Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

kaka
Kuna watu wanashindwa kufahamu kile anacho-offer Salah uwanjani ni nini Bali wanaangalia tu kwanini hakumpa pasi Mane!

Hivi unadhani Timu zikicheza na Liverpool wanakuwa Concerned na Bobby au Mane?
Tumeshawahi kucheza game Mabeki wakawa Man marking na Bobby au Mane?

Timu yoyote tunapoingia uwanjani basi wanayemuangalia kama ni Threat ni Salah! Sasa mchezaji kama huyu anayeteka Tenshen za watu juu Yake na wengine wakapata nafasi unasema aondoshwe au aekwe bench kisa tu alikuwa Selfish?

Watu wanasahau kuwa hayo Magoli wanayofunga Kina Mane na Bobby nusu Yake yanatokana na Mchango wa Salah.
ukipata nafasi uwe una peruzi na forum za team zingine mara moja ili uweze kufahamu maoni zaid kuhusu wachezaji wako nje ya mapenzi binafsi yq liverpool..mfano chini
spurs(thefightingcock.com)..wanamwogopa mane kuliko salah
mancity(bluemoon.com)...ikikaribia mechi na wao akili ipo kwa mane,wakiomba walker aamke vizuri kweli)
na pia vs barcelona recently ni mane aliyetubeba single ended na kusababibisha origi awe free kuperform na hakujali kama alifunga yeye au la..wakati hapo salah angetaka kuwa kama messi
 
Mkuu huwezi bishana na mtu ambae alishafikia sehemu akaandika NO SALAH NO LIVERPOOL.. tuache tu yapite sababu tumepata ushind ila kuhusu mchango wa mane na salah kila mwenye macho na akili nadhani anaona ni Nani tishio la timu pinzani.
 
Guadiora alikuwa anamuacha aguero nje anampa nafasi Jesus...unasemaje angeshindwa kumpumzisha Salah Kama Ana mtu wa uhakika!!??Guadiora Ana uthubutu ambao klopp Hana na huo ndio ukweli mchungu...plus sisi kwa hapo mbele hatuna mbadala wa uhakika ndio maana huyo Salah anafanya uhanithi
nadhani hili udhubutu wa Klopp ni kutokana na ufinyu wa kikosi maana hata akisema akae benchi ni dhahiri wengine lazima wa upgrade thier goal ratio kwa bahati mbaya huo muda haupo we are gunning for EPL sio trial basis..

Salah bado ni moto sana anahitaji kuangalia zaidi mahitaji ya timu kuliko mafanikio yake binafsi...Mane kuna kipindi 2017-2018 tena alitucost FA vs Westbrom na pia akaja akatucost point msimu huo huo vs Everton kwa mambo haya haya anayofanya Salah sasa hivi...

Salah attitude lazima ibadilike he is the best that one we know but he needs his forward partners in good blood sio mibifu isiyo na tija...
 
Mechi 4 za August tumeua na kuchota points zote 12. Sasa tunaingia September kuna mechi kama 3 hivi napo tuendelee kuuwasha tu moto tuchukue points zetu zote 9 na kuweka hesabu zetu sawa ili tuingie October na target kali sana
hilo ni muhimu sana ndugu maana kuanzia December na kuedelea tuna mechi nyingi mno na pia wear and tear itakua ishaanza kuwakamata wachezaji hivyo tunahitaji pointi nyingi mapemaaaaa
 
Nakubali Salah kafanya Ubinafsi lakini si sababu ya kuwa eti Auzwe au awekwe Bench! Huo utakuwa ni uzwazwa kabisa.

Mtu ana Magoli 3 na Assists 2 katika michezo 4 ya EPL unasema auzwe au aekwe bench kisa tu hakumpa pasi kipenzi chenu Mane? Hii ni too much sasa.

Tuwauzie basi Real au Man City
hilo la kuuzwa hapana, anarekebishika ni Klopp akomae nae na baada ya jana naamini Klopp atazungumza nae in length umuhimu wa team work....kazi yake ni kufunga na hua anafunga sana tu that we are thankful,....
 
Watu wanasema uselfish wake kuna Siku utaicost timu! Mbona magoli Yake hawayasemi kuwa kuna Siku yataisaidia timu?

Only selfish tu ndiyo tatizo lakini kufunga na kuassist sio faida?
hii ishu imeaubuka baada ya jana tu na nadhani kama Mane angejikalia zake kimya maneno haya yangekua machache...

Messi amekua akiongoza kwa assist na magoli Europe ni kwa sababu pale mbele wana opetate in the same mind, whoever is in proper position get thr ball to score sio just looking for self glory...

