TAARIFA JUU YA KUANZISHWA KWA KUNDI JIPYA
sisi
liverpool wazushi (kundi jipya ambalo bado halijapata usajili rasmi) tunaunga mkono kitendo kilichofanywa na
jordan pickford mchana ule uliozikutanisha pande mbili hasimu zinazopatikana merseyside.
sisi
liverpool wazushi tunaamini ya kwamba majeruhi aliyoyapata
virgil van dijk mchana ule ni zaidi ya ufunuo ulioshushwa kutoka kwa mama mpira wenye lengo la kuwakumbusha washika uongozi wa klabu yetu juu ya umuhimu wa kuwekeza kwenye safu ya ulinzi iliokwisha onyesha dalili za ulege ulege tokea kurudi kwa soka baada ya corona.
sisi
liverpool wazushi tulifurahishwa sana na hatua iliofikiwa na klabu ya kumuuza
dejan lovren kwa takribani paundi million 11 na tuliamini ulikuwa ni muda bora zaidi wa kufanya uamuzi huo, lakini tulisikitishwa sana na hatua iliochukuliwa na uongozi wa klabu kwenye uzibaji wa nafasi ya dejan lovren baada ya kuondoka kwake.
inashangaza sana kuona baadhi ya makundi (livepool wajinga, liverpool historia na livepool halisi) yaliunga mkono hatua iliochukuliwa na uongozi wa klabu ya kushindwa kutafuta mchezaji mwenye ubora zaidi ya aliyeondoka, wengine walifikia hatua ya kuwataja wachezaji mfano wa matip na gomez kuwa walinzi sahihi wa kuendelea kushirikiana na van virgil.... Hii ina maana ya kwamba makundi hayo yaliamini bwana virgil ameumbwa akiwa na miguu ya chuma hivyo basi hawezi kupata majeruhi kama wengineo.
sisi
liverpool wazushi tunamtaka CEO edward ahakikishe anakamilisha usajili wa mlinzi wa kati kwenye dirisha hili la usajili, kufanya hivyo kutapelekea mtakatifu wetu
jordan henderson arudishwe kwenye eneo lake halisi la kiuchezaji. Sisi liverpool wanafiki/wazushi tunaamini ya kwamba kutokuchezeshwa eneo halisi kwa jordan henderson ndio kunachangia safu yetu ya ushambuliaji ishindwe kufunga goli kwa takribani mechi 4 na wala hakuhusiani na ishu ya plagiarised (kunukuu mbinu hizo kwa hizo)
kama CEO edward atashindwa kukamilisha usajili wa beki kwenye dirisha hili, sisi liverpool wanafiki tumedhamiria
kufanya maandamano mpaka nyumbani kwa mtakatifu super nahodha jordan henderson ya kumshinikiza asisaini kandarasi mpya hapo livepool kwani tunaaamini ni timu itakayokuwa haina malengo ya kupambana kama ilivyo timu ya ndoto yake ambayo ni ARSENAL
sisi
liverpool wazushi kwa leo tunaambatanisha takwimu za
joel matip tokea asajiliwe mnamo mwaka wa 2016/2017
- 2016/2017 amecheza mechi 29/ 38 za ligi kuu
- 2017/2018 amecheza mechi 25/ 38 za ligi kuu
- 2018/2019 amecheza mechi 22/ 38 za ligi kuu
- 2019/2020 amecheza mechi 09/ 38 za ligi kuu
- 2020/2021 amecheza mechi 09/ 19 za ligi kuu
jumla = mechi 94 za ligi kuu
==============
LIVERPOOL wazushi tunatafuta wanachama kutoka pande zote za mashabiki wa ligi kuu na usajili utakuwa ni bure, pia tunaruhusu lugha ya kiswahili na kichato kwenye mijadala yetu