Lowassa anasafishwa!

Lowassa anasafishwa!

GT, ni kweli aliwahi kufanya kazi DAWASCO na sasa yuko TANESCO?


Ahhh mwanakijiji si unajua tena in the light of DRMASAU vs NSSF naona sasa mimi na wewe itabidi tuwe tuna trade kwa kuleteana evidence sasa je mwenzangu wewe kwenye hili la BADRA uko sawa?



Kama uko sawa then nistue

by the way mimi niko sawa mpaka kwa hao DAWASCO wenyewe...
 
Post hiyo juu imekaa vizuri sana isipokuwa pale kwenye majina ya wanaopakaziwa kuna jina moja la selelii wa Nzega, naomba niruhusiwe kumtoa kwenye orodha ya kupakaziwa kwani yeye na vijakazi wake walishikwa live na takukuru, Nzega pale Tazengwa nakwa habari zaidi vijana wake walipigwa sana na takukuru hadi mmoja wao akakiri kuhusika na utoaji rushwa toka kwa Selelii na ilikuwa kabla ya habari za Richmond Bungeni, kwa swala la Selelii kutoa Rushwa Nzega ina ushahidi wa kutosha narudia ni kabla ya habari za Richmond
 
kiungani, Nimeuliza Hilo Kwa Sababu Ni Rahisi Kwa Kiasi Gani Mfanyakazi Kutoka Wizara Moja Kwenda Wizara Nyingine Hasa Ukiwa Wa Nafasi Ya Kati?
It Depend How Badra Cheap She Is? She Can Be Used Like Condom Again And Again Latter On They Will Silenced Her, It Can Look Like Illines Or Domestic Accident Because She Knows More Knowing Much About Them Make Them Sick And Vanelable , Ask Me About Kyejo The Lawer She Is In Arv Dose Now While Those Who Was Using Her They Are Relaxing With There Mistreses Sapported With Viagra ,remember Yuo Need To Be Stinking Enough Before You Enter Politics Ever Move Must Have Pre Apmtive Mesures,they Like To Use Litle Creature And Week Personality Like Badra Cause The Royalty Of Men Always Is Sheking When The Itrest Has Been Shifted To Another Intrested Group,
 
Baada ya kupitia thread hii na kuiona ni crap, kama wafanyavyo waungwana wengine husoma na kuiacha ijifie yenyewe. Lakini mimi zaidi hapo naomba ipelekwe kwenye udaku. La kama iko hapa kwa maelekezo ya wale wenye kauli ya mwisho hapa kwenye forum wacha iendelee hapahapa.
 
hizi ni idara za serikali ambazo taratibu zake za uajiri hazina uhusiano na wizara husika

I understand that, mimi nilikuwa strictly najibu swali

Originally Posted by Mzee Mwanakijiji
Kiungani, nimeuliza hilo kwa sababu ni rahisi kwa kiasi gani mfanyakazi kutoka wizara moja kwenda wizara nyingine hasa ukiwa wa nafasi ya kati?

Which may have been out of context because ingawa mfanyakazi anakuwa chini ya shirika la umma lililo chini ya wizara, hawajibiki moja kwa moja kwa wizara bali kwa shirika.
 
mmm.jpg


Mhagama,%2BBadra%2Bna%2BSelali.jpg
 
kamanda mbona hilo sio swali kabisa, yaani haina mjadala! jamaa ameanza kusafishwa 4m day 1, na magazeti ya rai, mtanzania na the african ambao baadhi ya wahariri wake wamejengewa mahekalu makubwa tu mithili ya uwanja wa basket!

hata ukisoma gazeti la mwanahalisi la leo linaelezea bayana kinachoendelea kwenye kwmpuni ya habari corporation ambayo mmiliki ni Rostam Aziz.

balile aliyesomeshwa na mbowe(inavyosemekana) kwa ajili ya kufanyia kazi magaeti ya ytanzania daima alimchenjia na kwenda habari corp. ambako aliahidiwa uhariri mtendaji lakini kutokana na mbwembwe zake hakupendwa na yeyote kwenye kampuni hiyo kuanzaia kwa CEO, Rosemary Mwakitwange hadi waandishi wenyewe.

alisimamishwa cheo cha uhariri kwa kujifanya bora kuliko aliowakuta, amini usiamini jana tu amesababisha mhariri mtendaji, attilio tagalile, mwalimu chrisostom rweyemamu na ben mhina kujizulu nyadhifa zao kutokana na kutaka kumsafisha bwana mkubwa EL wazi wazi. soma mwanahalisi kamanda kwani haukuna kilichoachwa na vyote ni ukweli mtupu! hakika waandishi wa bongo wanapotea!


