Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Mnamuonaje huyu Calvin Ramsey?
 
Attachments

  • Screenshot_2022-06-12-15-04-24-550_com.facebook.katana.jpg
    Screenshot_2022-06-12-15-04-24-550_com.facebook.katana.jpg
    155.3 KB · Views: 15
CR7 kwa sasa ubora wake ni kibiashara zaidi kuliko uwajani maana zile gemu muhimu alionekana tu gemu ya Tottenham EPL. Huyu sio tegemeo kwa kurudi kwenye ubora wenu atawachelewesha sana.
Tetesi ni kwamba hakua chaguo la Ole maana hakuedana na mfumo wake lakini pale aliposema anahamia Manchester City basi akawachanganya chap kumrudisha Trafford ndio ikawa mwisho wenu EPL na sasa hata Big 4 mnaisaka kwa kushinda sana.

YNWA
Mbona una pindisha kusema Cr7 alikuwa virus msimu ulio pita na ndiye aliye mfukuzisha Ole kibarua na ndiye aliye fanya timu iwe out of top four.

Au basi
 
Mkuu kipindi cha dirisha la usajiri chanzo cha kukiamini ni Sky sports kwa mbaali Fabrizio Romano. Hao The sun sijui BBC ni kama Ijumaa wikienda tu.
Hats SkySports nao wanaokota okota taarifa tu za tetesi. Ambaye ana %age kubwa ya correct rumours ni Fabricio Romano
 
Mbona una pindisha kusema Cr7 alikuwa virus msimu ulio pita na ndiye aliye mfukuzisha Ole kibarua na ndiye aliye fanya timu iwe out of top four.

Au basi
Upo sahihi jamaa kurejea pale ilikua taa nyekudu kwa Ole sema hakujua achague kipi amkatae mazima ama amkumbali aafu amtie benchi na asiwe main player pale mbele...

Poor Ole akina Fergie na old boys waliokomaa CR7 arejeshwe ndio walimcost kibarua chake Ole. That is if tetesi zote ni za kweli kuhusu ujio wa pili wa CR7 Trafford.

YNWA
 
Mnamuonaje huyu Calvin Ramsey?
Ni under study wa TAA. Kwa namna timu kadhaa mpaka Itali zilisaka saini yake basi hapa tutapata kipaji safi.

Kwa usajili huu ni dhahiri sasa Neco Williams ni biashara sasa Fulham walete huo mpunga.

YNWA
 
Screenshot_20220612_180934_com.android.chrome_edit_799647803319124.jpg

Karibu Anfield Darwin Nunez hakika umechagua mahala sahihi kabisa kukuza kipaji chako zaidi. Hapa utakumbatiwa na mahaba mazito sana na kweli unajituma kazini na wimbo watakutungia...

Hili dili imekaa utamu sana miaka 6 huyu sasa anakuka kuteka hii ligi. Ni play maker kuwaleta wengine mchezoni, anafumania nyavu kwa miguu yote miwili na vichwa yumoo.

Julian Ward mpaka sasa ameridhi mikoba ya Edwards kibishi sana yaaani hatupoi...

Tukumbashane tu Michael Edwards alijiunga na Liverpool mwaka 2011 alihudumua idara tofauti kabla ya kufikia hili la Sporting Director ina maana mpaka FSG wameamua kuajiri kwa kumpadisha Julian kutoka kua msaidizi wa Edwards na sasa kua SD ni jambo la kujivunia.
Huyu Julian Ward ni mbombezi wa soko la Spain na Ureno hivyo tupo kwenye mikono salama. Jamaa ana network nzuri sana tutulie tu afanye yake.

YNWA
 
Tumjue Boss wetu mpya wa usajili.

LIVERPOOL SPORTING DIRECTOR

Jina : Julian Ward
Mwaka wa kuzaliwa: 1981
Aplipozaliwa: England
Timu alizocheza: Morecambe Football Club na Larne Football Club.
Elimu: Degree ya Sport Science, John Moores University.

Kazi.
Mwaka 2001: aliajiliwa na FA kama Performance Analyst.

Mwaka 2002 : aliajiliwa Prozone kitengo cha Performance Analyst.

Mwaka 2008: aliajiliwa Portuguese Football Federation idara ya Scouting, Analysis na Technical. Hili dili alipigiwa pande na rafiki yake wa siku nyingi Carlos Queiroz.

Mwaka 2010: Aliajiliwa Manchester City akiwa kama Scouting Strategist kwa America ya Kusini. Alikua supporting staff wa Mancini wakati Manchester City wanashinda ubingwa wao wa kwanza wa EPL mwaka 2011.

Mwaka 2012: Aliajiliwa Liverpool akiwa Mkuu wa idara ya Scouting kwa Europe akijiwekeza zaidi Uhispania na Ureno.

Mwaka 2015: alipanda cheo Liverpool na kua Meneja wa Pathway and Football Partnership. Ameweza kusaidia klabu kumkuza Brewster kwa mkopo wa Swansea na dogo kufunga magoli muhimu akipandisha dhamani yake na kumpelekea kupata soko la £23m kwenda Sheffield United, pia alishiriki kutoa ushauri kwa Elliott ahamie kwa mkopo Blackburn kwa vile aliamini kocha wa Blackburn ni moja wa makocha wenye kukuza vipaji safi kabisa na hakika dogo alipata uzoefu mzuri kabla ya lile jeraha lake.

Mwaka 2020: Alipanda tena cheo Liverpool na kua Msaidizi wa Michael Edwards kitengo cha Sporting Director akiwa makamu wake.

Mwaka 2021: Micheal Edwards, iliatangazwa rasmi November kwamba atang'atuka Liverpool kwenda kusaka changamoto mpya. Kutokana na hio nafasi kua wazi klabu baada ya kujiridhisha pasipo shaka uwezo wa Julian Ward alipewa ahadi akiondoka Edwards basi hio nafasi ya Sporting Director itakua ni yake. Tukumbushane Liverpool tangu zamani hua wana historia hii ya "recruiting from within" hivyo tuwe na amani kabisa huyu bwana mdogo Julian atakua salama kabisa..
Screenshot_20220612_223822_com.android.chrome_edit_803277439509716.jpg

YNWA
 
Zama za Ronaldo na Messi sasa zipo hatarini kua historia. Wafuatao wanatajwa kua waridhi wa hawa magwiji wa kwanza ni Mbappe, wa pili ni Halaand na wa tatu ni Darwin Nunez.

Muda utasema ni nani sasa atasepa na kufamania nyavu kuanza kusaka rekodi mpya.

YNWA
Duh ndo mwamba Ngoma huvutia kwake sio...huyu Nunez ana msimu mmoja Tu mzuri tiyari ushamlinganisha na kina halaand n mbappe? Overrated player huyu
 
Darwin Nunez muondoe mapena hapo usije aibika msimu huu au ujao
 
Duh ndo mwamba Ngoma huvutia kwake sio...huyu Nunez ana msimu mmoja Tu mzuri tiyari ushamlinganisha na kina halaand n mbappe? Overrated player huyu
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 Kwani Halaand na Mbappe wameshinda Ballon nao wapo kwenye foleni kama wengine hivyo kwetu sasa katua Darwin ambae ni contender kua mmoja wa under 25 bora misimu ijayo. Nina imani nae kabisa kwa taarifa zake tangu atue Ulaya ni dogo anaejua wapi anataka afike na safari yake.
Kingine tangu lini Klopp akatoa mpunga kama huo kwa 1 season wonder... Kama ambavyo wengi walishangaa kwa kutoa £75m kwa VVD akiwa amateur na sasa ameshashinda makombe yote available in Club level UCL, EPL, Carabao, FA, Super Cup na World Club Cup.

Na huyu Darwin atakua vile vile.

YNWA
 
Darwin Nunez muondoe mapena hapo usije aibika msimu huu au ujao
Kwamba Darwin ni Lukaku wa Liverpool 😂😂😂😂hapana huyu japo kachukuliwa bei chee kiasi kwa Lukaku lakini nina imani kwa zile mechi 2 tulivyokutana nao ningeshangaa sana kama Klopp angepita kimya kimya bila kupeleka ofa aisee.

Mpango ulikua Son wa Tottenham lakini walivyoingia Big 4 ikawa changamka kumng'oa pale..

Hii ndio Liverpool tunakua na plan A Son, plan B Darwin na plan C Nkunku wote kwangu wana fit zaidi Liverpool hivyo Mane kwa kweli namtakia mema sana Bavarians.

YNWA
 
Tumjue Boss wetu mpya wa usajili.

LIVERPOOL SPORTING DIRECTOR

Jina : Julian Ward
Mwaka wa kuzaliwa: 1981
Aplipozaliwa: England
Timu alizocheza: Morecambe Football Club na Larne Football Club.
Elimu: Degree ya Sport Science, John Moores University.

Kazi.
Mwaka 2001: aliajiliwa na FA kama Performance Analyst.

Mwaka 2002 : aliajiliwa Prozone kitengo cha Performance Analyst.

Mwaka 2008: aliajiliwa Portuguese Football Federation idara ya Scouting, Analysis na Technical. Hili dili alipigiwa pande na rafiki yake wa siku nyingi Carlos Queiroz.

Mwaka 2010: Aliajiliwa Manchester City akiwa kama Scouting Strategist kwa America ya Kusini. Alikua supporting staff wa Mancini wakati Manchester City wanashinda ubingwa wao wa kwanza wa EPL mwaka 2011.

Mwaka 2012: Aliajiliwa Liverpool akiwa Mkuu wa idara ya Scouting kwa Europe akijiwekeza zaidi Uhispania na Ureno.

Mwaka 2015: alipanda cheo Liverpool na kua Meneja wa Pathway and Football Partnership. Ameweza kusaidia klabu kumkuza Brewster kwa mkopo wa Swansea na dogo kufunga magoli muhimu akipandisha dhamani yake na kumpelekea kupata soko la £23m kwenda Sheffield United, pia alishiriki kutoa ushauri kwa Elliott ahamie kwa mkopo Blackburn kwa vile aliamini kocha wa Blackburn ni moja wa makocha wenye kukuza vipaji safi kabisa na hakika dogo alipata uzoefu mzuri kabla ya lile jeraha lake.

Mwaka 2020: Alipanda tena cheo Liverpool na kua Msaidizi wa Julian Ward kitengo cha Sporting Director akiwa makamu wake.

Mwaka 2021: Micheal Edwards, iliatangazwa rasmi November kwamba atang'atuka Liverpool kwenda kusaka changamoto mpya. Kutokana na hio nafasi kua wazi klabu baada ya kujiridhisha pasipo shaka uwezo wa Julian Ward alipewa ahadi akiondoka Edwards basi hio nafasi ya Sporting Director itakua ni yake. Tukumbushane Liverpool tangu zamani hua wana historia hii ya "recruiting from within" hivyo tuwe na amani kabisa huyu bwana mdogo Julian atakua salama kabisa..
View attachment 2258781

YNWA
Ndio hawa wapo kwenye kikundi cha uchoyo.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom