Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Mkuu hili swala la kuongoza ligi kila mtu alipoongoza ligi ilikuwa inasema tunachukua ubingwa kwa hiyo hata kwa Man U ikitokea ikaongoza ligi sitashangaa kauli zao.

Bado man city kuongoza ligi kwa muda,nayeye akiongoza ligi watu watasema atachukua ubingwa.

Kwa navyoona ligi bado sana kwa sasa hata ukiongoza huwezi kushinda mechi zote mpaka ligi iishe .me nasubiria kuanzia mechi ya 7,8,9 ya mzunguko wa pili pale mtu akiongoza ligi unaogopa maana mechi zinakuwa zimebaki chache.

Me sina wasiwasi najua hilo kombe linarudi tena pale anfield.kelele za man u zisitutishe kabisa wala kuogopa.huyo bruno wao wanao mtegemea ataumia tu wataanza kupoteza.
Kabisa yanii mm bado naimani na timu majanga ya majeruhi tulionao na bado tupo juu ya msimamo amna timu ambayo ingeweza msimu huu mm naona LFC inanafasi bado man u kuna kipindi walikuwa wanazingua mbaya tuu wametusogelea pressure inaongezeka kuna villa akishinda mechi zake anakaa apo nyuma ya mkiaa tutakuwa tunacheza kwa pressure afu umakini unaweza kuongezeka
 
Nakuelewa mkuu, ndiyo maana nikawa nam-favor Jota at least alirudisha ile spark ya magoli, na alikuwa anasababisha kama kaushindani fulani ambapo mwisho wa siku timu inashinda.

Kuna point umezungumza ya kutafuta creative mid isiyo na history ya injury, hili nadhani haliko kabisa kwenye mahesabu ya timu, tena kwa hizi taarifa za Gini kuelekea kusaini ndo kabisa tusahau.
Mkuu Jota hayupo hivyo aanze Takumi ni workhorse dogo na lile goli alilofunga pale Selhurst Park ilikua very crucial kwake na Klopp should have taken a gamble tena kwake...

EPL bado mbichi sana na tuna advantage kwamba hakuna mwenye uhakika wa kushinda every game now and then sasa ikitokea akaanza Manchester City kuanza winning na huo uwezo wanao basi tuhesabu hatupo tena kwenye mbio...

Mnakumbuka vyema msimu wa 2018 2019 tulipata sare za kijinga sana vs. West Ham na vs Leicester na ukawa ndio mwisho wetu kwenye mbio zile.. Na kipindi hicho ilikua hivi hivi ma front 3 walikua kwenye dry spell ya kutisha mno....

Mpaka game ya Southampton Klopp has to find a way to make this boys click oj the right direction...

Vs Crystal Palace we had 7 shot on target and all were converted baada ya hapo we are in deep shit target wise..

YNWA
 
Klopp on Newcastle draw...

Being top] is nice but it doesn't mean anything," Klopp said after the game.

"We drew tonight and we are still top of the table so that just shows how difficult the season is for everybody. When life gives you lemons, make lemonade."

"We didn't get the result we wanted but it's not the worst thing in the world and there are worse things happening," Klopp told Amazon Prime.

"But I liked the game - we are not happy with the result but I'm fine with the performance, because that's the way we have to play and protect.

"We did all that but it's still disappointing."

YNWA
 
Ukimtoa ndio hizo chance hupati tena.

Nafasi alizopata alikuwa alengi goli yeye anapiga nje,mpaka alikuwa anatia hasira,sasa tutashindaje kama anapiga nje?
Ha ha haaaa kwa hiyo Salah akiumia hatutapata tena chance noma sana.

Kocha asie kalili mechi ya jana Shaqili angeingia mapema nafasi ya Salah.
Goli lilishamkataa hata angecheza dakika mia mbili
 
Ha ha haaaa kwa hiyo Salah akiumia hatutapata tena chance noma sana.

Kocha asie kalili mechi ya jana Shaqili angeingia mapema nafasi ya Salah.
Goli lilishamkataa hata angecheza dakika mia mbili
Shaqir delivery is superb...

Zile kona zote na mipira ya adhabu he could have delivered a killer one...

But anyway hizi zote ni maybes...

We ain't playing the worst football either minus the point won...

How the boys turn this dry spell around will be the season changer....

The defense coaches has done a tremendous job defending now TAA need to find his attacking spark.. Robbo been our threat this season from the flanks...

The goalkeeping coach superb pia..

MF its same old story..

Forward coaches need to do real job with our attackers...

We sort thar and boom we aint gonna be getting this useless draws...

YNWA
 
Kuna game atakuja kuanzishwa Shaqiri na atacheza dakika 90' halafu baada ya Mchezo wale wanaomlilia leo watakuja kumtukana hapahapa Shaqiri na Klopp wake.

Tukumbuke ya Origi tu Msimu uliopita kuna Watu walisema auzwe Salah ili achezeshwe Origi, hatimae sasahivi akiingizwa Origi wanataka kupasua TV.
 
Nakuelewa mkuu, ndiyo maana nikawa nam-favor Jota at least alirudisha ile spark ya magoli, na alikuwa anasababisha kama kaushindani fulani ambapo mwisho wa siku timu inashinda.

Kuna point umezungumza ya kutafuta creative mid isiyo na history ya injury, hili nadhani haliko kabisa kwenye mahesabu ya timu, tena kwa hizi taarifa za Gini kuelekea kusaini ndo kabisa tusahau.

Kila nikiangalia kuwa Milner anaelekea miaka 35 na bado anaaminiwa basi nazidi kuamini Kuwa Mido ya GINI na HENDO watacheza ndani ya Liverpool mpaka kufikia umri wa kama Milner.

Hivyo basi Klopp kamwe hatowauza kina OX, Keita na Thiago juu ya kuwa ni Wagonjwa muda wote! Anachokifanya atakaa na Mido zake Gini-Fabi-Hendo, then hao kina Keita anachukulia kama ndiyo Depth ya Mido zake.
 
Naunga mkono kilichoongelewa hapa
Screenshot_2020-12-31-21-15-43.jpeg
 
Miongoni mwa sababu zilizonifanya niache kumlaumu Klopp hata kama sikubaliani na baadhi ya Falsafa zake ni kugundua kwamba Klopp ni sawa na Mourinho huwezi kuwabadilisha kwenye kile wanachokiamini.

Mourinho tokea nianze kumfahamu akiwa Porto ni muumini wa mpira wa kujilinda wala hakuna wa kumbadilisha kwenye style yake hii.
Na Klopp tokea aje Liverpool amekuwa ni muumini wa kutumia beki za pembeni kutengeneza mashambulizi wala hakuna wa kumbadilisha kwenye style yake hii.
Sasahivi Timu zimeshamjuilia hivyo tukishuka tu Uwanjani wanamkaba TAA na Robbo hapo unakuta tayari tumezimwa na hana Plan B ya kutumia Midos kwani Mido zetu hazina ubunifu wowote zaidi kurudisha mipira nyuma na kushindwa hata kudribble mtu mmoja.
 
Heri ya mwaka mpya waungwaa Wote
Nahisi hatupo Serious na Ubingwa msimu huu japo ubingwa wenyewe unatupendelea
Asante sana kheri ya mwaka mpya pia..

Ubingwa upo mikononi mwetu endapo tu nafasi chache tunazopata zitakua magoli na huku Allison kuendelea kutulinda kutopoteza mechi...

Pamoja na kukataa tamaa kwa wengi juu ya matokeo hafifu tunayopata binafsi naona hatupo vimbaya sanaa..

Ifahamike usajili uliobadili hii timu na kutufanya serious contenders na hatimae kushinda vikombe hivi ni..
Aliison

VVD

Fabinho

Salah...

Kwa sasa hawa wawili hawapo VVD majeruhi na Fabinho hachezi nafasi yake hivyo tunakosa output yake pale kati..

Naamini timu yoyote yenye kikosi cha wastani kama yetu wangeteseka kuwakosa star performers wake kama ambavyo tunateseka sis japo tunakocha mwenye system inayowafanya wachezaji kung'ara hakika tushukuru kwa hilo..

In everything give thanks...

Future is bright...

YNWA
 
Wakati City anchukua ubingwa kwa tofauti ya Point moja

Christmas na mwaka mpya

Liverpool alikuwa anaongoza League

Movie inendeleaaa....!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom