Don Clericuzio
JF-Expert Member
- Dec 8, 2017
- 16,930
- 40,585
Nimeelewa
Asante Malafyale kwa maelezo. Ni kweli Coutinho au mchezaji yeyote anayetegemewa na timu anatakiwa aondoke wakati aidha kuna mbadala au mwisho wa msimu. Ndio maana Hazard anasisitiza hataondoka katikati ya msimu Chelsea
Nadhani mimi mtaniona wa ajabu kidogo kutokana na hilo swala, simwoni jamaa kama msaliti isipokuwa alipigania kwenda sehemu alipoona pana maslahi kwake.
Kabla ya hiyo January jamaa aliomba kuhama mapema, that was July. Timu ikagoma kabisa na kuna bids kadhaa zilikataliwa mpaka transfer window ikafungwa. Ilipokuja nyingine timu zikafikia makubaliano jamaa akaondoka.
Wachezaji wanachukuliwa kama watumwa, tunasahau kwamba wako kazini, akiuzwa na timu tunasema ni business, akiomba kuondoka tunamwita msaliti.