Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

well said Mkuu nimekupata vyema.....ingekua poa na sasa mashabiki wa Majogoo hapa JF tusambaziwe medal zetu hehehe..
 
Na Kizuri Zaidi Mashambulizi Yao Mengi Real Wanamtegemea Marcelo! Sasa Tukikutana Basi Marcelo na Aje Ashambulie Amuache Mo Salah Peke Yake aone Segere...


Na Akimkaba Mo Salah Basi Atauwa Mashambulizi na Hatimae Ronaldo Atageuka Mzururaji tu.
Yaani kama uko kwenye akili yangu natamani sana game ya liver na Madrid tunataka kuinyamanyisha dunia
 
Naona watu wanakariri sana mpira

Kosa sio kumtoa Salah ila hayo ni matokeo ya mpira na lazima tuujue na sio kuukurupukia.

Roma wangeweza kupata magoli ata Salah alipokuwepo uwanjani. Tayari watu wamesahau kuwa dakika 20 za mwanzo za mchezo Roma ndio walionekana kuwa hatari zaidi, je Salah hakuwepo uwanjani??

Wewe mpenzi wa mpira unayesema mechi bado mbichi huku moyoni mwako unasema Liverpool bila Salah ni nyeupe je huko kwao Roma Salah hatocheza?? Jibu ni kwamba atacheza.

Mnasahau kuwa Liverpool ni mabingwa mara 5 ulaya huku wakiwa na historia nyingi za comebacks ambazo huyo Roma hana. Kuwafunga Chelsea na Barca kwao sio kipimo cha ubora.

Wewe shabiki wa mpira unayekaa ukiwa na mtazamo wa mwelekeo mmoja nataka nikukumbushe tu kuwa, Liverpool ndiyo timu pekee ambao ina wastani wa kufunga angalau magoli matatu katika mechi za ugenini msimu huu wa UCL.

Hii post naiandika kishabiki ila na facts tupu. Unaposema kuwa Liverpool ina beki mbovu je unataka kusema kuwa beki nzuri huwa haifungwi magoli?? Je unataka kusema kuwa wao Roma waliweka wale washambuliaji wao wafanye jukumu la ulinzi au la kushambulia??

Unaposema Liverpool inabeki mbovu huku kuna timu mnazoamini kuwa zina beki bora kabisa na zimeshatolewa tunakuwa hatuwaelewi na tunakuwa na mashaka na uwezo wenu wa kuujua mpira.

Ndio mpira una maajabu yake na Roma wameweza kufanya msimu huu kwa kumtoa Barca ila niwaambie tu maajabu ya mpira sio Comebacks bali kuna maajabu mengine ya kufungwa nyumbani na ugenini kwa goli nyingi na hayo pia yatafanywa kwa Roma pia.

Ili Liverpool isikufunge basi cheza mipira ya kihuni huni ambayo haina utaratibu kama ya yule mwimbisha kwaya ya taarabu kikundi cha Old Trafford. Ukija wote tucheze mpira kwa faida ya mashabiki my friend hii Liverpool haitokuacha Salama.

Narudi kwa nini Salah anatoka: Salah kwa sasa ndo Star player wa timu ni lazima kocha amlinde.

Umeshaongoza goli tano unachotaka ni kipi tena?? Je unataka aendelee kuwepo uwanjani ili aumizwe na mabeki waloijikatia tamaa??

Je unapokuwa na timu yenye kikosi finyu huku wachezaji wako tegemezi wengi ni majeruhi unatakiwa kufanya nini zaidi ya kuwalinda waliopo ili usiongeze majeruhi??

Risk ya kurudisha goli tano bila Salah ni ndogo sana kuliko risk ya kumpoteza salah kwa majeruhi. Ni kichaa tu ndo asingemlinda mchezaji wake bora hasa pale anakuwa Tayari katimiza wajibu wake.

Niwaambie tu kitu: Tatizo la magoli kufungwa anapotoka Salah uwanjani sio Salah kutoka bali tatizo ni wanaoingia kama mbadala wake.

Mchezaji anayembadili Salah haingii kufanya majukumu ya Salah zaidi anaenda kuikaba timu yake.

Niwakumbushe tu: Mechi bado mbichi sana kama mnavyosema na maajabu yatatokea ila hayo maajabu yatakuwa ni ya Roma kufungwa goli nyingi sana kwake. Ila msije mkageuka na kusema kuwa Roma hakustahili kucheza nusu fainali na wengine mtasema hii ni nusu fainali mbovu kabisa ya muda wote...!

Ila kweli Liverpool inabeki mbovu sana ila nashangaa imefikaje nusu fainali na ubovu huo inamaana timu zingine nazo hazijui kufunga. Bora kuwa na silaha unayoweza kuitumia kifasaha kuliko kuwa na ngao ambayo haiwezi ata kukuokoa vitani.

Jana tumetia mpapaso mechi ya pili tunakula kiboga sebuleni kwenye nyumba ya mshua wao (sisi watoto wahuni)

TUKUTANE KIEV.
 
Kikubwa nilichogundua hawa wenzetu wanaotupinga ni husda tu baada ya kuona timu zao hazijafika hatua hii mm nawafananisha na MTU ambaye kaz yake kumsifia baba wa mwingine akifanya vizur badala ya kuelekeza nguvu ya kumshaur baba yako mjue WAP. mlipoteleza hadi kuwa hivyo na mwaka huu mtahama sana timu mlikuwa fc Porto mkaja man city Leo mpo as Roma cjui final mtakuwa timu gani lakini nachowapongeza mmeanza kuwakubali wachezaji wetu Mmoja mmoja mwisho wa siku mtaikubali timu nzima karibuni LFC na mlio wengi ni mashabik wa miaka ya 2000 hamjui historia ya Liverpool kumbuken Liverpool is among of European giant si hivyo vitimu vyenu vya karne ya 21 ndio vimeanza kuona mafanikio
 
Lazima Liverpool tubadilishe Mfumo Wa Wages Kwa Baadhi Ya Wachezaji Kwani Ni Jambo la Aibu Kuwa Mchezaji Wa Bench Wa Manure anakula Hela Ndefu Kuliko Sadio Mane.

Mo Salah Katika New Contract Wanataka wampe £200K jambo ambalo not fair kabisa.
Kweli mkuu salah anastahili 250+ aiseee!
 
U23 mmoja wamliplace coutinho kijana wetu huyu naye apate medal goal zake zile 5 zina mchango mkubwa hadi kufika hapa tulipo
 
Kocha ambaye hajawahi kuchukua hata champions league mnamwita master class coach

Makocha wako waliochukua UEFA Champions League mbona wanamuogopa hawataki kukutana klopp Maana wakikutana vibarua vitaota nyasi .


Kakutananao hao waliochukua UEFA Champions League kawafunga tena kwa aibu ya mwaka
kwanini tusimwite master class?

Kama unataka achukue UEFA Champions League ndio safari hii anaenda kubeba.

Akili yako inadikilia Liverpool imefika hapo kwa kubahatisha, ujui mpira Mkuu kama unajua auangaliagi mechi za Liverpool.

Kwanza mlikuwa mnasema Liverpool hawana world class players,lakini ndio hivyo Liverpool inasonga mbele kwa nguvu ya klopp.

Mtu kama Milner uwezi kuamini ndio mwenye assist nyingi ndani ya msimu mmoja kuanzia wewe uanze kuijua UEFA Champions League.

Wachezaji alionao klopp akipewa makocha wako waliochukua UEFA Champions League hawata fika kokote wao wanataka world class players, Sasa kama Ndio hivyo kwanini klopp nisimwite master class coach?

Mtu kama robertson kamtoa hull city iiliyoshuka daraja msimu uliopita kwa paund mill8 tu, lakini Sasa Hivi robertson hakuna winga yoyote anayetaka akutane .

Amekuwa beki kisiki yaani solid, sasa kwanini nisimwite master class coach.

Na wachezaji anawabadilisha kulingana na mapungufu walioonyesha kwenye mechi iliyopita.

Mfano Huyu dogo TAA mechi na man u,man u walitumia upande wake iliwapitie huko,walifanikiwa na dogo kuonekana dhaifu,mechi iliyofuata man City wakaiga kupitia huo upande kilichowakuta hawakupata hata shot on target hata moja na biashara ikaishia hapo,maana sasa watapitia wapi?

Liverpool ijafika hapo kwa Bahati mbaya Mkuu klopp ni master class coach.
 
Unaambiwa msako wa Liverpool ni sawa na msako wa mgambo, ni mpelampela mwanzo mwisho..

Roma amefanya dharau sana kufunga magoli mawili pale Anfield, hii haitamwacha salama, lazima tumkandamize goli sio chini ya tatu pale pale kwenye ardhi yake.. Sisi ni Liverpool na tunatokea Merseyside sisi sio Barcelona na hatupajua Catalonia
 

Pale ambapo standard 7 anaomba form 6 asifaulu wawe wamoja.

Wanaanza vipi kuwa sawa?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…