Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Shame....
Tujiandae kwa kelele.....
Hii kipigo sikuwahi kufikiri mwamba kwa liverpool hii ingeweza kuwa mdebwedo kwa kiwango hiki.

Heddo angecheza tusingepigwa goals zote hizo. Jamaa anajua ku control tempo ya game. Ikiwa ya moto anaipooza. So pengo lake naliona wazi kabisa.

Tumemkosa Mane farward line ikapoteA makali. Nilale tu maana kelele Itakuwa nyingi kwa week nzima.

Poleni kops wooote. Msisahau kumpa mh Lissu kura hapo 28/10
 
Wana Liverpool HALISI tumepoteza mechi,tena tumepoteza kwa aibu LKN tusikate tamaa,ndiyo soka!
Tuache wanao tukana team hapa wafanye hivyo,sisi tuendelee kuwa nyuma ya team.
Klopp atafanya mabadiriko tutakuwa sawa.
 
You Will Never Walk Alone 😂😂😂

Kwa niaba ya Manchester United napenda kushukuru kwa kutembea na sisi weekend hii....hatujawalk alone,tumetembea pamoja na mmetushika mkono kabisa!
Huu ndio ubinadamu,kuwa pamoja katika shida na raha.....tumetambua mchango wenu na tumeshukuru!

You did it better than us!🤣🤣🤣
 
Ukitoa Salah na Robo .
Hakuna mchezaji mwingine alicheza kitu cha maana kikaoneka wachezaji hawana morali hata kidogo upuuzi .

Firminho ndio kaisha kabisaa hana jipya

Gomez ndo kakumbwa sijui na jini mahaba

Adrian king Ngwaba alituambia ni bora ya Karius ×100 nimeamini leo aise.

Yani huyu tokea aokotwe mtaani na kupewa Jezi ya Liverpool nimekuwa nikikosoa usajili wake na kusema bora Karius kuliko huyu! Lakini amekuwa akipatiwa utetezi wa Guinness World Records kuwa ametupa Super Cup.
 
Tumecheza vizuri hilo halina ubishi! Hata ukiangalia ushindi wa Aston Villa basi wameshinda kwa Tabu sana.
Goli 7 unasema wameshinda kwa taabu.visingizio havikosekani.wewe kubali kuwa mmefungwa kwa uhalali sio tena unaanza kusema mara hao kwa taabu
 
Siku Imekua Nzito Ivyi.

Inanitokeaga ivyi Kwenye Simba Sikujua Nitahisi Ivyi Kwa Liverpool

Lol!
 
Hii ndio hali halisi ya timu yetu kwa sasa,hata mechi tulizoshinda nilishawahi sema hapa, tumeshinda kibahati na wala si kutokana na uimara wa timu.Tuendelee kujifariji tu ila msimu huu hatuna chetu.
 
Hii balaa tena nyingine.
ab2df6f8-ddfe-42ab-920a-1ad3b3f06d3c.jpg
 
Yani huyu tokea aokotwe mtaani na kupewa Jezi ya Liverpool nimekuwa nikikosoa usajili wake na kusema bora Karius kuliko huyu! Lakini amekuwa akipatiwa utetezi wa Guinness World Records World Record kuwa ametupa Super Cup.
Athari za homa ya Corona katika team LFC sio ya kufungwa hivyo
 
Wana Liverpool HALISI tumepoteza mechi,tena tumepoteza kwa aibu LKN tusikate tamaa,ndiyo soka!
Tuache wanao tukana team hapa wafanye hivyo,sisi tuendelee kuwa nyuma ya team.
Klopp atafanya mabadiriko tutakuwa sawa.
Tupo pamoja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom