Lowassa anasafishwa!

Lowassa anasafishwa!

wanaposema kuhusika moja kwa moja na Richmond wana maana gani? Kwamba Lowassa alienda akabeba majenereta na kuyaleta Ubungo na kuyafungua? kama ni hivyo of course not!

Lakini alihusika moja kwa moja na kuingiwa kwa mkataba huo..... absolutely! Si yeye aliyeunda Kamati ya Waziri Mkuu iliyojiingiza katika kazi ya ununuzi wa serikali kinyume na sheria ya manunuzi ya serikali? gademu.. basi jitahidini kutuzuga basi!
 
Wanajaribu kumsafisha ili labda arudi ulingoni ...................si ni mwenaoo???sijui mtakipasua chama jamanii kumbukeni hicho sio chenu fuateni maadili chama na miongozo na si urafiki na influance ya kishikaji.....
 
ccm haiwezi kukubali makosa kirahisi........ccm bado ipo katika zama za kutaka kukifanya chama kama kitukufu kisichofanya makosa.
wanachokosea ni kuwa u cant fool all the people all the time, .......wananchi weshawang'amua.
 
Kwa kuwatetea Mafisadi, wazee wa Chama cha Kaya, Mmerikoroga, maana haitacukua muda kabla tena, morani wenu hajatundikwa msalabani kwa mara nyingine, kwa hii ya Richmond mmemuona kana Yesu amewafia wenye dhambi, lakini hii nyingine itakayoibuka atakuwa shetani yeye mwenyewe, na hili mtaliona wakati mkipunga mshetani ya kisiasa.
 
Habari za kwamba EL hakuhusika moja kwa moja na Richmoduli inatia kichefuchefu
 
wanaposema kuhusika moja kwa moja na Richmond wana maana gani? Kwamba Lowassa alienda akabeba majenereta na kuyaleta Ubungo na kuyafungua? kama ni hivyo of course not!

Lakini alihusika moja kwa moja na kuingiwa kwa mkataba huo..... absolutely! Si yeye aliyeunda Kamati ya Waziri Mkuu iliyojiingiza katika kazi ya ununuzi wa serikali kinyume na sheria ya manunuzi ya serikali? gademu.. basi jitahidini kutuzuga basi!


Oops! Wewe kalaga bao. Wanachosema hawa wajumbe ni kwamba Lowasa hakuhusika pekee; mkuu wa nyumba ndio hasa alikuwa kinara. Ukifika hapa, kwa utamaduni wa CCM, inabidi yaishe. Hapa hutasikia tena kelele za wabunge wa CCM kuhusu hili la Richmond maana wameshajua ukweli na hawana cha kufanya.

Jana nimeongea na mbunge mmoja kijana wa CCM aliyekuwa moja wa vinara katika kumsulubu Lowasa. Anajuta kwa kuwa alikuwa hajui ukweli. Anasema, kwa maneno yake, " Kitila nilipojua mkuu ndio hasa mwenye kilevi na ndiye aliyekunywa nilipigwa butwaa nikabaki mdomo wazi".

Sasa na sisi hapa JF tuna tatizo la ku-single out some few fisadis na kujaribu kuwatolea uvivu. Well, hii inatusaidia sana kutoa hasira, lakini ukweli ni kwamba haisaidii hata kidogo katika kutokomeza ufisadi hadi pale tutakapoamua ku-deal na mzizi wa matatizo. Haya yaliyojiri kwenye kikao cha NEC yatukumbushe kwa mara nyingine tena kwamba tatizo la ufisadi katika nchi yetu ni la mfumo wala sio la watu wachache wachafu. Mfumo mzima ni mchafu-tuna hiari ya kupambana na huo mfumo au kukubali tuishi nao kama sehemu ya utanzania wetu.
 
Usafi wa Lowassa, uchafu wa CCM
*
Ansbert Ngurumo


STAILI ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetumia kujisafisha inavutia, inashangaza, inachekesha na kutafakarisha kidogo. Ni staili inayozua maswali yasiyo na majibu au yenye majibu yasiyoridhisha.

