Wanabodi nichukue fursa hii kuwa wish mwaka mpya 2022 wenye heri na neema.
Nafarijika sana kua mmoja wa familia ya Liverpool hapa JF hakika mwaka 2021 umekua ni matokeo mchanganyiko kimatokeo kwani tulianza mwaka kwa kususua sana kutokana na majeruhi na wachezaji kuchuja kiwango lakini baadae Klopp alipambana kupata jawabu na tukamaliza ndani ya big 4 2021.
Mwaka umeisha tukiwa pazuri japo sasa kwa mbali ni kama upepo umekata zile kosa kosa pale mbele zimerudi kwa kasi ya 5G bila shaka nina imani na Klopp na jopo lake kupata majibu vijana warejee kwenye ubora kwani kumkimbiza Kipara Pep hua hakuna kulegeza kamba.
Kwa namna ya pekee tuzidi kushikamana tuzidi kuwaombea mafanikio vijana wetu na sisi tutembee kifua mbele.
Ubingwa wa EPL kwa ufupi upo kwa kipara asilimia [emoji817] na sioni akiuachilia. Pazuri ni kwamba kuna Champions League, kuna Carabao na kuna FA hivyo tuna nafasi bado ya kupata angalau kombe lolote hapo.
View attachment 2064383
Tupo pamoja sana.
New year new hopes we are Liverpool we never give up.
YNWA