Captain Marvelous
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 15,313
- 32,605
Kabisa ndugu binafsi niwadiss tu pale timu ipo kwenye nafasi bora kabisa ya kusonga mbele lakini tume stuck kwa kukosa kuingia sokoni wakati sahihi...Tushukuru hata hapa walipotufikisha, tulishapoteaga kwenye ramani kabisa mzee 2010/11-2013/14, 2015/16-2016/17 miaka sita hatujui uefa inafananaje
Im grateful for FSG
Klopp kashajenga msingi wa mafanikio ilikua ni wao sasa kuleta nguzo na kusema kweli walionyesha nia hio japo sasa kwa kutumia njia zisizo endelevu maana hii kutegemea kuuuza ndio kununua ni cycle ina mwisho wake na ukichanganya na covid ndio kabisaaa.. Hata leo FSG wakimsapoti Klopp kuleta MF mmoja (Bissouma) strika mmoja (Halland 😆😆) winger mmoja (Traore🤔🤔) mbona tutakua sorted na hutasikia tena tukiwa diss hapa aisee...
Kingine ni priority zao hua zinachanganya kwa mfano walimnyima Gini mkataba mpya akidai angalau miaka 3 na alipwe above £120,000 kwa wiki. Ikumbukwe Gini ndio mchezaji pekee asiekua na majeruhi ya mara kwa mara na ndio mchezaji aliecheza mechi na dakika nyingi tangu Klopp ametua Anfield. Wakamnyima mshahara na mkataba lakini muda huo huo wakampa semi pancha Henderson mkataba mpya malipo £150, 000 kwa wiki. Hata kwa bila kuingia kwenye data utaona hapa FSG wanatuzingua sometimes...
Zipo tetesi wanatazama situation ya Mbappe kwenda Real Madrid ili wanufaike aidha kumuuza Mane au Salah kwenda PSG ili wao wapate mpunga kununua wachezaji wengine wanaohitajika pale Anfield.
Hivyo hawa Ma Yankees tunawashukuru sana kutuletea
- Champions League Trophy
- Super Cup
- Club World Cup
- EPL Trophy baada ya miaka 30.
YNWA