Huwa nawashangaa sana mnaposema "anfield"
Sijajua huwa mnakuwa mnajifariji
Si juzi Atalanta kapress hapo anfield mkala gori mbili
Mbona mnapenda sana kujificha "anfield "
Overrated pitch
Mkuu jitahidi uwe unaangalia na mechi za anfield,sio tu unaletewa matokeo.
Mkuu mechi karibia zote za anfield kwenye epl tumecheza vizuri sana yaani tuna kuwa tunashinda Halafu tunakuwa tumeupiga mwingi sana.sio ushindi wa kubahatisha.
Ndio maana kila mtu anakuambia anfield liverpool licha ya kishinda tu ila anaupiga mwingi sana.
Mkuu naona leo utakuwa wa kwanza kuamini kuwa anfield sio mahali salama kwa timu pinzani.
Msimu ulipita ni burnley peke yake alijitahidi akapata point 1, wengine wote walikufa pale. Msimu huu hakuna atakae chukua point hata moja pale anfield, na dalili zinaonekana.
Hata kama timu inapata ushindi uwe unaangalia na huo ushindi wake,mfano ushindi wa Chelsea kumbe alikuwa anakutana na timu zipo nje ya top 12, sasa hivi anakutana na timu zipo ndani ya top 12 anafungwa mechi mbili mfululizo watu wanaona timu inazingua .
Ushindi wa anfield kwa liverpool hauna mashaka yoyote.
Game ya kwanza na atalanta tulimfunga 5 bila nyumbani kwake,mechi ya marudio kocha kazarau mechi yule aliyewapiga hatrick na wengine wakutegemewa waliwekwa nje Baada ya kufungwa goli moja zikafanyika sabu 5. Ikawa too late,na sio kwamba tulizidiwa.
Hicho ndio kilichotokea kwenye mechi na atalanta.
Sasa spurs na wengine huko tunapo enda sijao wakipata msamaha pale anfield.