Unaposema timu kubwa unaamisha timu zipi..
Kwanza hilo la kuweka ofa ni siri ya wahusika na ukumbuke haya yote hayasemwi na wachezaji husika mbali ni bla bla za magazeti na mitadao..
Kwa miaka ya hivi karibu Stev G alibakia Anfield pamoja na kutakiwa na Real Madrid na Chelsea.
Surez alibaki Anfield pamona na kutakiwa na Arsenal na Barcelona.
Bobby Firmino alichagua Anfield badala ya Stretford boys kuleta bla bla.
VVD alichagua kusubiri nusu msimu atue Anfield huku Chelsea kipindi kile wakiwa wamefika bei.
Allison aliichagua Anfield huku nao Chelsea wakiwa wamefika bei.
Mane simu moja tu ya Klopp ilmleta Anfield na kuwakacha Stretford boys..
Chamberlain aliwagomea Chelsea na kutua Anfield.
Elliott alipata ofa kutoka Chelsea, Spurs, Manchester United lakini mwishowe alitua Anfield.
Keita nae Bayern, Barcelona walikua wanamnyatia lakini alichagua majogoo wa jiji.
Klopp alifuatwa na mpaka Babu Fergie akumbali kutua Stretford boys lakini alwagomea na kusema hajaamua wapi atafanya yupo mapumziko na mapumziko yalivyoisha akatua Anfield na kushinda makombe yenye hadhi yote akiwa na Majogoo.
Stefan Bajcetic ametua January akitokea Celta Vigo huku akiwapiga chini Manchester United na Barcelona na kuchagua kuja Anfield.
Kwa haraka haraka nawakumbuka hao.
Ifahamike pia hawa wachezaji ni wafanya kazi hivyo kwao maslahi ndio chaguo la kwanza wapi anatua, cha pili kucheza mashindano ya Uefa na kingine ni aina ya kocha aliepo klabu husika kwa mfano Thiago inasemekana ndoto yake ilikua acheze chini ya Klopp hivyo Manchester City na Manchester United walimkosa kwa sababu hio..
YNWA