Lililo dhahiri ni kwamba, kwa kitendo cha kujisafisha, kwa kutumia kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), CCM imekiri kile ilichokuwa inakikataa kwa muda mrefu - kwamba imechafuka.

Lakini staili yake ya kujisafisha inatufanya tuhoji upya: Uchafu ni nini? Umeingiaje CCM? Umeingizwa na akina nani? Umeingia lini? Na unaondolewaje? Labda CCM wangejiuliza maswali haya na kuyatafutia majibu ya kina, wangepiga hatua kidogo.
Majibu ya maswali haya yanatosha kuandika kitabu ambacho kitaandikwa siku moja na kuwa marejeo ya vizazi vijavyo kuhusu historia ya ukombozi wa nchi hii kutoka mikononi mwa wakoloni weusi waliojipa haki ya kutafuna matunda ya uhuru wa Watanzania bila ridhaa yao.

Ikumbukwe kwamba zilipoibuliwa tuhuma dhidi ya CCM, hadi baadhi ya watani wake kisiasa wakakiita Chama Cha Majambazi; Chukua Chako Mapema; Chama Cha Majangili; Chama Cha Mafisadi na kadhalika. Viongozi wakuu wa wanachama walipinga, waling’aka, kuwakebehi na hata wakawatisha waliotoa tuhuma hizo.
Katika hali ya kutapatapa na kukata tamaa, na kama ilivyo kawaida ya CCM kufanya propaganda katika masuala ya msingi, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alitamka hadharani kwamba tuhuma dhidi ya CCM ni kelele za mlango zisizoweza kumzuia yeye (akajiita mwenye nyumba) kulala! Wiki hii ni yeye aliyeongoza kikao cha NEC kujaribu kujisafisha, kwa staili aliyochagua yeye na viongozi wenzake. Viongozi wenzake, naye akiwamo, pamoja na wastaafu, wamefunikwa na kashfa nzito mno kichwani hadi miguuni.

Hawaonekani! Hata waliotishia kwenda mahakamani baada ya kuhusishwa na ufisadi wameshindwa kwenda kwa sababu dhamiri zao zinawaeleza ukweli kwamba hizi si kelele za mlango, bali sauti za wanyonge, wenye mali ya nchi hii, ambao hatimaye wamegundua mnyonyaji wao ni nani.

Watuhumiwa hawa wanaogopa yasifumuke mengine wakiwa kule mahakamani. Na licha ya ushahidi wote uliopatikana hata bila kwenda mahakamani, vyombo vya dola vimeshindwa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.

Polisi wetu wameamua (bila shaka kwa maagizo ya kisiasa) kufanya kazi ya kisiasa. Wanakimbizana na vibaka na wezi wakuu mitaani; wanawabambikia kesi wananchi maskini wanaotafuta kwa jasho. Wakati mwingine wanawanyonga ili kuwanyang’anya walicho nacho.
Wanashindwa kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wanaotuhimiwa kwa wizi mkubwa unaofilisi hata maisha binafsi ya polisi wenyewe. Maana kama watuhumiwa walishindwa kwenda wenyewe mahakamani kuwashitaki waliowatuhumu, Jeshi la Polisi lingetusaidia kwa kuwakamata watuhumiwa ili haki itendeke.

Kimsingi, hata wanasiasa makini wanaotaka kujisafisha matope ya ufisadi, walio na dhamiri ya kuonyesha kwamba hapa kuna ari mpya, wangepaswa kuchukua hatua za kisheria ili kujisafisha au kuwasafisha watuhumiwa au kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria.

Huo ndiyo ungekuwa usafi wa CCM na serikali yake. Hapo ndipo rais angeanzia kuisafisha na kuwasafisha wenzake. Angechanganya hatua hiyo na zile fursa kadhaa zilizojitokeza, akabadilisha sura na mfumo wa utawala; akaondoa wachafu na kuweka wasafi; akafukuza wazembe na kuingiza wachapakazi.
Angepata pa kuanzia upya; na tungemsikiliza. Mara zote alizobahatika kufanya mabadiliko madogo na makubwa katika Baraza la Mawaziri zilikuwa fursa muhimu za kutuonyesha nia yake ya kusafisha serikali na CCM. Alishindwa kuzitumia.

