Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Na nyinyi safari hii mnishangaza si kawaida yenu boss wenu sijui kanywa pombe ya aina gani but kinachonisikitisha bei ya kumnunua Hugo Ekitike kwangu ni mchezaji wa kawaida si ya kutoa hiyo hela Bora yule florian wirtz huyu mtu haswa ila sio huyo Hugo Ekitike ana Nini special ya kufanya mtoe hiyo hela sio striker tishio
🤣🤣🤣
Kwa kweli, inaonekana kama FSG wameamua "kufungulia pochi" baada ya Klopp kuondoka kitu ambacho kinaleta maswali mengi kwa mashabiki. Wakati Klopp akiwa na mafanikio makubwa na timu, mara nyingi alihangaika na bajeti ndogo, akitoa matamshi kama "we can’t act like Chelsea" au "there’s no money tree." Lakini sasa, ghafla, inaonekana fixed deposit account ime mature na Wamempa Slot ATM card ya kuzitoa!
 
IMG-20250726-WA0021.jpg
 
Tungebaki na Nenez na Ekitie tukasajili na Guehi basi pamoja na DM mmoja tu tukaanza msimu wetu
We hujui mpira nunez wa nini pale Sasa hivi miaka yote Kawa flop la kudumu epl we chezaji Gani Kila msimu alijirekebishl aje isak afanye kazi na ekitike huu sio mda wa kukaa na maflop
 
View attachment 3416828
Hugo vs Isak in numbers.

Slot ana kibaraua kizito sana kwa huyu dogo aisee.
Shot conversion yupo chini sana ukitazama alipiga shoti 117 na kupata goli 15 ni kwamba haitoshi....
Kazi kwa jopo la makocha kuweka mkatati safiii ili aongeze bidii na tuone magoli

YNWA
Advantage ya dogo ni versatility

He can move from no 9 to any of the four attacking positions
 
Advantage ya dogo ni versatility

He can move from no 9 to any of the four attacking positions
Kwa namna nilivyosoma huyu mwamba ni dizaini kama Bobby Firmino Fulani hivi kwamba ni mchezeshaji na mfungaji....Kule Frankfurt alicheza na Mamosh vyema tu na sasa atakua na King Salah Sina wasi wasi tutegemee Nini.

YNWA
 
Na nyinyi safari hii mnishangaza si kawaida yenu boss wenu sijui kanywa pombe ya aina gani but kinachonisikitisha bei ya kumnunua Hugo Ekitike kwangu ni mchezaji wa kawaida si ya kutoa hiyo hela Bora yule florian wirtz huyu mtu haswa ila sio huyo Hugo Ekitike ana Nini special ya kufanya mtoe hiyo hela sio striker tishio
Henry akaunti yake imedukuliwa SI bure aisee.
Dirisha hili wanamwaga sana ela lakini subiri soon utaona wanaanza mauzo .. ukumbuke pia washauza Trent kwa 10m, Quansah 35m na Kelleher 18m, Philips etc hivyo japo wametoa ela wameanza kurejesha kiasi zilipotoka.....
Bila usajili wa DM na beki mmoja tutapata shinda ndugu na kwakua dirisha bado lipo wazi ngoja tuone namna tunavyoingia vitani kutetea ubingwa wetu.
Kingine hatujanunua wachezaji wengi dirisha ja joto 2024 zaidi ya Chiesa hivyo pesa bado ipo.
1000093196.jpg

Kwa sasa tupo hapo mkeka utabadilika.

YNWA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom