Captain Marvelous
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 15,313
- 32,605
FSG hawajawai kutaka kuuza hii timu mazima yaani ni mpala wapewe ofa murwa sana.. FSG wao mpango wao ni kuuza hisa kadhaa na wabaki na maamuzi ya mwisho uedeshangi wa timu na si vinginevyo...Sasa ni wazi mambo mazuri yanakuja kama Mpaka SCOUSERS wenyewe wameona ujinga wa FSG na kuamua kupaisha Ndege siku ya Game against Manure yenye slogan inayosena FSG OUT, KLOPP IN.
Nadhani FSG watajua kama waliowaamini sasa wamezindukal
Naona Timu ikiuzwa sasa.
Kwako Captain Marvelous
View attachment 2540683
Ifahamike hawa jamaa wamejaribu mbinu kadhaa kutaka kujinufaisha zaidi kimaslahi na mara zote wameamgukia pua kwa mfano
# walikua waumini wa Super League kutoka na pesa walizoona inaleta.
#walitaka kuuza branding rights ya jina Liverpool nako wakaangua pua.
#walitaka kupandisha bei ya tiketi za mechi mpaka 220, 000tsh kwa tiketi moja hili nalo walichemka.
#walitaka kuwapa wafanya kazi likizo baada ya Corona kuingia kwa kasi Uingereza, hili nalo waliangukia pua.
Hawa FSG ni wawekezaji mahiri sana aisee ukitazama utaona chini yao wamejenga kambi ya mazoezi ya kisasa pale Kirkby ambayo inatumiwa na ngazi zote za klabu. Wameongeza ukubwa wa uwanja na kuanzia msimu ujao Anfield watazamaji wataingia 61,000, haya yote ifahamike ni uwekezaji wa kimkakati ili kuvutia wawekezaji wakitaka kuuza mazima ama kiasi cha hisa...
Forbes wanakadiria value ya Liverpool ni zaidi ya £3 billions kwa sasa ambayo ni ongezeko maradufu(ongezeka mara 10)la value ya Liverpool kutoka kuinunua mwaka 2010 kwa £300m..hivyo wao kutaka kuuza mazima wakati huu ni sawa kwao kwa timu imekua na wakitazama timu nyingi value yao inaishia figure hizo hizo hivyo ni kama mwisho wa kukua kwa value ndio hapo mwisho...
Kinachowasukuma kuuza sasa ni kwa kua pia ule mfumo wao wa sell to buy ulipigwa KO na corona na sasa hautekelezeki na kwa kua wao sio waumini wa kukopa ili kununua wachezaji wanaona ni bora wauze hisa kadhaa wapate kama £500m apewe Klopp aingie sokoni..
Kingine pia uedeshangi wa klabu sasa unachukua karibu asilimia 70 ya mapato yote kwa kulipa mishahara ya makocha, wachezaji na wafanya kazi, kulipa hoteli, umeme, maji nk hii kwa FSG haijakaa powa sana kwa kua wao ni waumini wa kulipa mishahara kiduchu ili kuhakikisha kinachotumika hakifiki asilimia hizo 70 za mapato.. Nk. Sasa wanaona pia soko limebadilika sana kwamba ukimhitaji raw talent kama Halaand anaingia na mshahara wa £400k kwa wiki hii kwao kitendawili kwamba hawana uwezo wa kushindana na vilabu vinavyomilikiwa na nchi ambazo ni PSG, Newcastle na Manchester City..
Mpaka hapo utaona njia pekee sasa ya kuwatuliza mashabiki wanaoamini kwamba hawa FSG ni ma opportunist wasiokua na mpango wa kumpa Klopp kikosi imara kwa kuingia sokoni ni kuuza share kadhaa ili pesa ipitakane anunuliwe MF mmoja au wawili, beki mmoja na strika mmoja ili kumpa Klopp silaha za kupambana kuleta ubingwa wa EPL nyumbani.
Wapo wateja kutoka Abu Dhabi na Bahrain wameishia £2b hii haijawashawishi FSG kuuza.
Kwa kua bado hawajapata ofa wanayotaka maana wengi wameishia £billion ameibuka Henry na kusema hauzi klabu.. Hizi ni siasa ili wale interested parties wapadishe dau lao. Kingine wanatazam City Football Group wanaomiliki Manchester City wameuza hisa kadhaa kwa kapuni ya China na wawekezaji kutoka America Silver Lake hivyo na FSG hawana namna zaidi ya kusaka pesa za usajili kwa kuuza share kiasi.
Sisi hatutaki mambo mengi wao wasepe Liverpool imewazidi kabisa hawa jamaa wasepe tu.
YNWA