Akawahamisha mawaziri kutoka wizara moja hadi nyingine; akawapunguza wachache wasio na tuhuma nyingi; akawabakiza wale wanaotuhumiwa kila siku. Ni sawa na mtu anayefagia nyumba yake halafu akakusanya uchafu wote akaulundika chumbani anakolala; kisha akawatangazia wana familia na majirani kwamba nyumba yake ni safi.

Harufu ya uchafu inayowakera hao, inamburudisha yeye, maana yeye na wao wana tafsiri tofauti ya usafi na uchafu. Tusisahau kuwa kabla aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu, rais alikuwa ameunda Tume ya Profesa Rwekaza Mukandala kumsaidia kuwachunguza mawaziri wake na kumpa ushauri juu ya nani mbovu, nani ana nafuu, nani aondolewe na nani abaki.

Kwa bahati mbaya, hakuunda tume kabla ya kuwateua, ili kubaini ubovu wao. Lakini wengi wa wateule wake ni wale ambao yeye na wao wamekuwa pamoja serikalini kwa zaidi ya miaka 17. Haiwezekani kwamba hakuwajua. Wala hakuhitaji ushauri wa tume.

Wananchi wenyewe walionyesha wasiwasi juu ya baadhi yao. Iweje wananchi wajue udhaifu wa mawaziri, yule aliyewateua, tena mwenye vyombo vya kiutawala vya kumsaidia kuwajua, ajidai kwamba hawajui hadi aletewe taarifa na tume ya ‘kisomi’! Ajabu ni kwamba, hata tume ilipoleta majibu, hakuyatumia. Akawateua wale wale, tena wengine wakamkejeli kwenye vyombo vya habari. Andrew Chenge ni mfano hai. Alipoteuliwa kuongoza Wizara ya Miundombinu, wanahabari wakamhoji kwanini amerudi akasema “muulize rais aliyeniteua. Ndiye anajua sababu.” Chenge alikuwa sahihi.

Na hata baadaye alipoondoka kwa kashfa za kuficha nje mabilioni ya shilingi ambazo hazijajulikana alivyozipata, alitoa kauli nyingine kwamba ameondoka ili kumwondolea ugumu rais. Maana yake, kama si kwa ajili ya rais, Chenge asingeondoka.

Lakini maana kubwa zaidi inayopatikana kwenye kauli yake ni kwamba kama asingeondoka, rais asingemfukuza! Kauli kama hii ilitolewa pia na Lowassa alipojiuzulu uwaziri mkuu, akasema amefanya hivyo si kwa kuwa ana mkono kwenye Kampuni ya Richmond, bali kwa kuwa alitaka kulinda heshima ya chama na serikali.
Baadhi yetu tuliandika kumsahihisha Lowassa, tukasema alijiuzulu kulinda heshima ya rais kwa kuwa wote walikuwa washiriki wakuu katika mradi wa Richmond. Kuna jambo lilitokea wakati ule ambalo lipo hadi sasa. Ile heshima ya chama na serikali haikurejea.

Kwa hiyo, kujiuzulu kwa Lowassa hakukusaidia kurejesha heshima ya serikali na CCM. Na sababu mojawapo iliyosababisha heshima hiyo isirejee ni kwamba mafisadi wale wale wameendelea kuwa viongozi wa CCM na serikali.

Wao walitaka tuamini kwamba fisadi ni Lowassa; akiondoka serikali inakuwa safi. Wapi! Sasa NEC ya CCM imekaa na kumsafisha rasmi Lowassa kwa kusisitiza kauli yake ya awali.

Maana yake ni kwamba CCM na serikali hii ya Kikwete inamhitaji sana Lowassa. Na imegundua kwamba inahitaji kumlinda. Inajua, kwamba tunavyojua, kwamba alipokuwa waziri mkuu, Lowassa hakutenda jambo lolote zito kwa uamuzi wake pekee.

