Mambo yalikuwa magumu kwa Liverpool licha ya kuwashambulia sana wapinzani wao lakini waliambulia patupu dhidi ya West Brom
Liverpool hawajashinda mfululizo katika michezo miwili ya Ligi Kuu ya Ligi Kuu baada ya kutokana sare ya 0-0 na West Bromwich Albion huko Anfield.
Majogoo waliuanza mchezo kwa kasi kubwa kwa kulisakama lango la wageni huku wakitaka kupata goli la mapema.
Robert Firmino alipata nafasi ya wazi katika kipindi cha kwanza lakini umakini wake mdogo ndiyo ulisababisha Majogoo hao wasipate goli la kuongoza.
Westbrom wali jibu mashambulizi hayo kwani Hal Robson Kanu alipata nafasi karibu nyuma ya nyavu lakini mpira ulitoka senti mita chache baada ya kumpita mlinda mlango wa Liverpool Loris Karius.
Pamoja Sadio Mane, Firmino na Phillipe Coutinho kurejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuanzia benchi katika mechi ya wiki ilihopita, Liverpool bado hakuwa na makali katika eneo la kushambulia ili kusababisha matatizo kwa wageni.
Nyota bora wa Ligi na Liverpool, Mohammed Salah alipata nafasi nzuri lakini alishindwa kufunga baada ya krosi nzuri kutoka kwa Trent Alexander-Arnold lakini alishindwa kupiga kichwa kizuri ambacho kingeweza kuzalisha goli.
Majogoo waliwashambulia sana Westbrom katika nusu ya mchezo huku wageni wao wakifanya mashambulizi machache tu.
Jay Rodriguez alichukua nafasi ya Robson Kanu na Pardew aliafanya mabadiliko hayo kwa lengo la kwenda kuishambulia zaidi Liverpool.
Hata hivyo, Liverpool walidhani wameshinda mechi hiyo katika dakika za mwisho lakini goli alilofunga Dominic Solanke lilikataliwa kufuatia kuunawa mpira kabla ya kufunga
Hadi mchezo unamalizika Liverpool na Westbrom zilitoshana nguvu