Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Yaani ukisoma Liverpool Echo utadhani ndo wanampangia kikosi Klopp, maana walipropose Trent Kupumzika na imekuwa hivyo.

Ngoja tuone game itakuwaje, hope tutashinda.
Huyu jamaa ntamtilia shaka sasa na mbinu zisizo badilika.

Kaweka beki imara hafu anampanga huyo mkimbiaji uwanjani dah. Leo kuna kazi ya kukaba nadhani mana kina milner watashindwa kupandisha mashambulizi kwa udhaifu wa Hendo
 
Hajiulizi kwanini Chelsea walivomchukua yule mwarabu salah hakutumika sana akauzwa mapema tu!!
Kama hujamuelewa ngoja nikueleweshe. Alichozungumzia hapo ni kwamba timu ni vizuri ikarecruit wachezaji ambao wameshazoea kuchukua makombe au hata kama hawajazoea basi kuwe na wachezaji ambao wameshachukua toka zamani. Hazard alikuna Chelsea kawakuta kina Didier wameshazoea mataji na yeye akaingia kwenye mfumo huo.

Unamsajili Shaqiri unategemea akupe nini huyu? Ni heri usajili anayetoka nje ya EPL Atleast anakuwa na motisha kucheza ligi inayotazamwa na sana ulimwenguni. Hawa wanakua na passion.
 
Jamani naangalia mpira hapa mbona Liver hatuna mashambulizi yoyote dhidi ya kuchezewa tu mpira, mmm tutatoboa kweli??
 
Jamani wachambuzi hebu mtusaidie huu mpira wa leo wa Liver una maana gani mbona sijazoea kuuona hivi, umekuwa slow, umepooza wala hauna hata madhara kwa timu pinzani.
 
Joe Gomez ndio amewekwa Right-Back

Huyu Kocha wetu huyu! Sema basi tu hamna namna. Right back wetu ambae huwa namuona yupo vizuri defensively ni Nathaniel Clyne
Ndio nafasi yake halisi, centre back ameanza kucheza siku hizi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom