Tuna gemu ngumu sana pazuri ni kwamba wengi walitegemea tusiwepo tulipo yaaani wanaobeti majuu wakati ligi inaanza kuanzia nani bingwa mpaka nafasi ya 4 mbona wameliwa mazima maana wengi wali beti Manchester City bingwa, Chelsea wa pili, Manchester United wa 3 na Liverpool akipambana sana kuingia nafasi ya nne.
Lakini Klopp kama Klopp akawa anawachora tu akijua fika vijana alionao wataleta ushindani wa kutosha na kweli imekua sapraizi kwa wengi nafasi hii ya pili tulipo imewavuruga mpaka ma pundits wapinzani wanaishia kutoa pongezi za kweli kwa Klopp wakiongozwa na Gary Neville nk.
Msimu uliopita tulipata majeruhi ya kutosha tukapoteana sana mpaka kumaliza big 4 tulihitaji msaada wa Alison afunge goli la msimu



sasa naona ma pundits wengi walitegemea eti akina Mane, Salah, Firmino hawawezi tena kupambana kupata ubingwa eti wametumika sana pale Liverpool hivyo ni muda sahihi kuwapisha Manchester United na Chelsea wafukuzane na Kipara kwenye ubingwa wa EPL.
Kutoka kutabiliwa kumaliza ligi nafasi ya 4 au 5 mpaka kumkimbiza Kipara mpaka anakonda tunastahili kujipa cheers jamani sio jambo rahisi kumkimbiza Kipara mwenye backing ya Mansour oil money aisee. Klopp anachokifanya pale ni dhahiri ni cha kupongezwa. Kututoa alipotutoa na kushinda EPL baada ya miaka 30 kwa wachezaji wa ku unga unga wakati mashindani wetu ana pointi ma talent kwa bei yoyote hakika Shikamoo Babu Klopp.
Cheers to all Liverpool fans ambao ni BELIEVERS OF LIVERPOOL COURSE.
Tuna gemu ngumu nyingi tu kwa mfano tuma gemu na Tottenham, tuna gemu na Manchester United, tuna gemu na Everton, tuna gemu na Wolverhampton nk zote hizi hakuna rahisi lakini tunaamini vijana wetu watapambana kadri wawezavyo kutoka kifua mbele na pointi 3 muhimu.
Ki ufupi niseme kila mmoja ashinde mechi zake mahesabu sahihi ni Mei 22 baada ya mechi.
MALAIKA WA USHINDI LEO TULETEE POINTI 3 UGENINI NA TUSHINDE GEMU HII NGUMU.
YNWA