Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

HAYA ule utamu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya umerudi tena. Safari hii mambo ni moto kwelikweli, maana ile hatua ya makundi tu inaanza, Liverpool inakipiga na Paris Saint-Germain.

Unaambiwa hivi, huo ni mtihani mzito kwa Kocha Jurgen Klopp, ambaye atapima kikosi chake kama kweli kipo vizuri kwa mapambano mazito baada ya kushinda mechi zake zote tano za kwanza kwenye Ligi Kuu England.

Mechi hiyo ngumu itapigwa leo Jumanne uwanjani Anfield, ambapo kutakuwa na shughuli nyingine pevu huko San Siro, wakati Inter Milan itakapoikaribisha Tottenham Hotspur.

Mechi nyingine kali itazishuhudia AS Monaco ikikipiga na Atletico Madrid, wakati Barcelona itakuwa na kibarua na PSV, huku Club Brugge ikiwa na kasheshe la kuikabili Borussia Dortmund na FK Crvena Zvezda itacheza na Napoli.

Kesho Jumatano kutakuwa na mechi nyingine kali kwelikweli, wakati Manchester City itakapocheza na Lyon, huku Real Madrid ikicheza na AS Roma. Man United nayo itaanzia ugenini kwa Young Boys, wakati Valencia itacheza na Juventus, huku Viktoria Plzen itacheza na CSKA Moscow na Shakhtar Donetsk itacheza na Hoffenheim. Kesho Jumatano pia kutakuwa na mechi kati ya Ajax itakayokuwa nyumbani kucheza na AEK Athens na Benfica itakipiga na Bayern Munich.
 
Kona ya Anfield

Tuchel na Cakir ndio wanaoijua Anfield, siyo Neymar

Bill Shankly 1892

USIKU! Yes Usiku wa Alhamisi ya April 14, 2016 ndio usiku pekee wa kusisimua kuwahi kutokea katika dimba letu la Anfield. Usiku uliokuwa na jasho, damu na machozi. Usiku wa vita.

Usiku ambao Borrusia Dortmund yake Thomas Tuchel ilikutana na maajabu ambayo AC Milan na West Ham kwa nyakati tofauti iliwahi kukutana nayo mbele ya Liverpool kwenye viwanja tofauti.

Ni usiku ambao mwamuzi Cuneyt Cakir kutoka Ugiriki alipuliza kipyenga cha mwisho huku Dunia ikishuhudia Liverpool ikiibuka na ushindi wa magoli 4-3.

Hujanielewa bado: Huu ulikua ni mchezo wa second leg hatua ya robo fainali kati ya Liverpool na Dortmund. Mchezo wa awali ulimalizika kule Ujerumani kwa sare ya bao 1-1.

Unabakia kuwa usiku wa maajabu kwa namna ambavyo Liverpool ilitoka nyuma na kuibuka na ushindi.

Tayari kikosi cha Tuchel kilishatanguliza mguu mmoja nusu fainali lakini goli la dakika ya 90+1 kutoka kwa beki Dejan Lovren likashuhudia vijana wa Jurgen Klopp wakipindua matokeo.

Wakati huu ambao unajaribu kunielewa nikueleze kwamba kesho Tuchel anarejea tena pale Anfield. Safari hii anakuja na PSG katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi.

Tuchel anaielewa atmosphere ya Anfield anajua namna ambavyo yeye na wanae wa BVB walikutana na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki, watu wa Liverpool na wachezaji wake ndani ya uwanja.

Ubora wa Liverpool huanzia nje ya uwanja ilipo mitaa ya 11th Street Pub hadi St Elsie..huwa hatupoi..tunakinukisha ile kinoma na Tuchel anajua hilo.

Sasa punde tu baada ya makundi kupangwa staa wa PSG, bwa'dogo Neymar alikaririwa akiitupa nje ya mbio za ubingwa wa EPL, Liverpool. Kwamba anatuchukulia poa.

Hapa ndipo hasira zetu dhidi ya PSG zilipozidi na kwa sababu huyu mtoto hajawahi kutua Anfield nafikiri ni vema angemuuliza Tuchel nini alichokutana nacho.

Mtu pekee tofauti na Tuchel ambaye anaweza kumueleza Neymar ugumu wa kucheza na sisi kwenye uwanja wetu wa nyumbani hasa linapokuja suala la usiku wa Ulaya basi ni Cakir.

Huyu ndie refa ambaye pia kesho atachezesha pambano letu na PSG, anajua watu wa Anfield walivyo, anaijua roho ya kipiganaji tuliyonayo. Pengine anawaonea huruma PSG kimoyo-moyo.

Kinachofurahisha ni kwamba PSG wamekuwa na rekodi mbaya pindi wanapokutana na refa huyu ambapo hawajashinda kwenye mechi mbili ambazo Cakir alisimama katikati.

Sisi tuna bahati nae, tuliichapa Dortmud ya Tuchel yeye akiwa katikati ya uwanja hivyo hatuna shaka na nyota yake kwetu.

Niwasihi mabeki wa PSG wakiongozwa na babu Thiago wawe makini spidi waliyonayo wale wakorea weusi wetu kule mbele si ya kitoto.

Wasidhani tutaleta utani hata kidogo, Bobby Firmino imethibitishwa kuwa atacheza na jicho moja baada ya kuumizwa na Vertogen juzi Jumamosi.

Hatuna shaka na hilo msimu uliopita alipiga magoli manne bila kuangalia goli 'no look' nini game moja na PSG? Waleteni hao matozi bwana!.

