Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Inauma sanaaa kifo kisikie kwa mwingine ila ikifika kwa umpendae maumivu yake ni makali mnooo
 
Asante sana rafiki kipenzi, ndio hivyo bado niko naugulia maumivu na hali ya kutokuamini.
Pole sana Mkuu
Naelewa maumivu yako vizuri maana mimi pia nilifiwa na Mzazi miaka michache nyuma.

Omba Mungu akupe ustahimilivu, Si rahisi.
Ila pia usiache kupita huku jukwaa la michezo
Utapata uchangamfu wa akili.
Jichanganye na watu , ukipata muda wa kuongea, ongea, lia, ukipata watu wa kukusikiliza hisia zako usiache kuongea... Inapunguza machungu.

Nawaombea familia nzima
Mungu asiwaache katika kipindi hiki kigumu.
Twajua ya kuwa Mungu aweza kufanya mambo yote makusudi yake kamwe hayazuiliki.
Bwana alitoa na sasa ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
 
Utakuta waswahili nao wanaiga kma wazungu kuzaa watoto wawili huku akijitapa mimi watoto wengi wa nini

Ndo inakuja kutokea kma hivi mtu huna ata wa kukupeleka hospital
Kaka usikufuru kuna ajali hapa hapa bongo tu zimeondoa familia nzima yenye baba mama na watoto zaidi ya hao wawili. Kikubwa ni kumuomba Mungu atujalie mwisho mwema.

Hakuna aijuae kesho yake.
 
Mimi nimekufuru au nimesema ukweli ambao watu wanaiga wazungu
Kaka usikufuru kuna ajali hapa hapa bongo tu zimeondoa familia nzima yenye baba mama na watoto zaidi ya hao wawili. Kikubwa ni kumuomba Mungu atujalie mwisho mwema.

Hakuna aijuae kesho yak
 
Huwezi amini jana nilikuwa na night shift, nimetoka night na natakiwa nirudi night. Nilipotoka nikalala nimeamka saa saba naingia X nakuta hii kitu nikawa na scroll machozi yananitoka tu nikajiona kabisa sitaweza kwenda night ya pili nikatamani niende bar kunywa nikaona naweza kuharibu kazi.

Kuna jamaa hapa maskani nilimwambia aje alime majani yaliyozunguka nyumba hakuwa amekuja ilibidi nizime simu nikachukua jembe nikaanza kulima majani kuzunguka nyumba kuanzia saa 8 mpaka saa 12 ili tu nisipoteze focus. (Sijawahi fanya hii kazi huwa nalipa mtu afanye).

Sehemu ni kubwa nikajikuta saa 12 kasoro bado nalima tu ndio nikajiandaa kwenda job.

Hawa wachezaji mtu anaweza kuuliza kwanini huwa hupost hata status ila huyu unampost ila hajui tu connection ambayo huwa ipo kati ya sisi mashabiki na wachezaji wetu.

It's so immense kiasi kwamba hata anapohamia tu team nyingine huwa tunaumia sana achilia mbali kufa.

Jota ameniuma mazee hata night ya jana niliomba tu nipumzike nisifanye kazi.πŸ’”πŸ˜­
 
Jamaa ameumiza watu ....
Yaani Kuna groups flani za Wana Liverpool ..watu wanalia kama vile ni ndugu yao....

Jota alikuwa mpole sana, Hana makuu...natural finisher wa hali ya juu...
Ameiacha familia yake katika hali ya kustaajabu...hapa Duniani tuishi kwa unyenyekevu tuu
 
Ukiongeza na fact kuwa ana watoto watatu wadogo wote wamezaliwa Liverpool, ametoka pia kufunga ndia juzi tu na pia amefariki na kaka yake pamoja ambao ndio watoto wa pekee wa familia yao inaumiza zaidi asee
 
Rest in peace Jota
 
Dah! Hiki kitu cha kuwa alikuwa ni mpole ndio kilicho niumiza mimi na kila ukiingia FB au social media unakuta post za kumuhusu yeye yaan mpaka sasa mwili unaishiwa nguvu 😭😭.
Bahati nzuri wiki hii nilikuwa nina ruhusa kazini, yaan ningekuwa na naingia sijui ingekuwaje 😭😭
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…