Yote aliyatenda kwa idhini na ushauri wa rais. Ndiyo maana yalipomtokea yaliyosababisha ajiuzulu, rais alikuwa wa kwanza kumtetea, akasema amepatwa na ajali ya kisiasa; kwa kuwa Lowassa ni kiongozi mchapakazi, mwadilifu na mzalendo wa kweli.
Aliyasema hayo huku akijua kuwa umma wa Watanzania unamzomea Lowassa na kumwona fisadi wa kutupwa, maana katika sakata hili la Richmond, jina la Lowassa limetajwa mno kuliko hata la wamiliki halisi wa Richmond.
Hili ndilo ambalo CCM imejaribu kupambana nalo. Na kitendo cha NEC kumsafisha Lowassa sasa, ni uthibitisho kwamba CCM imesisitiza kauli ya Rais Kikwete juu ya ‘uadilifu na uzalendo’ wa Lowassa. CCM na Serikali ya Kikwete inamuogopa Lowassa. Na haikuanza leo.

Lakini woga huu uliongezeka pale walipoona Lowassa anawekewa zulia jekundu kwao Monduli! Woga ulizidi walipoanza kusikia akijitetea hadharani. Wakajua wasipofanya kitu, atalipuka na kulipua mambo. Wakaamua kumlipua yeye kwa njia mbili.

Kwanza, wakawa wanamtumia wajumbe wa kumpa pole na kumfariji kwa yaliyompata. Pili, walipogundua bado ana kinyongo na kwa hulka yake atazidi kusema mengine wasiyotaka aseme - maana alishaamua kujitetea asife kibudu - wakaingiza nguvu ya dola. Wakamuonya. Akaufyata! Hadi leo najiuliza. Kuna kitu gani serikali inaogopa kwa Lowassa? Kitu gani waliogopa asiseme? Na hapa walipofikia, inawezekana hatasema tena; maana wamemsafisha. Wamemziba mdomo.

Lakini usafi huu wa Lowassa una maana gani pana? Wamemsafisha Lowassa kumlinda mwingine. Na ulinzi huu ndiyo sababu ya NEC kuwatisha wabunge na kuwawekea ‘gundi’ mdomoni wasijadili masuala ya ufisadi wa EPA bungeni.

Huu ni uchafu ambao wakubwa hawataki kuondokana nao. Uchafu huu ndiyo asili ya nyadhifa zao. Uchafu huu ndiyo ulaji wao. Ukizungumzwa kwa uwazi, ukaanikwa, hakuna mmoja wao atakayebaki. Hakuna atakayemfukuza mwingine. Na ndiyo maana wamekuwa wakilindana na kuogopana hata mambo yanapokuwa yameharibika waziwazi.

Na ndiyo maana wengine tunatilia shaka hizi harakati za CCM na serikali kujisafisha kwa kuwatoa kafara wachache na kuwakumbatia wengi. Wanataka kutumia ‘usafi’ wa Lowassa kuisafisha CCM na serikali. Lakini wanashindwa kuchukua hatua za dhati kwa mafisadi wa EPA.

Hakuna atakayewaelewa. Hata Richmond (sasa Dowans) bado inaendelea kulipwa mamilioni wasiyostahili (sh 152,000,000 kila siku). Matendo haya ya NEC huku serikali ikishindwa kuchukua hatua dhidi ya mafisadi, ni sawa na CCM kujisafisha kwa kunawa matope. Sote tunajua matokeo yake.

Inavutia kufuatilia mchakato wa namna hii; inashangaza CCM wasivyojua maswali ya mbadala. Si hawa tulio nao.
ansbertn@yahoo.com
www.ngurumo.blogspot.com
+447853850425
 
Habari kutoka Igunga zinasema kwamba Rostam Aziz afanikiwa katika mpango wake. Baada ya maswahiba wake Chenge na Lowassa kushindwa kujisafisha kupitia ziara zao za majimboni. Pia Karamagi ambaye alijaribu kuisafisa TICS bungeni bila mafanikio. Yeye alitanguliza kwanza timu ya watu kwa ajili ya kuwaweka sawa wazee na baadhi ya wapinzani.

