiana kwa karibu na "boi" au "vitwana" wakuu wa Rostam: Prince Bagenda na Deodatus Balile. Kazi yao kubwa ni kuwashughulikia "maadui wa mtandao" kwa taarifa mbalimbali za kashfa kupitia magazeti mapya ya Rostam, Lowassa na Karamagi: TAIFA, NYUNDO n.k.
Wamefaulu kuandika mengi kuhusu Ole Sendeka (eti anawapa mimba wanafunzi), Anne Kilango (eti ana hasira kwa mumewe kukosa Urais), Samwel Sitta (eti ana nyumba ndogo na ni mwizi wa dawa), Dk. Mwakyembe (eti ni mwizi wa maji), Selelii (eti ni mtoa rushwa kutokana na kesi ya kubambikiwa Nzega) n.k.
Badra kamaliza assignement yake DAWASCO, sasa "kapelekwa" TANESCO kumsaidia fisadi mwingine, Dk. Idrisa Rashid ambaye ni mwana VODACOM mwenzake na Rostam na mtu ambaye anatajwa kwenye kesi ya vijisenti kwa kupelekewa zaidi ya pauni za Kiingereza 400,000 kwenye akaunti yake Afrika ya Kusini. Naambiwa akishamaliza assignment yake hapo TANESCO, Badra anajiunga na TICS! Kama si mamluki wa Rostam/ Lowassa, huyu Badra ni nani basi? Ijabu