Rajab_Omar
JF-Expert Member
- May 15, 2016
- 16,480
- 27,185
Yani Weekend Ninamuonea Huruma Soton sijui Tutamfanyaje!!
Hahaha, ndoto yako imetimia naona.Hakika nimeliona goli la Mbappe...View attachment 870491
Ndo tushashnda na mpira tumemilikiMmeponea liverpool ilikua sare kabisa aseh
Labda nikunong'oneze tu, ni kwamba Liverpool watashinda goli 4 kwa bila kule uwanja wa PSG, ukumbuke hii sentensi brosuper sub...huyu jamaa namkumbali sana...rarely anapata sifa zinazomstahili but he is the real deal..
haters wamenywea maana vitisho tutafungwo sijui 3, 5 hakuna..
Hii ndio Liverpool bana kupambana mpaka dakika ya mwisho
Umejuaje wee mhuni maaaniselanina walahi, umeongea Maziwa tupuKuna nyakat unaweza ukawa unapitia magumu lakn ukikumbuka kumbe Kuna mfariji ambaye kamwe haachi kukupa tabasamu na ukasahau magumu yote hakika LIVERPOOL MMENIPA FARAJA NA KUYASAHAU YOTE
Tumepona au tumeshinda mkuuMmeponea liverpool ilikua sare kabisa aseh
almanusura iwe sare anyway hongereni liverpoolTumepona au tumeshinda mkuu
Heb toa pongezi
Almanusura iwe 4:1almanusura iwe sare anyway hongereni liverpool
Kona 13 kwa 1Kops tumewazid kila kitu PSG
Shots, on targets, passes, corners,
Huyo kocha alikufa dakika kama hizohizo akiwa na BVB hapohapo Anfield tena referee akiwa huyohuyoalmanusura iwe sare anyway hongereni liverpool
Kona ya Anfield
Tuchel na Cakir ndio wanaoijua Anfield, siyo Neymar
Bill Shankly 1892
USIKU! Yes Usiku wa Alhamisi ya April 14, 2016 ndio usiku pekee wa kusisimua kuwahi kutokea katika dimba letu la Anfield. Usiku uliokuwa na jasho, damu na machozi. Usiku wa vita.
Usiku ambao Borrusia Dortmund yake Thomas Tuchel ilikutana na maajabu ambayo AC Milan na West Ham kwa nyakati tofauti iliwahi kukutana nayo mbele ya Liverpool kwenye viwanja tofauti.
Ni usiku ambao mwamuzi Cuneyt Cakir kutoka Ugiriki alipuliza kipyenga cha mwisho huku Dunia ikishuhudia Liverpool ikiibuka na ushindi wa magoli 4-3.
Hujanielewa bado: Huu ulikua ni mchezo wa second leg hatua ya robo fainali kati ya Liverpool na Dortmund. Mchezo wa awali ulimalizika kule Ujerumani kwa sare ya bao 1-1.
Unabakia kuwa usiku wa maajabu kwa namna ambavyo Liverpool ilitoka nyuma na kuibuka na ushindi.
Tayari kikosi cha Tuchel kilishatanguliza mguu mmoja nusu fainali lakini goli la dakika ya 90+1 kutoka kwa beki Dejan Lovren likashuhudia vijana wa Jurgen Klopp wakipindua matokeo.
Wakati huu ambao unajaribu kunielewa nikueleze kwamba kesho Tuchel anarejea tena pale Anfield. Safari hii anakuja na PSG katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi.
Tuchel anaielewa atmosphere ya Anfield anajua namna ambavyo yeye na wanae wa BVB walikutana na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki, watu wa Liverpool na wachezaji wake ndani ya uwanja.
Ubora wa Liverpool huanzia nje ya uwanja ilipo mitaa ya 11th Street Pub hadi St Elsie..huwa hatupoi..tunakinukisha ile kinoma na Tuchel anajua hilo.
Sasa punde tu baada ya makundi kupangwa staa wa PSG, bwa'dogo Neymar alikaririwa akiitupa nje ya mbio za ubingwa wa EPL, Liverpool. Kwamba anatuchukulia poa.
Hapa ndipo hasira zetu dhidi ya PSG zilipozidi na kwa sababu huyu mtoto hajawahi kutua Anfield nafikiri ni vema angemuuliza Tuchel nini alichokutana nacho.
Mtu pekee tofauti na Tuchel ambaye anaweza kumueleza Neymar ugumu wa kucheza na sisi kwenye uwanja wetu wa nyumbani hasa linapokuja suala la usiku wa Ulaya basi ni Cakir.
Huyu ndie refa ambaye pia kesho atachezesha pambano letu na PSG, anajua watu wa Anfield walivyo, anaijua roho ya kipiganaji tuliyonayo. Pengine anawaonea huruma PSG kimoyo-moyo.
Kinachofurahisha ni kwamba PSG wamekuwa na rekodi mbaya pindi wanapokutana na refa huyu ambapo hawajashinda kwenye mechi mbili ambazo Cakir alisimama katikati.
Sisi tuna bahati nae, tuliichapa Dortmud ya Tuchel yeye akiwa katikati ya uwanja hivyo hatuna shaka na nyota yake kwetu.
Niwasihi mabeki wa PSG wakiongozwa na babu Thiago wawe makini spidi waliyonayo wale wakorea weusi wetu kule mbele si ya kitoto.
Wasidhani tutaleta utani hata kidogo, Bobby Firmino imethibitishwa kuwa atacheza na jicho mojabaada ya kuumizwa na Vertogen juzi Jumamosi.
Hatuna shaka na hilo msimu uliopita alipiga magoli manne bila kuangalia goli 'no look' nini game moja na PSG? Waleteni hao matozi bwana!.
Eddie Cavan na Mbappe wanapaswa kutambua uwepo wa Le Commandment Field Marshall, Virgil Van Djik kule nyuma. wakumbuke wanacheza na beki ghali duniani.
Neymar huyu hatoamini jinsi ambavyo Trent Anord atamficha ndani ya viatu vyake vya Armour Magnetico..nawahakikishieni alichokutana nacho Gaucho kwa Arbeloa miaka 10 nyuma ndicho huyu tozi atakutana nacho.
Tukutane Anfield saa hizi hapo 21:45 InShaaAllah