Kwa mkakati huo, ametoa fungu zuri kwa ajili ya wao wenyewe kuandaa mikutano ya kumwita tena. Chini ya Mkakati huo Rostam ametangulia kufanya ziara zake za kawaida kama Mbunge. Ni katika mkakati huo ametangaza kutogombea tena ubunge 2010.

Baada ya kutangaza huko katika kipindi cha miezi mitatu ijayo itafuata mikutano ya wananchi wa makundi mbalimbali kumwomba kuendelea kuwa mbunge wao. Wataanza wazee, wakina mama, vijana, walimu, wapinzani na baadaye viongozi wa dini. Pia wazee wa jadi watamtangaza Rostam kama mzawa halisi wa Igunga.

Mkakati huo una uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kwa kuwa toka mwaka 2000 Rostam alishapanga safu yake katika ngazi zote huko Igunga. Hii ndio maana hata katika chaguzi amekuwa akipita bila kupingwa.

Hata hivyo, uamuzi wake umemweka katika mazingira magumu jirani yake Samuel Sitta. Hivyo, wadadisi wa mambo wanasema vutana vutana ya hawa watu wawali zitaurudishia mkoa wa Tabora katika siasa za Tanzania nafasi ambayo mkoa huu ilikuwa nao wakati wa kupinga ukoloni enzi za kina Mirambo na hata katika heka heka za kumwondo mkoloni.

Baadhi ya watu katika CCM wamempongeza Rostam kwa kujisafisha kwa akili tofauti na Mkapa na wenzake.

PM
 
Pm

Unayoyasema yana ukweli hiyo ndiyo nchi yetu ambayo inahitaji nguvu za ziada katika kuikomboa. Nilisema hapa kuanzia chini ni vigumu kuikomboa, kuikomboa tanzania kutaanzia juu kwenda chini.
 
Kakindomaster nakuunga mkono, kama una maana ya mapinduzi,
kama ni uchaguzi sina uhakika kama tutafanikiwa.
 
tuliwahi kuandika hapa, kuwa umaskini wa wanachi wetu ndo unaotufikisha hapa. hawa wanaigunga wanahongwa pesa walizoibiwa wenyewe.

rostam ni mzaliwa wa chimala-mbeya, alikimbilia igunga baada ya kumaliza wale tembo wa usangu yeye na rafiki zake akina mulla na wengine. wao akina mulla wanaendelea kuwaliza tembo hadi leo

kwa mkakati huu wa kuwaganja njaa wana -igunga atatawala milele, aibu! aibu!, aibu yenu wana-igunga na tazameni, mwenyezi atakihama na kukitangaza kiti chenu mahame. inatia uchungu sana
 
kwa mkakati huu wa kuwaganja njaa wana -igunga atatawala milele, aibu! aibu!, aibu yenu wana-igunga na tazameni, mwenyezi atakihama na kukitangaza kiti chenu mahame. inatia uchungu sana
Ule usemi wa waafrica ndo tulivyo wala siushangai!Wananchi wa Zimbabwe jana nimeona wanavyomuunga mkono MGABE pamoja na ugumu wao wa maisha unaambiwa wamevaa mavitenge yana picha ya jamaa yaani jamaa kavaa sare na wananchi!
Siwachangai wana IGUNGA!kuna mdudu ndani ya vichwa vyetu sijui ni nini?sijui ndo upendo umezidi pamoja na kuwa na maisha magumu?
 
Kakindomaster nakuunga mkono, kama una maana ya mapinduzi,
kama ni uchaguzi sina uhakika kama tutafanikiwa.

Mkuu haika kwanza kinachohitajika ni kama EL na NK walivyoshikwa mashati na kutolewa. Hili lilitakiwa watolewe hata kwenye chama. Hiyo ndiyo top down. Usafi lazima uanzie juu na pia kuhakikisha watu kama Chenge na RA wanatemwa kwenye vyama kabla hawajaenda kwa wananchi.

Lakini umasikini uliopo vijijini tena sasa hivi ambapo karibia asilimia kubwa ya watanzania vijijini wanalala gizani na wakati mwingine wengine hawana chakula, watu kama RA watapeta kwa asilimia kubwa sana.

