Mkuu pale juu itakua ishu akikaa huyu kipara wa kutoka Catalan. Hawa jamaa sio watu wazuri aisee.
Klopp bado ana mtihani sana na baadhi ya wachezaji, kupoteza pasi maeneo ya hatari kwetu imekua ndio main weakness msimu huu. Konate, Henderson, Salah kwenye hili waongeze bidii.
Pale mbele nako pamoja na kufunga goli 4 palikua napo pamepwaya especially Jota alipata nafasi za kutosha umaliziaji ukawa kikwazo.
Depth ya kikosi imeanza kuleta ushindani haswa kwa vijana. Tsimikas amekua na wakati mwema sana kila akipangwa na hii imempelekea Robertson kuja ki vingine mechi ya juzi sio business as usual. Alitengeneza nafasi 4 za kufunga magoli. Ni amefanya hivyo mara ya kwanza msimu huu mechi ile.
Sasa kwenye mbio za ubingwa EPL msimu huu hakuna margin of error labda iwe very minimal.
Key focus ni game management ya Fabinho, Thiago, VVD na Jota. Hawa wakibaki salama tupo pazuri sana. Wanaleta balance kwenye timu na kufanya kila idara iwe top performance.
Chelsea naona kumkosa Ben ni dhahiri ni pigo.
YNWA