Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Uzuri wa game za liverpool vs chelsea knockout stage or fainal huwa hazidissappoint, ni nije na me nakuja hivyo

Nashindwa kuelewa tukicheza na nyie huwa tunacheza mpira wa maana ila tukikutana na citu nikama tunaogopa vile
 
View attachment 2224725
Mane bhana ndio nini kupiga penati ya chini vile na kuwapa uhai Chelsea. Hivi mlitazama benchi yao walivyoshangalia kwa shangwe Mendy kuokoa ile penati.

YNWA

Nadhani muda mwengine tusiangalie Mafanikio ya Mtu mmoja mmoja bali tuangalie mafanikio ya Timu.

Since aliposajiliwa Liverpool Mane hajawahi kuwa mpigaji penalty mzuri na ndiyomana hata Timu ya Taifa anapewa na anazikosaga mara nyingi tu.

Hivyo ni wazi jana alipewa Penalty ya mwisho ili imboost kwenye kugombea Ballon D'or hatimae ikawa vice versa.

Muda mwengine tusirudie kosa.
 
Game uliiona lakini? Shida ilikuwa ni pale ambapo kuufungua ukuta wa Chelsea alafu wao walikuwa wanashambulia, ukizingatia wachezaji wetu wamechoka kulingana na race za EPL, EFL na FA unaweza kata tamaa, all in all tumebeba kombe let us enjoy.
 
Sasa hivi Liverpool imekuwa na Wapigaji Matuta hatari sana Yani huwezi kuamini! Hivyo tukifika Matuta na Real Madrid Sina wasiwasi kabisa.

Imagine na jana tulikuwa na Matuta yetu Matatu ya uhakika yapo jukwaani, SALAH, FABINHO na ORIGI.

Uwanjani kuna:-
Milner
Thiago
TAA
Jota
Firmino
Tsimikas
 
Game uliiona lakini? Shida ilikuwa ni pale ambapo kuufungua ukuta wa Chelsea alafu wao walikuwa wanashambulia, ukizingatia wachezaji wetu wamechoka kulingana na race za EPL, EFL na FA unaweza kata tamaa, all in all tumebeba kombe let us enjoy.

Hapana! Issue sio kuufungua ukuta wala kushambuliwa, issue unapoangaliwa mpira unatakiwa uwe na Confidence + hope.
Sikuzote katika maisha haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia but kuamini kama utashinda.
Sio jambo zuri kwa Mshabiki kuanza tu game tena ikawa mwanzo mwisho unatanguliza kauli za kufungwa tu.


Mimi kipindi nakaa home niliacha kuangalia mpira home kwasababu ya Baba yangu mzazi! Unajua kwanini?
Toka mpira unapoanza analalamika kufungwa mpaka inamaliza! Hata kama dakika ya 90' munaongoza 3 kwa 0 basi utamsikia 'Ahhh yatarudi muda wowote haya'.

Hivyo ukiangalia Mpira Jiamini na kuwa na Imani ndugu.
 
Tetesi ni kwamba Klopp aliwauliza wachezaji wenyewe kila mmoja aseme atapiga penati ya ngapi hawakupangiwa kwamba fulani apige ya kwanza au huyu apige ya 5 hapana mbali kila mmoja kwa kinywa chake alisema nipige ya 2 mara mwingine ya 7 nk...

Kweli Mane hajawai kua mpigaji bora wa penati tangu ametua Liverpool sikumbuki hata kwenye mechi za kawaida kama aliwai pewa penati maana nakumbuka zamani ilikua Coutinho akaja Bobby akaja Milner na sasa ni Salah.

Hili Ballon tukomae zaidi kule Paris tuchomoke na ushindi na sioni wa kumzima kuikosa.

YNWA
 
Uzuri wa game za liverpool vs chelsea knockout stage or fainal huwa hazidissappoint, ni nije na me nakuja hivyo

Nashindwa kuelewa tukicheza na nyie huwa tunacheza mpira wa maana ila tukikutana na citu nikama tunaogopa vile
Manchester City ni moja ya timu inaongoza kushinda mpira wa pili uwanjani popote pale haijalishi ni upande wenu au upande wao hapana jamaa wataku harass mpaka utaachia mpira na kwa vile wana quality ya kaunta na ballers lazima mateso yatokee. Mfumo wa Manchester City upo peke yake na wachezaji wa Pep anachojua wote ni workaholic kule hakuna pedestrians ni mbio dakika 90.

Sasa ukija Liverpool na Chelsea tuna walimu almost wana identical philosophy ya uchezaji kasoro tu wachezaji tulionao hivyo gemu hua zina balance kiasi fulani..

Jana fainali ilikua safi ukizingatia wachezaji uchovu sasa umewakamata walijitahidi sana kutupa burudani.

YNWA
 
Mpiga penalty namba moja bado ni James Milner, Salah ni namba mbili. Milner akiwepo dimbani Salah hapigi penalty labda kama Milner atoe go on na sababu kubwa ni kiatu cha mfungaji bora EPL.

Kwa huko UCL Salah hayupo kwenye orodha ya wafungaji bora, ikitokea penalty na Milner yupo dimbani atapiga penalty Milner.
 
Ni sawa ishu muda mwingi sasa babu Milner hayupo uwanjani na pia akiwepo sasa hua anamwachia Salah kama ulivyosema ishu za kiatu cha mfungaji bora.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…