Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Kabisa, watu wanamlaum tu bure, TAA anahitaji kupumzika ila wao wanalazimisha tu
 
Southgate kasema ukweli kabisa bora akomae na Trippier au James kuliko Trent sasa Klopp badala aseme dogo amjibu Southgate kwa kuupiga mwingi kuanzia kushambulia na kudefend ndio leo kaharibu kabisa...

Haya matatizo anayalea Klopp kuwapa hawa wachezaji hati miliki ya namba.. Wachezaji wafuatao wakiwa wazima lazima Klopp atawapanga tu
VVD sio wa zamani..
Salah sio wa zamani..
Henderson sio wa zamani..
Fabinho sio wa zamani..
Trent sio wa zamani...
Robbo sio wa zamani..
Matip sio wa zamani...
Milner sio wa zamani..
Nk nk
Hao wachezaji wote msimu huu wamenza na kiwango cha kawaida sana na Klopp badala aseme laivu bila chenga utasikia oooh jua lilikua kali sana, au upepo au barafu... Hana kifua cha to call a spade a spade na spoon a spoon...

High intensity football inahitaji damu changa exceptional kua robo tatu ya timu lakini sasa Liverpool hii imejaa wachezaji ambao wana hati miliki ya namba na ambao hata wacheze vipi next gemu wamoooo... Kazi ipo.

YNWA
 
Ungekuwa ww ungewaweka hao uliowataja? Thubutu yako
 
"Eras come to an end"
Sasa hivi kila ngaliba mnaekutana nae lazima awakekete.
Sadio Mane endelea kushikilia hapohapo mpaka hizi Broiler (kuku tahira) zije kukupigia magoti.
 
"Eras come to an end"
Sasa hivi kila ngaliba mnaekutana nae lazima awakekete.
Sadio Mane endelea kushikilia hapohapo mpaka hizi Broiler (kuku tahira) zije kukupigia magoti.
Hii era haijakaa powa kabisa... Okay tume enjoi kubaki Big four wakati wengine wakitupwa hukooo tangu atue Klopp lakini kwa kushinda Ligi Pendwa ya EPL hakika tumefeli sana. Klopp na FSG aidha ni vipofu ama ni wabishi kusoma trend ya hii ligi. Kwanza ni kuwatazama Manchester City ni vipi wananyakua Epl almost kila miaka miwili once kama sio consecutive jibu ni rahisi tu upana wa kikosi na ubora wa kikosi chenyewe..
1st 11 ya Liverpool ya Mwaka 2018 ndio hio hio ya mpaka sasa ipo yaaani wachezaji 9 bado ni serial starters mpaka wa leo. Inaonyesha poor planning na poor transition ya mfumo.

Klopp mwenyewe alibugi kuwatoa wanyamwezi wawili wa kazi kazi Mane na Gini na kubaki na wagonjwa wengi tu especially MFs.... Yanayotukuta ameyataka mwenyewe...

Choice has consequences. Klopp pride inamtadika haswa.

Next game ni Rangers.

YNWA
 
Ungekuwa ww ungewaweka hao uliowataja? Thubutu yako

Shinda za hii timu ndugu ni wachezaji kutumika kama ma robot huku timu ina ela za kutosha lakini wala hakuna kununua... Kitambo sana hiki kikosi kilitakiwa kiwe kime evolve kuanzia wachezaji mpaka mfumo..

Mkuu dirisha ngapi za usajili zimepita huyu Babu Klopp akipewa ushauri na pundits kwamba hiki kikosi kimefika mwisho ni wakati sahihi sasa aanze leta damu changa...
Nakumbuka wakati wa usajili ulioisha ma Pundits wa Skysport hua wanasema kila timu inahitaji kuimarisha eneo lipi ili iwe na ushindani.. Kwa Liverpool walisema tunahitaji
Beki wawili(RB n CB)
MF wawili (AM n HAM)
Strika mmoja
Pia wakashauri ni wakati safi Klopp kuwaachie Milner, Kieta na Ox kwa sababu ni failed project ili payroll ipumue na kupisha nafasi kwa wengine especially damu changa below 27yrs...lakini Klopp hakua tayari kusilikiliza hilo suala na Carragher alikomaa sana ishu ya MF.. Dakika za mwisho akaumia Henderson hapo sasa Klopp ndio kwanza akawa mkali hakutaka ataulizwe tena ishu ya usajili MF akisema yeye sio mtu sahihi kujibu swali hilo, matokeo yake wakaanza kutapatapa wakatua Aston Villa kumtaka Luiz haha Steve akakomaa hauzi, wakatua Brighton kwa Caicedo ishu ikawa bei £50m wakasepa, wakatua kwa Tellimans pale Leicester bei ikawa £30m.. Mwishowe haooo Juventus kwa Melo mkopo.. Kimsingi utaona namna gani kulikua na poor planning... Na ukukumbuke Klopp alishajua weakness ya hii timu ni MF ndio maana alitua mapema kwa Tchouameni mazima kabla dogo hajaamua kwenda zake Real Madrid sasa unajiuliza alitegemea muujiza upi kwa hii MF yake isiyoweza kupoza mashambulizi ama kupeleka mashambulizi yaaani ipo ipo matokeo yake defence inakua over worked outrun out muscled tunaishia kuchapika...

Haya ya sasa sio kwa bahati mbaya yapo well documented. Net spend ya Liverpool dirisha hili haikufika hata £60m lakini kwa vile ni timu ya sell to buy hakukua na mchezaji wa kuuza ela kubwa ili Klopp aingie sokoni mazima zaidi ya kusaka mchezaji wa mkopo.

Imagine being Melo unaona gaffer huyooo kwa Milner 🤔🤔🤔....

YNWA
 
Sure kilichobakia ni kufukuza kocha...
FSG hawana kifua labda Klopp mwenyewe aseme nimeshindwa. Hawa FSG kwa huyu Klopp ni asset kubwa sana kwao kibiashara ujio wake umepaisha overall value ya Liverpool brand ndani na nje ya uwanja... Sitegemei wao wamtimue unless mapato yashuke sana mashabikii waanze kusema FSG out hapo sasa watamtoa kafara wakati wao ndio kikwazo kushindwa kumpa ela Klopp za usajili wakati sahihi...

YNWA
 
Tumepatikana msimu huu na ujue sasa ni mechi kila baada ya siku 3 yaani tuwe na subira maana wakati kiwango chetu kipo hovyo sana wenzetu wanapaa hawana utani kabisa....

Tangu Klopp atue Liverpool hajawai kua na nyakati kama hizi yaani tumeshinda gemu 2 msimu huu EPL na kutoa sare 4 ni matokeo ambayo mwenyewe namuona kabisa amevurugwa... Ushauri angesikiliza mapema haya hayapo kabisa.. Lakini akakomaa kuwategemea wazee wake ambao sasa wanapitwa kiulaini kama sio wao vile....

Muda sio rafiki kwa Klopp maana mechi zinakuja kama mvua.

YNWA
 
"Net spend ya Liverpool dirisha hili haikufika hata £60m"

Darwin Nunez mlimnunua kwa €75m
Fabio Carvalho €5.9m
Calvin Ramsay €4.9
Jumla mlitumia €85.8

Mliowauza
Sadio Mane €32
Neco Williams €20
Minamino €15
Marco Grujic €9
Ben Devies €4.7
Total €80.7

Kwenye usajili wenu msimu huu FSG walitoa €5.1 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]


"Eras come to an end"
 
Mechi ngumu ni city tu ee!? Ok
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…