ROBERTO FIRMINO "BOBBY" Striker Version.9.10.11.7.8.6
.
Roberto Firmino a.k.a "Bobby" mzaliwa wa pale Brazil nchi inayoliishi na kulipumua soka
.
Pale jiji la Maceió, jiji namba moja kwa matukio hatari ya utekaji, tattoo wanachora ata kwa wembe, amini usiamini, na ndipo alipotoa roho ya upambanaji
.
Mitaa ambayo cocaine ina bei sawa na karanga, Bobby aliuza madafu ufukweni uku akipiga danadana, mbona fresh tu, Brazil huku sisi tushazoea

.
Marcellus Portella daktari na mtaalamu wa meno (dentist) ndie aliemuona Bobby na kumpigania kupata timu akiamini ipo siku atacheza timu ya taifa, kitu ambacho ni kigumu na chenye heshima kwa waBrazil
.
Marcellus alimtoa Clube de Regatas ambapo alipokua daktari wa timu kisha akampeleka Figuerense, na kuanzia hapo akawa wakala wake na udaktari ukabaki kwenye vyeti, hiyo ndo power ya football
.
Baadae 2014 akaenda Hoffenheim pale Germany, anafunga goli 16 anachukua ile tuzo ya "Best Breakthrough Player Award"
.
2015 akaenda Liverpool, Liver yenye Benteke, kocha Brendan Rodgers winga ya kulia, pia nyuma ya striker, ila haikuwahi fanikiwa kupata chemistry na Benteke
.
Anakuja Jurgen Klop yule Benteke kando, akampa Firmino role ya false 9, toka hapo amekuwa muhimu zaidi safu ya ushambuliaji
.
Bobby hakupi goli 20+ ila anakupa kitu ambacho hakuna striker mwingine anakupa, ni version mpya ya striker, anakuja chini anakaba, anapiga pasi na assist
.
Watu wa IT wamempa code name V.9.10.11.7.8.6 hizo namba hapo Bobby ndani ya mechi moja anafika pote na anafanya kazi zake
.
Maisha ya soka alianza kama kiungo mkabaji, ila kipingi yupo katika majaribio "trial" Figuerense alifunga tikitaka mbili, kuanzia hapo akawa striker
.
Anavyo nyumbulika ni kama hana kiuno, mguu kama hauna ankle vile, macho ya ki'Asia, roho na tabasam la ki'Palestina
.
Karibuni amekuwa mfungaji wa magoli muhimu, tangu Club World Cup hata usiku wa jana, timu ilicheza kawaida tu ila don't worry, you got Bobby, Bang

Game Over
.
Bobby ni King of Celebrations, smile lake linatoa harara, yale meno meupe kwenye jua akikenua anakuumiza macho

, sababu amelelewa na dentist sasa kwanini meno yasing'ae
.
Ana Speed, Control, Vision.
Sent using
Jamii Forums mobile app