Mahojiano ya Slot na Liverpoolfc.com baada ya kukamilika kwa ratiba ya majira ya joto ya timu yake...
Kuhusu ushindi...
“Nadhani katika mechi zote mbili tulitengeneza nafasi nyingi, tukafunga jumla ya mabao saba – manne kwenye mechi ya kwanza, matatu kwenye ya pili jambo hilo linatufurahisha sana kwa sababu hakika hatukufunga kila nafasi tuliyopata. Haswa katika kipindi cha kwanza cha mechi ya pili, nadhani tungeweza kufunga mabao mengine zaidi ya tuliyopata. Hivyo kilichonifurahisha zaidi ni uwezo wa kutengeneza nafasi na hata kufunga mabao saba katika mechi mbili ni jambo zuri pia.
Kuhusu kama anafurahishwa na safu ya ushambuliaji msimu huu...
“Ndio, lakini pia tumewapoteza wachezaji wawili bora – Diogo [Jota] na Luis Díaz. Lakini tumempata Hugo [Ekitike] ambaye bila shaka ni mchezaji atakayekuwa muhimu sana kwetu. Rio naye anaonesha mambo mazuri kila mara kwenye mechi za maandalizi. Katika mechi nyingine za maandalizi, nafikiri tuliruhusu nafasi nyingi kwa wapinzani. Leo tumewazuia kabisa – jambo hilo pia limenifurahisha.”
“Lakini kisha kuruhusu mabao mawili kupitia mipira ya adhabu (set-pieces), haswa kwenye mechi ya pili, hilo si jambo unalolitaka – hasa ukizingatia tunacheza dhidi ya Crystal Palace Jumapili, ambao ni timu yenye nguvu kwenye mipira ya adhabu. Hilo ni jambo lingine la kufanyia kazi – tumeshafanyia kazi hilo tayari lakini tutalifanyia kazi zaidi wiki hii inayokuja.”
“Lakini wachezaji wako fiti, wamefanya kazi kwa bidii, wamecheza soka zuri, na wametetea kwa nguvu na kwa ubora – isipokuwa tu yale mabao mawili ya mipira ya adhabu.”
Kuhusu kuboresha timu kwa ujumla...
“Nadhani daima kuna nafasi ya kuboresha kila eneo. Kama nilivyosema, tumeongeza silaha mpya kadhaa – kwa maoni yangu – zenye uwezo wa kipekee. Kwa mfano, Florian [Wirtz] ana ubunifu mkubwa sana katika eneo la mwisho la uwanja. Tumepoteza ubunifu mkubwa kutoka nyuma kwa kutokuwepo kwa Trent [Alexander-Arnold]. Mipira ya Trent ya krosi na uwezo wa kuwatafuta wachezaji waliokuwa wanakimbia ilikuwa ya kipekee sana – nafikiri Flo ana ubora huo pia, japokuwa anacheza nafasi tofauti kabisa. Lakini analeta ubunifu huo, na kasi ya Hugo, pamoja na kasi ya mabeki wa pembeni wote wawili – Milos [Kerkez] na Jeremie [Frimpong] kama tulivyoona leo.
Kama nilivyosema, unahitaji kufanya hatua ya ziada katika kila unachofanya kwa sababu wapinzani wetu nao hawalali – si tu kwamba wanajaribu kuboresha vikosi vyao, bali pia wamesajili wachezaji wengi, kama tulivyofanya sisi. Ndiyo maana Ligi Kuu ya England msimu huu inatarajiwa kuwa ya kusisimua tena.”
Kuhusu kama ataendelea kuvaa tracksuit (nguo za mazoezi)...😂😂😂
“Hapana, sidhani! Nafikiri hata msimu uliopita wakati wa pre-season nilivaa tracksuit pia. Kwa kawaida nitavaa mavazi tofauti, lakini kwa leo hii ndiyo yalikuwa bora zaidi.”