Wakati mwingine posting za aina hii ni nzuri ili kupima joto ya wananchi. Lakini tunamkaribisha mapema kabla sukari haijaisha midomoni maana naona kujilamba kumezidi.
 
Huyu mwache athubutu kurudi kwenye siasa.
Hizo data watu wa jamboforum watakazozitoa kuhusu huyu, bora abaki tu ajenge hoteli na hela za wizi hizo, achunge ng'ombe...

Well, hii nimeitoa kwenye tovuti moja ya kibongo. Imeandikwa na Katibu Mstaafu wa Julius Kambarage Nyerere (Samwel. H. Kasori): Please ejoy it...

Katika makala yangu iliyopita nilizungumzia juu ya mawaziri bila kumtaja Mheshimiwa Edward Lowasa, Mb wa Monduli. Kwa haya aliyoyafanya baada ya kuomba kwa Spika Bungeni na kupewa nafasi ya kwanza ajieleze kuhusu ufisadi wa Richmond, namtafadhalisha asome na kurudia mara kadhaa nukuu niliyoanza nayo hapo juu sambamba na hiyo ya mtaalamu SENECA.

Nukuu (deleted): Reason: ndefu.

Napenda niseme kuwa kwa yale aliyosema Bungeni na Monduli na katika mahijioano ya TVT, Lowasa aliyosema “si mkweli hata chembe moja”. Waandishi wa habari wengi tu wamekwisha mchambua kwa usahihi jinsi asivyokuwa mkweli, asivyo muadilifu anavyopenda kusifiwa kwa gharama yoyote na asivyolitakia mema Taifa letu.

Kama Mwanasheria Mkuu, Mwanyika na wenzake, Lowassa hakuridhika na ushauri wao juu ya Richmond na kuona kuwa ulikuwa na madhara kitaifa, kwanini hakutafuta ushauri wa ziada? Je? Hizo ndizo rasilimali watu pekee nchini katika ushauri wa kiserikali? Je, Vyuo Vikuu na Mahakama Kuu hakuna wataalam wa kisheria wa kuisaidia serikali? Did he leave any stone un-turned?

Kwa mapenzi mema na nchi yangu, ningependa kutoa mfano hai jinsi Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika ki-chama na kiserikali.

Itakumbukwa kuwa huyu mheshimiwa Edward Ngoyayi Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 aliyeenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi kama mtumishi wa chama na serikali. Pia kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi: Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo: “Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma”. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu.

Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema “Bwana Kasori, jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali”. Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu. Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa “Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma”. Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa “Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa”!

Ningependa kuwaomba Watanzania radhi kuwa jibu hilo ( na kwa uzito wa maneno hayo) kuwa: “Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa”

kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; “Kawawa sikumwambia hivyo”! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali. Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa “Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam”. Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.

Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe. mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe (muulizeni maana nasema ukweli).

Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza kuuliza lilikuwa, "Lowasa yuko wapi?" Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema, “Rashidi, huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako, nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?”

Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia “NDIO ALINIAMBIA”. Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa “Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge. Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu?

Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?”. Mkutano ukaisha hapo Msasani.

Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki, sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolimbikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza! Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya “total transgression of CCM regulations and ethics.” Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gani cha CCM na taasisi ipi ya serikali, akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri. Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi ya takwimu za mienendo ya kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si suala la kubebana kwa majina tu!

Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri, alihamaki, "AHH!!" Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.

Japo tuliyapuuza ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa, sasa Mungu kayaanika hadharani. Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.

Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa “Natural Justice” hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli? Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao?

Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe. Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi peke yake tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli?

Ni vema tukakumbuka na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM: katika katiba (ccm) inasema 15 (7) “kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa..."

Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena “For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet! There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious” Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo!
 
Nionavyo ni kama Lowassa mnamuonea tena sana.

