SORRY TO LIVERPOOL FC,HAYA NDIO MAJIBU YENU.
Baada ya wiki iliyopita kutoa mtazamo wangu kuhusu udhaifu wa Liverpool fc ambao ninaamini utakua ni kikwazo kikubwa kwa wao kurudisha zama zao na kutwaa mataji,kuna maoni na maswali mengi sana wengi walihoji,hasa mashabiki wa Liverpool fc.
Nimeamua niwajibu hivi,
EDEN HAZARD vs Mo SALAH
Jibu ni jepesi tu,Hazard is the World Class player but Salah is not.
Daima hauwezi kumlinganisha mchezaji aliyeisaidia timu yake kutwaa kila aina ya kombe isipokua Champions league (2 Epls,1europa league,FA & league cup) na mchezaji asiye na kikombe chochote katika ligi kubwa ulaya.
Kama ni tuzo binafsi,basi tuzo alizopata Salah msimu uliopita karibu 98% Hazard alishaanza kuzichukua zamani tu,so the answer is so simple.
LIVERPOOL FC HAINA "WORLD CLASS PLAYER"
Mwandishi wa gazeti LA the telegraph Chris Bascombe aliwahi kuelezea definition sahihi ya "world class player" japokua kumekua na discussions kuhusu hili.Katika makala yake aliyoiandika katika gazeti hilo Bascombe aliandika "World class player in football is that player in his/her position,He/She has a great consistency,outstanding consistency,outstanding quality & an ability to win a match for their side on a regular basis whether that from scoring memorable goals or producing defensive masterclass at the back".
Kwa maelezo hayo,Bascombe alihitimisha kwa kuandika Liverpool fc haina World class player.Bascombe kwa maoni yake anaamini Eden Hazard,David de Gea,Sergio Aguero & Ngolo Kante ndio wachezaji wenye sifa za kuwa World Class players pale England.
Liverpool fc imekuwa na wachezaji wengi wenye vipaji tena vipaji vya ajabu,niliandika wiki jana kuwa Mohammed Salah & Sadio Mane ni wachezaji wazuri wenye vipaji lakini bado si washindi.
Nilisema,binafsi ninaamini ili klabu itawale soka katika kipindi husika kwa kutwaa mataji mengi ni lazima i-recruit wachezaji washindi (winners),hasa klabu kubwa duniani kama Liverpool na Leo ninaongeza ni kweli inatakiwa iwe na Proven Goalkeeper,Proven Centreback,Proven Strickers & Bigger squad).
Liverpool fc wanakosa wachezaji ambao tayari wamesha-prove,wachezaji ambao ni washindi,wanajua jinsi ya kushinda na wamekuja kushinda,wenzetu wanasema Winners breed Wonders..Hakuna aliyesema Liverpool fc hawana timu nzuri lakini the discussion ni " calibre" yao.
Mfano,mechi kati ya Tottenham na Barcelona nilimuona mbrazil kinda Arthur Melo katika midfield lakini angalia Arthur anacheza alongside Sergio Busquet,Ivan Rakitic,Messi nk,,jiulize Confidence anayopata yule kijana,ukimkuta Arthur wa miaka mitano ni Xavi mpya,hiki ndicho wanachokosa Liverpool fc,wachezaji wote ni wakiwa,hakuna mshindi,tena wametoka timu ndogo zisizo na mategemeo ya ubingwa kama Virgil Van dijk kutoka Southampton,Sadio Mane kutoka Southampton au Roberto Firmino ambaye bado anajifunza namna na kutwaa mataji,je anajifunza kwa nani hapo Anfield?...Liverpool lack Winners na sioni nafasi kubwa kwao kutwaa taji wala kurudisha enzi zao.