Timu imejaa wagonjwa na bado tunaambiwa ma good times are coming kwa mwendo wa 4G 🤓🤓🤓
Some disappointment in life turns to be blessing = tuchapwe kabla ya dirisha kufungwo ili Klopp na Ma Yankees waache bla bla....
Edwards kafanya mengi mazuri sana lakini usajili wa Ox na Thiago ni janga kwa Liverpool hawana fitness ya ku fit uchezaji wa Klopp... Klopp anahitaji Toyota all seasons car yeye kanunua Euro cars choicy na expensive to maintain...
na hili la kumpa Keita mkataba mpya ndio nasema duniani maajabu yapo.
Klopp wala asijifiche kwa Bellingham asipoleta ubingwa msimu huu EPL itakua jambo njema aachie timu aje kocha mwenye kifua cha kutimua hawa ma dead woods wote... Bora kua na kikosi kiduchu cha wachezaji wazima kuliko hii ya Liverpool ya sasa kumejaa wagonjwa...
Tukumbushane tu ni kwamba Manchester United na Arsenal wamepoteana hili ilikua advantage kwa Liverpool kujizolea makombe EPL season after season lakini tumempa kipara platform kuifanya EPL farmers league...
Chelsea, Arsenal na Manchester United hawatapoteana milele one day watarejea kwenye ubora wao hivyo hii nafasi tulionao sasa ni adimu sana kutokea... Tazama Liverpool ilivyopoteana miaka ileee nini kilitokea Babu Fergie alijikusanyia EPL za kutosha i guess 13 yaaani hii ilitakiwa iwe case study kwa FSG lakini wenyewe wamekaa na kuona Big 4 ni ushindi tosha...
Tutaelewana tu.
YNWA