Tetesi za soka Ulaya Jumapili : Newcastle wamsaka Benjamin Sesko, Liverpool yaimarisha dau la kumsajili Isak
Saa 1 iliyopita
Newcastle United wamewasilisha dau la pauni milioni 65.5 kumnunua mshambuliaji wa Slovenia na RB Leipzig Benjamin Sesko, 23. (Sky Sports), wa nje.
Lakini Leipzig wanataka kipengele cha mauzo kiongezwe kwenye mkataba huo kabla ya kufikiria kukubali ofa ya Sesko. (Telegraph - Subscription Required)
Manchester United bado iko kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili Sesko, ambaye bado hajaamua kati ya Manchester United au Newcastle. (Fabrizio Romano)
Liverpool itawasilisha ombi la pili kwa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, ikiwa Newcastle watapata mbadala wake. (Daily Mail)
Arsenal walifikiria kumnunua Isak kabla ya kumsajili mchezaji mwenzake Viktor Gyokeres lakini walikuwa na mashaka juu ya rekodi ya utimamu wa afya yake (ESPN).
Chelsea wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi na RB Leipzig Xavi Simons, 22, na winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 21, badala ya mmoja wao. (Fabrizio Romano), nje
Mshambulizi wa Korea Kusini Son-Heung Min, 33, amekubali kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Soka LAFC baada ya kuamua kuondoka Tottenham. (GiveMeSport), nje
Barcelona wamekataa ofa ya Chelsea ya kumnunua fowadi wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27, kama dau la kubadilishana kiungo wa kati wa Uhispania Fermin Lopez, 22. (Mundo Deportivo - In Spanish),.
Beki wa Uholanzi Jorrel Hato, 19, amekamilisha vipimo vya afya katika klabu ya Chelsea kabla ya uhamisho wa pauni milioni 35.5 kwenda Stamford Bridge. (Sky Sports)
Manchester United wako tayari kutoa dau la pauni milioni 61 kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Fermin Lopez, 22. (Sport - In Spanish)
AC Milan wako kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay Darwin Nunez, 26, kuhusu kuhamia San Siro lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal. (Sky Sports Italia - In Italy)
Crystal Palace wameshindwa kumnunua beki wa Inter Milan na Ujerumani kwa pauni milioni 28 Yann Bissek, 24. (Gazzetta Dello Sport - in Italian, external)