Ukifananisha akili ya Lowassa haitofautiani sana na Kikwete, japo Kikwete mjanja wa kuruka viunzi.Nasema wanawiana kwani hawa wote akili, ufahamu na uelewa wao ni mdogo sio tu katika uongozi bali katika general life lao.

Lowassa ni kipofu, hana akili, mbumbumbu ulimwengu huko huku, hasomi alama za nyakati,yeye kang'ang'ania kile akitakacho kwa gharama zozote.Ofcourse yeye ndiye alikuwa awe rais kama mipango yake ingeenda vizuri tangu miaka 10 iliyopita. na bado anataka kwa gharama zozote.

Nasema mnamuonea , kama akipita CCM, AKACHANGULIWA KUWA RAIS, KELELE ZETU NI BURE KUMBE SI YEYE TU ZEZETA MPAKA WALE NDUGU ZETU!!!! AKIFANIKIWA KUPITA CCM KWA ASILIMIA KUBWA NDIYO RAIS!!!!!!!

KWA SABABU LOWASA NI KIPOFU, BASI WATAKAOMPA KURA NI VIPOFU, KAMA WALIOMPA KURA KIKWETE!!!!!!!!

WA KULAUMIWA NI YULE ATAKAYEMPA KURA!!!!!!!!!!!!
 
Na hii mnaionaje? nafikiri muda si mrefu atapokelewa huku.

Ukonga prison cells being prepared for `VIP` guests?
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

MAJOR renovations are underway on at least 15 cells in the notorious Ukonga maximum security prison on the outskirts of Dar es Salaam amid reports that the special holding rooms may be used to accommodate high-profile individuals expected to be prosecuted soon on grand corruption charges.

According to informed sources, the apparent preparations at the prison facility are being done at a crisp pace in anticipation of an influx of so-called ?-'VIP' prisoners.

Other sources have also confirmed that the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) has lined up five major corruption cases for prosecution in the near future against prominent politicians and former senior government officials.

At the same time, the high-level investigation into the external payment arrears (EPA) embezzlement scandal at the Bank of Tanzania is also expected to result in the prosecution of several local business tycoons and other prominent individuals.

The sources say the special prison cells being prepared at Ukonga are self-contained with their own toilet facilities, beds with mosquito nets, and windows. The ongoing refurbishment work includes plumbing, sewerage, and window installations.

It is understood that prior to the renovations, the prison cells were in appalling condition, many of them with flooded latrines

ThisDay
 
Ndugu zangu wa JF, hii ni breaking news: Sasa imethibitika kuwa yule waziri wetu mkuu ambaye aliamua kuachia ngazi kwa kuhusika; iwe moja kwa moja au vingevyo, anatarajia kurejea serikalini kwa nguvu zote na kwamba ameanza kujifananisha na alhaj Ali Hassan Mwinyi, yule rais wetu wa awamu ya pili.

Lowassa kasema atarejea kwa nguvu zote na hakika wabaya wake watakiona cha mtema kuni. Nadhani ana uhakika huo na habari zinasema ameshamueleza Kikwete, kumbukeni ni shwahiba wake mkubwa na ni jicho lake- elewa hajaomba ametaka. Na atapewa.

Miongoni mwa mikakati ya kurejea kwenye serikali ni eti kuhakikisha kuwa nia yake ya kuiongoza Tanzania inafanikiwa kwa njia yoyote ile. Kumbuka amekuwa na nia hiy siku zote mara baada ya kuingia kwenye siasa baada ya kuwa amechuma fedha nyingi kutoka AICC na maeneo mengine, ikiwemo kipato kikubwa kutoka kwenye nyumba zake nyingi Dar na Arusha ambazo zote ziko kwenye prime areas.

Endapo atakosa nafasi hiyo, amemuandaa mtu ambaye Kamanda wenu ameanza kumtafuta ili kuzungumza naye na baadaye kuweka maelezo yake JF.

Waandishi wa habari ni miongoni mwa watu waliotengewa fedha nyingi kwa kazi hiyo. Miongoni mwa mikakati ya awali ni kugeuza mwelekeo wa kumtengeneza Lowassa rais wa mwaka 2015 na kumsafisha kwanza kwa kutumia magazeti ya Mtanzania, Rai, The African, Tazama na huenda fedha hizo zikapenyezwa kwenye vyombo vingene.