Sema tatizo linalotukuta wao ndio viongozi hata wa nidhamu ktk vyama hata umesikia na katibu ni mtu wao mkuu. Hivyo kazi inazidi kuwa ngumu
 
Pm

Unayoyasema yana ukweli hiyo ndiyo nchi yetu ambayo inahitaji nguvu za ziada katika kuikomboa. Nilisema hapa kuanzia chini ni vigumu kuikomboa, kuikomboa tanzania kutaanzia juu kwenda chini.
Kamwe kwa kuanzia juu kwenda chini hutofanikiwa! Aina ya mfumo huo hauna nafasi tena kwa nchi maskini kama Tanzania. Katika sustainable city programme ambayo ina lenga katika kumshirikisha mwananchi wa chini katika maamuzi ya maendeleo na siasa kwa ujumla, inaonyesha kuwa maamuzi ya kutoka juu hayana nafasi tena katika maendeleo ya jamii ikiwa ni kisiasa au kiuchumi.

Nahisi RA ameweza vema kuitumia theory hiyo, kwa kuweza kuwashirikisha wananchi wa chini katika jimbo lake la uchaguzi katika kutatua matatizo yao ya kila siku, kiasi kwamba pamoja na kelele zote bado anaonekana kuwa anafaa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Iwapo K'master na kundi lako mnataka kupata support ya wananchi wa chini, ni vema kwenda huko huko kwao na kujifunza ni nini wanataka katika maendeleo yao kiuchumi na nini kinachowakera na nini wataka kifanyie kazi mwanzo. Baada ya hapo ni kutafuta njia ya kuweza kuwashirikisha katika kuondokana na matatizo yao. Hii ni njia ya msingi ya kujenga kujijali kwa wananchi hao na kuthamini juhudi zao kimaendeleo na kisiasa.

Narudia tena mfumo wa top to bottom hauna nafasi kwa Tanzania... Tanzania ya sasa inahitaji bottom up approach
 
Narudia tena mfumo wa top to bottom hauna nafasi kwa Tanzania... Tanzania ya sasa inahitaji bottom up approach
Ambayo Muirani huyu ameamua kuitumia ili kuhakikisha hachezi mbali na dola. Yamkini ya kufanikiwa ni asilimia 95%. Kwa mtaji huu safari yetu ya ukombozi ni ndefu mno. Mungu ibariki Tanzania.
 
Wakuu Wakereketwa naomba niwafahamishe kwa wale ambao hawawafahamu members wa Mtandao Safisha Lowassa (MSALO) na Operesheni Safisha Lowassa (OPL).
MSALO ambayo ndiyo Sekretarieti Kuu imeunda Operesheni Safisha Lowassa (OPL) ambayo tayari imeanza kazi yake kwa viwango vilevile vya 'ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya'.

Makao makuu.
MSALO makao makuu ni Dar es Salaam ila Ofisi kuu ipo Dodoma ambayo ina deal na all operations.

Wahusika Wakuu.
1.Jenista Mhagama
2.Catherine Peter Noni.
3.Yusuph Makamba.
4.Andrew Chenge.
5.John Komba.
6.Rostam Azizi ( Head of Finance).
7.John Guninita
8.Peter Serukamba.
9.John Barongo.
10.Nazir Karamagi.
11.Lawrence Masha.
12.Dk.Deodorus kamala.
13.Dk. Emmanuel Nchimbi.
14.Adam Malima.
15.Janet Masaburi.
16.Nawabu Mulla.
17.Adam Kimbisa.
18.Chrissant Mzindakaya.
19.Tomy Mwang'onda
20.Dk.Ibrahim Msabaha.
21.KIngunge Ngombale Mwiru.

Walengwa Wakuu.12.
1.Spika Samuel Sitta.
2.Anne Kilango Malecela.
3.Anne Makinda.(naibu Spika)
4.Dk.Harrison mwakyembe.
5.Lucas Selilii.
6.Christopher Ole Sendeka.
7.Prof.Mark Mwandosya.
8.Bernard Membe.
9.Samwel Malecela.

Founder and CEO.

1.Edward Lowassa.

Co-Founder and Financier.

1.Rostam Azizi.
 
Back
Top Bottom