MJUE RIO NGUMOHA
Jina kamili: Rio Bass Ray Ngumoha Adigun
Tarehe ya kuzaliwa/Umri:Agosti 29, 2008 (miaka 16)
Mahali alikozaliwa: London, England (Newham)
Urefu: 1.70 m
Uraia:England 🇬🇧Nigeria 🇳🇬
Nafasi anayocheza: Ushambuliaji - Winga wa kushoto.
Mguu anaotumia zaidi: Mguu wa kulia.
Ameiwakilisha timu ya taifa ya Uingereza kwa level za under 15, 16 na sasa 17.
Klabu ya sasa: Liverpool FC U18
Alijiunga na klabu: Septemba 4, 2024 akitokea klabu ya vijana ya Chelsea.
Mkataba unaisha:Juni 30, 2026
Klabu ya pili:Liverpool FC UEFA U19.
Alipata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha wakubwa cha Liverpool chini ya kocha Arne Slot, alipocheza dhidi ya Accrington Stanley kwenye Kombe la FA mwezi Januari 2025.
Rio Ngumoha aliandika historia katika mechi yake ya kwanza akiwa na Liverpool, baada ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuanza katika mchezo wa mashindano rasmi katika historia ya klabu hiyo.
Ngumoha alikuwa na umri wa miaka 16 na siku 135 alipopata nafasi ya kucheza na Liverpool ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Accrington Stanley kwenye Kombe la FA.
Mtindo wake wa uchezaji ulifananishwa na ule wa mshambuliaji wa Bayern Munich, Jamal Musiala, ambaye naye aliwahi kuwa mchezaji wa akademi ya Chelsea kabla ya familia yake kuhamia Ujerumani mwaka 2019.
Akizungumza na LFCTV baada ya kichapo kutoka kwa AC Milan, Harvey Elliott alimsifia kijana Rio Ngumoha kwa kiwango chake. Alisema:
Hana woga. dhidi ya AC Milan ameonyesha hilo dhidi ya AC Milan, moja ya timu kubwa barani Ulaya. Alikuwa kama mtoto aliyepo uwanjani kwa starehe – japo ni kweli yeye ni mtoto!"
"Anachotakiwa ni kuendelea tu na juhudi hizo, na sisi tutajitahidi kadri tuwezavyo kumsaidia. Nadhani kama ataendelea kucheza kama anavyofanya sasa na kuendelea kujituma, basi kijana huyu ana maisha ya mazuri ya soka yanayomngoja mbele."
Maneno ya gwiji wa Chelsea kwa klabu ya Liverpool; Liverpool wamesajili "Mchezaji wa Kiwango cha Juu" kwa kumsaini Rio Ngumoha, kijana wa zamani wa Chelsea, kwa mujibu wa gwiji wa klabu hiyo ya London, John Terry.
Rio Ghumoha alishawahi kusema kuwa Mohamed Salah ni miongoni mwa role model wake.
Chelsea walikasirishwa sana na Rio kuhamia Liverpool Kama ilivyoripotiwa na Daily Mail, klabu ya Chelsea inaelezwa kuwa "imekasirika sana" na maafisa wa Stamford Bridge "wamejaa hasira" baada ya kumpoteza "kipaji cha kipekee cha kizazi hiki" kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu ya England.