Haya kazi kwenu wana JF- huenda tukampata Rais Lowassa, rais Rostam au Rais Msabaha miaka michache ijayo.

Tuinusuru Tanzania yetu kwa nguvu zote.

Usinikumbushe machungu haya na naomba nibaki na imani kwamba hatarudi Serikalini kuendeleza mchakato wa mchwa kula rasilimali zetu
 
Naanza kuona saa ya kuchukua silaha mikononi kuikomboa nchi yetu inakaribia....
 
Gustanza_The: naomba unitumie hata kwenye PM, ile link ya Kasori, maana nina hamu ya kusoma makala zake. Asante sana kwa kutuhabarisha kuhusu this piece of history. Huyu jamaa hatafika mbali!
Waberoya: what you said is true, tusimlaumu individual, it is the collective guilt because we feed and keep a corrupt system alive. lakini hata kama hatujampigia kura Kikwete, mimi na wewe bado tuko guilty kwa sababu tunaangalia tu wakati nchi inazidi kuangamia.
 
Duh, makubwa!! Lowassa & Kikwete - what a team!!. Kwamba moja wao ni Raisi wa Tanzania inaonyesha tulivyo majuha wa kutupwa..
 
Mtandao wa Rostam, Karamagi na Lowassa umeanzisha magazeti mapya manne: NYUNDO, MTANDAO, UMMA na TAIFA kwa lengo la kuwasafisha mafisadi hao na kumtisha Kikwete aone kuwa Urais wake uko hatarini kuporwa na kundi linalopigana kufa na kupona dhidi ya ufisadi Serikalini. Magazeti hayo mapya manne yanaungana na magazeti yao mengine manne ya RAI, MTANZANIA, TAZAMA na ASUMIN kuendeleza mkakati huo wa kumfanya Lowassa Rais mwaka 2010. Wanaposema 2015 ni geresha tu, danganya toto. Tayari kikao chao cha KALOKIRO kimemteua Lau Masha kugombea Urais ikiwa kazi ya kumsafisha Lowassa itashindikana kufikia mwaka 2010.
Jopo kubwa la wandishi mamluki, likiongozwa na Prince Bagenda,Charles Charles, Deodatus Balile, Mhingo Rweyemamu na Manyere Jackton, linayaendesha magazeti hayo kwa malipo makubwa. Lazaros
 
Nakubaliana na wewe 100 per cent. Uandishi wa magazeti haya ni wa kitoto, haufichi maslahi ya wazi ya mafisadi hao. Lakini, kama Mbunge mmoja alivyosema hivi karibuni, Watanzania si mabwege wa kuendelea kuchezewa na wajinga wachahche waliolewa kwa utajiri wa kupora. Hivi Lowassa kweli anadhani anaweza siku moja kuwa Rais wa Tanzania, Karamagi Waziri Mkuu na Rostam Waziri wa Fedha? Wajaribu tuwashikishe adabu.
 
Mie kama wazo lao ni masha basi nitawaona hawana maana kabisa..Mie nimeshawashauri sana waangalie biashara zao na waachane na siasa tu,JK alishawaambia hli na nashangaa kung'ang'ania siasa kama walizaliwa kuwa viongozi,

Mie najua Mwisho wa Masha ni 2010,kwa ubunge coz ataangushwa vbaya sana hata kama akihonga pesa za TANGOLD.Iike mahali tuanze kuangalia ni kwanini wafanyabiashara wote wakubwba wankimbilia Siasa,Kuna nini katika siasa?

Kwanini Mbowe ameingia kwenye siasa ?Kwanini Rostama ameingia katika siasa?Je siasa ni Biashara?kuna kitu ambacho mimi wewe na wengine tunajua kidogo kuhusus siri hii.Je ni nani yupo tayari kutuambia siri hii?
 
waacheni waanzishe lakini wakae wakijua .. "waTanzania si mabwege!" - Dr. Harisson Mwakyembe

Hata waanzishe magazeti 50 tunajua BABA mla rushwa, MAMA mla rushwa sasa huyo anayezaliwa ni mla rushwa pia!


attachment.php



Kibonzo kutoka kwa "Nathan aka Kijasti"
 

Attachments

  • rushwa-mke-mume.jpg
    rushwa-mke-mume.jpg
    43.9 KB · Views: 319
Back
Top Bottom