Washabiki wa Liver hatuna haja ya kutukana wachezaji wala kocha, ni kweli haikuwa siku nzuri jana ila kuna mambo yakujifunza. ndio mechi ya kwanza kufungwa na tumefungwa away na team nzuri sasa mapungufu yameonekana kwamba system ya 433 tabu imekuwa kwetu tumeona tulivyoenda 4231 tukawa vizuri, ni wakati sasa wa Fabinho kuwa main hold midfield kuhusu Lovren hakuwa na game nzuri na tunajuwa Gomez majeruhi kwa hiyo hatuna choice kwa sasa na Arnold kapata shida jana lakini huyu ni kijana mdogo sana na kajitahidi na atakuwa vizuri tu, Nataka kujiuliza tukianza matusi kwa kufungwa na City je yangetukuta ya City kufungwa tena kwake na Palace halafu Leicester sio tungeshikiana mapanga. Liverpool tuko 4 points bado ni juu yetu kushinda mechi zetu na tuchukulie hii game imepita ila yako yakujifunza, na uhakika next game katikati tutawaona Fabinho, Gini na Keita or Shaqir na uhakika na hilo. YNWA