Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Vilabu vitatu vyamtolea macho Muani
Dakika 57 zilizopita
Tottenham, Manchester United na Newcastle wanamfuatilia mshambuliaji wa Paris St-Germain Randal Kolo Muani, 26, baada ya uhamisho wa mchezaji kwenda Juventus kukwama. (Le Parisien)
Winga wa Manchester United Muargentina Alejandro Garnacho, 21, bado ana nia ya kutaka kuhamia Chelsea wakati akijaribu kuondoka Old Trafford msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)
Jaribio la Chelsea la kutaka kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig Mholanzi Xavi Simons, 22, limegonga mwamba kwani timu hiyo ya Bundesliga haitaki mchezaji yeyote wa kikosi cha klabu hiyo ya Premier League kwa kubadilishana (Sun)
Valencia wanakaribia kumpa mkataba mpya kiungo wa kati wa Uhispania Javi Guerra, 22, ambaye anaivutia Manchester United na AC Milan. (Marca)
West Ham wamewasilisha dau la euro 8m (£6.9m) kwa mlinda lango wa Botafogo Mbrazil John Victor, 29, wakati Galatasaray, Everton na Manchester United hapo awali walionesha nia. (Fabrizio Romano)
Lyon wako kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Tyler Morton, 22. (Sky Sports)
Manchester City wako tayari kuwauza kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish, 29, James McAtee, 22, na Kalvin Phillips, 29, pamoja na mlinda lango wa Ujerumani Stefan Ortega, 32, msimu huu wa joto, mradi tu watapata ofa zinazofaa. (Athletic)
Beki wa kushoto wa AZ Alkmaar David Moller Wolfe, 23, anasafiri kwenda Uingereza kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Wolves, huku raia huyo wa Norway akitarajiwa kununuliwa kwa pauni milioni 12. (Sky Sports)
Beki wa Inter Milan,Yann Bisseck, 24, amekataa uhamisho wa kwenda Crystal Palace, ambao dau la pauni milioni 28 lilikubaliwa kwa Mjerumani huyo. (Gazzetta dello Sport)
Atalanta wamekataa dau la pauni milioni 36.5 kutoka kwa Inter kwa winga wa Nigeria Ademola Lookman huku wakitaka kitita cha pauni milioni 43.5 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Fabrizio Romano)
Middlesbrough wamekubali dili la thamani ya £3.5m kumnunua beki wa kulia wa Blackburn Muingereza Callum Brittain, 27. (Sky Sports).