Salah is top top player what he needs ni kuanza kua a bit accomodating to his fellow forwards...and am positive ataongeza magoli na pia ukumbuke anavyotoa pasi anajiweka position nzuri ya kupenetrate arudishiwe pasi afunge that how Messi opetates...

Mane msimu wa 2017-2018 alikua mbinafsi zaidi ya Salah lakini alivyojitahidi kupunguza huo ubinfsi ameongeza magoli aliyofunga compared na 2017-2018...

Salah is still the best lethal we have in this squad..na hata assist bado yupo juu...he just need a bit of knowing Liverpool dreams of winning EPL cant rest on his shoulders alone bila ya team work we are done and done..
 
Ratiba yetu EPL ya September ni hii hapa

Ina mechi 3 tu ambazo zina changamoto kubwa ndani Yake

Saturday 14
Liverpool – Newcastle United

Saturday 21

Chelsea - Liverpool

Saturday 28

Sheffield United - Liverpool
lol the vs The Blues away...

na pia kuna Carabao na Champions league..
 
hilo la kuuzwa hapana, anarekebishika ni Klopp akomae nae na baada ya jana naamini Klopp atazungumza nae in length umuhimu wa team work....kazi yake ni kufunga na hua anafunga sana tu that we are thankful,....

Mimi niliyazungumza mengi baada ya kuona Mdau mmoja kapost kuwa eti Salah ni mchoyo auzwe!

Kuna mwengine kapost eti aekwe benchi!!!

Hivi huyu ni mshabiki wa Liverpool kweli anayetaka Salah auzwe halafu tumtegemee Origi na Xhaqiri kisa tu Mane Kanuna?

Huyu ni mshabiki wa Liverpool kweli anaetaka Salah aekwe Benchi achezeshwe Origi na Xhaqiri Kiss tu Mane Kanuna??

Hivi Timu inayotafuta ubingwa wa EPL inaweza kuwaza kumuuza au kumueka benchi Mshambuliaji hatari kama Salah ambaye Hakuna hata Timu moja Duniani isiyotamani kuwa Naye?

Shida Yote ni Kuwa Watu Wanaishi kwa Kukariri!! Eti wanasema Tilimfunga Barcelona bila Ya SALAH!!! This is bloody crazy!!! Wanazani Siku zinafanana kuwa Siku zote lazima itakuwa vile??
Au wanasahau kuwa Liverpool pia ishashinda bila ya Mane?

Yani Hawa Watu Waliomshambulia Ramos kumuumiza Salah kwenye Mechi ya Final vs Real na kulialia eti angekuemo Salah tungeliwafunga Real, ndiyo leohii wanaodai eti Salah aekwe Bench au Auzwe!!!!!

Hii issue sio kubwa kihivyo lakini Kuna Hawa Washabiki wa Liverpool kutoka Mkuranga ndiyo Akinuna Mane kwao ishakuwa balaa.
 
NO WAY KUMUUZA SALAH.....kwanza hilo linajulikana kwa wenye kufuatilia mpira Mane alikua kipindi fulani ni mbinafsi zaidi ya Salah alishatu cost point na exit ya FA hivyo ni suala linalorekebishika...

Binafsi nasema abakie tena sana Salah pia ni binadamu na twasema..human is to error...ishu hapa ni isiwe mazoea, kama Mane alipunguza na sasa kua tishio kwa kufunga basi naamini na Salah will work on this amicably...

We need this boys showing this HUNGRINESS as Mane did its healthy and good for the team...

Kwa hali hii kweli kombe la EPL linatuaaaa....

Chelsea walimtoa Diego na Morata mpaka leo wanahaha....Manu wamemtoa Lukaku na sasa hawasomeki tenaaa....

Salah suit us better...ukikumbuka tulipotoka kwa akima Baloteri, Aspas, Markovic nk utajua huyu mwarabu is the best we can wish and lucky he is here doing whats others couldnt even come near to offer....
 
Hawa wazungumzishwe hawa
 
Attachments

  • IMG-20190901-WA0011.jpg
    IMG-20190901-WA0011.jpg
    21.7 KB · Views: 24
  • IMG-20190901-WA0012.jpg
    IMG-20190901-WA0012.jpg
    16.2 KB · Views: 31
  • IMG-20190901-WA0013.jpg
    IMG-20190901-WA0013.jpg
    39.1 KB · Views: 26
  • IMG-20190901-WA0014.jpg
    IMG-20190901-WA0014.jpg
    18.3 KB · Views: 24
  • IMG-20190901-WA0009.jpg
    IMG-20190901-WA0009.jpg
    11.3 KB · Views: 23

Similar Discussions

Back
Top Bottom