Eddie Cavan na Mbappe wanapaswa kutambua uwepo wa Le Commandment Field Marshall, Virgil Van Djik kule nyuma. wakumbuke wanacheza na beki ghali duniani.

Neymar huyu hatoamini jinsi ambavyo Trent Anord atamficha ndani ya viatu vyake vya Armour Magnetico..nawahakikishieni alichokutana nacho Gaucho kwa Arbeloa miaka 10 nyuma ndicho huyu tozi atakutana nacho.

Tukutane Anfield saa hizi hapo 21:45 InShaaAllah
ahahhaahah imebidi ni like tu hata kama sio shabiki wa Liverpool. Shime shime yasije watokea ya msimu ule na madrid. vinginevyo kila la heri
 
Klopp ameshindwa nini kuchukua kombe lolote hata "Yale ya mbuzi" wakati aliweza kuchukua ubingwa alipokuwa Bundesliga? Nini kimemshinda kwenye EPL? Achana na Sarri ambaye hajawai kubeba kabisa.

Twende na Klopp, kwanin ameshindwa EPL wakati Bundesliga aliweza?
Akikujibu unitaq.
 
Kila siku nyinyi mnapima uwezo na kujenga timu hatari Sana hii. Inamaana bado hamuamini mabeki wenu.

Mkija ugenini muwe mnaweka hashtag za kujitambulisha, maana naona mnabwabwaja bwabwaja, unamuuliza mgeni mwenzio aliyeandika utumbo.

Hivi Uefa mnacheza lini? Au ndo inabidi mshinde kwa majirani kuwanga ili tuwe wamoja.

Huu msimu mtaumiza nafsi kwa kuchukia kitu kizuri.
 
Klopp ameshindwa nini kuchukua kombe lolote hata "Yale ya mbuzi" wakati aliweza kuchukua ubingwa alipokuwa Bundesliga? Nini kimemshinda kwenye EPL? Achana na Sarri ambaye hajawai kubeba kabisa.

Twende na Klopp, kwanin ameshindwa EPL wakati Bundesliga aliweza?
Mpaka sasa hajashinda EPL lakini hajashindwa kwasababu bado yupo anashindana
 
Chelsea katika Harakati Zao Za Kucheza Mechi Za Futuhi (Kila Alkhamis) Wameamua Kujibabaisha na Kuanza Kukomalia Timu Za Watu Zinazoshiriki Ligi Ya Wanaume Ya CL.

Lakini Watambue Tue Kuwa Liverpool Kamwe Haiwezi Kutolewa Hatua Ya Makundi.

Hata Kama Leo itafungwa basi Wajue Mechi ya Leo sio Knockout Stage Bali Kuna Mchezo Mengine inafuata.
 
Haya Maneno Mengine Ni Tofauti Na Kinachotokea Uwanjani. Lakini Game Ya Leo Tutaprove Kama Anachoongea Salah Ni Sahihi au sio Sahihi.

Salah on bond with Mane/Firmino: “There's a real solidarity between us because we don't worry about who's going to score the most or first. Each of us works so that the others score. And as you have seen, we all score." #LFC
 
Haya Maneno Mengine Ni Tofauti Na Kinachotokea Uwanjani. Lakini Game Ya Leo Tutaprove Kama Anachoongea Salah Ni Sahihi au sio Sahihi.

Salah on bond with Mane/Firmino: “There's a real solidarity between us because we don't worry about who's going to score the most or first. Each of us works so that the others score. And as you have seen, we all score." #LFC

Nachofurahi ni kwamba ujumbe umewafikia kutoka kila pande ya dunia, ibaki ni akili zao wenyewe.

Nategemea kuona mabadiliko leo.
 
Ukiiangalia Hiyo Video Yapili Hapo Chini Utamuona Na Gini jinsi alivyofanya Ubinafsi Wa Kutotoa Mpira Kwa Wenziwe na Tukapoteza Nafasi.

Ni wazi Kuwa Wachezaji Wetu Wanacheza Kwa Ajili ya Mtu Kufunga na Hawachezi Kwa Ajili ya Timu Kushinda.

Cha kushanga juzi kwenye Instagram Gini Ali like one of the comment written by shabiki wa Liverpool kuponda igotism ya mane yaani uselfish

in no minutes akadete na akapost kua Ali like kwa bahati mbaya!

very strange!!!!
 
Leo Nipo Upande Huu

InshaAllha Waenda Tenda Maajabu Watu Wazidi Shangaa
 
Mkuu Unajua Kwanini Tumeconcede Magoli 2 tu Mpaka Sasahivi?
Moja Ya Sababu Ni Kuwa Tumepigiwa Shuti Chache On Target jambo ambalo maranyingi Alisaon Anarelax na Kucheza Zile Back passes anazorudishiwa.

Na Moja Sababu ya Sababu Ya Kuface On Target Shots chache Si Ubora Wa Beki tu Bali Kuna Kazi Kubwa anayoifanya Gini na Milner.

Sasa Mchezaji Kama Hendo Ndiye Aliyekuwa Chanzo Cha sisi Kupigiwa On Target Nyingi Na Kuconcede Magoli Mengi Kutokana na Yeye Kutokuwa na Uwezo Wa Kulinda Hata Kidogo Bali Alikuwa Akitukaribishia Mashambulizi Kwa Kwa Kucheza Miback passes yasio na Sababu.


Yule alikuwa mtu wa Sub, Waingereza kama kawaida yao kutetea na kumlinda muingereza mwenzao hata kama uwezo hana ni kama jadi yao. Hii nimeiona sana mitandao yote ya kijamii, watetezi wakubwa wa huyu jamaa ni waingereza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom