Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Kwenye hili Group tunapita ila concern yangu ni je tutaongoza hili kundi?

Kuongoza kundi kuna faida yake pale utakapoingia 16 bora na mpinzani utakayekutana nae! Kama hukuongoza kundi manake utakutana na kigogo atakayeongoza kundi.
Sijawahi kuwa na wasiwasi wa nani tutakutana nae after makundi hata miaka tuliyoingia fainali yote nadhani tulikuwa wa 2 pia. Hii mechi nilijua ngumu kutoka sababu napoli wangepania sana...ndo maana mwanzo nilisema asichoshe wachezaji apange tu akina lallana na shaqiri ili tumuwaze chelsea maana hili kundi tutapita tu. Hawa akina samatta hawana dili.lolote wala salzburg...ila ndo tushawachosha akina robertson na chelsea kala kidude atakuja na moto huyo balaa. Kama alivyotukimbiza kule kwenye supercup.
Ila nashukuru Kante atakuwa hajapona
 
Kwa nilichokiona mimi vs Naples

Wanatufunga kwasababu Plan yao ya kwanza ni Kidhibiti Midfield (Due to our incompetent Midfield) kuhakikisha Kati wanatawala wao ili waweze kuwa na 3 alternatives za kufanya Mashambulizi.
Kutokana na kudhibiti Mido yote basi Mido zao wanaweza kuanzisha mashambulizi upande wa kulia, au upande wa kushoto, au kupitia kati moja kwa moja.

Pia sababu nyengine ya kutufunga ni kwamba kila game wanakuwa na game plan ya kumshut down completely TAA kwani wanajua ndiye threat kwa mpinzani! So, leo wamefanikiwa tena kumzima kama last season asiweze kupanda juu na kitengeneza nafasi.

Pia jambo jengine ni kwamba leo Bobby hakuwa katika ubora wake na huku Koulibaly alikuwa anakwenda na Salah toe to toe pale anapokaribia kwenye 18..
Kutokana na kutokuwa vizuri kwa Bobby pamoja na kukabwa kwa Salah, basi na Mane akawa anapotea kirahisi.
Liverpool hamko serious mtu ana Allan pale kati wewe una herndason unategemea kushinda?
 
....hahahaha "marehemu alikua mbabe jamani"

Hii gemu sijaangalia nikijua Liva anashinda nikajikalia zangua nacheza PES mara nasikia msiba.
Napoli msimu uliopita walimtwanga uyo Liverpool wako sasa ulijuaje watafungwa?
 
Nilipitia baadhi ya Comments kuna nyengine zinasema Hendo na Milner walikuwa wanatesa pale kati! Dah kweli tunatofautiana kwenye kuangalia mpira!
Yani Napoli wamezuia dimba la kati kwa dakika zote 90 halafu anatokea Mtu anasema tulikuwa tunatesa pale kati???
tell her
 
Kwenye hili Group tunapita ila concern yangu ni je tutaongoza hili kundi?

Kuongoza kundi kuna faida yake pale utakapoingia 16 bora na mpinzani utakayekutana nae! Kama hukuongoza kundi manake utakutana na kigogo atakayeongoza kundi.
Sasa tunaanza ramli Napoli apoteze moja na sisi tushinde gemu zote zilizobaki kwa magoli mengi tu ili tuongoze kundi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom