Hivi hizi free kicks anazopigaga Messi na kuingia nyavuni huwa ni suala la kocha anafundishaje au ile ni Natural Instincts tu za Messi?!
Ule mkwaju wa Messi jana yadi 70,ananyoosha mguu mpira unatembea hadi pembeni juu mpaka kipa anaukosa hadi kambani...
Yaani ile Messi najiuliza anafanyia mazoezi mara ngapi?! Jamaa anajua mpira...nahisi hata kina Maradona hawakufikia uwezo na maajabu haya.
But,beki ya Barca ni mbovu mno...
Liver wangekuwa makini haswa Mane na Salah wangepata goli mbili muhimu jana.
Sioni Barcelona ikiizuia Liverpool second leg kupata goli...tena wakizubaa zinaweza rudi zote,japo nao Liver kumzuia Messi asifunge nayo itakuwa ni another task.
Anyways,timu bora imeshinda jana...
Shikamoo Messi bila kumsahau Mnyama Suarez....jitu liko on fire sana.
Vipi Van Dijk jana alikuwa benchi ama, sikumuona!!