Don Clericuzio
JF-Expert Member
- Dec 8, 2017
- 16,930
- 40,585
kweli Mkuu sisi Liverpool Halisi mipango yetu lilikuwa ni Kuchukuwa makombe Manne!
Lakini tulipotolewa Carabao basi mipango yetu ikawa ni kuchukuwa Makombe 3 kwani Carabao likawa la kipumbavu.
Tulipotolewa FA basi mipango yetu ikawa ni kuchukuwa makombe 2 ya EPL na CL kwani FA ni la kipumbavu 😀😀
Kunasiku nilicheka mpaka basi hapa!
Nakumbuka vizuri kuwa last msimu wa 2016/17 tulimkataa Moreno baada ya mechi ya kwanza kuchomesha goli 1 dhidi ya Arsenal tuliyoshinda 4-3
Basi Mliverpool Halisi alitukosoa na kusema hatujui chochote klopp najua zaidi! 😀😀
Msimu uliopita 2017/18 baada ya kusajiliwa Robertson pia tukamkataa Moreno na tukataka achezeshwe Robertson, Basi Mliverpool alituambia Klopp anajua zaidi kumpanga Moreno, sisi hatujui chochote Robertson hawezi kucheza mbele ya Moreno!
Lakini cha ajabu hapa kuna siku alikuja na mpasho wake kuwa eti 'Klopp katuumbua kupitia Robertson kwani tulimponda kuwa kanunua mchezaji kutoka timu iliyoshuka daraja' ha ha ha ha ha
Jamaa anageuza maneno kila sekunde..
Kuna siku atakuja kusema hapa kuwa Alisson katuumbua kwani tulimponda kusajiliwa kwake..![]()
![]()
Depression kaka, kuna watu raha yao ni kupenda kuchokoza watu ili tu uibuke ugomvi, na mkikaa kimya atakuchokoza yeye halafu atasema wewe ndo umemchokoza.
Naona watu wamemtenga sasa kila muda inabidi atupie single zake.
Sema kapata kampani ya Liverpool HALISI mwenzake DullyJr, featuring yao inanoga sana.